Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Tatizo ni umasikini
Umasikini mbaya sana mkuu

Ungangali wa mtoto inategemea na wewe mzazi nyumbani, mtoto akirudi shule mpigishe kazi ndogondogo kama kujifulia nguo mwenyewe kulimalima vinyasi vinavyo zunguka nyumba,sio junia kaangalie katuni

anakomaa,kwasababu hata huko kayumba unako mpeleka ukimdekeza wenzake watamshika makalio
 
Q
Anadhani wazazi wanaouza viwanja kusomesha watoto ni wajinga.

Tuangalie mfano hai kwa Shilole ,aliweka bondi hati ya nyumba kusomesha watoto hii yote hii kutambua umuhimu wa elimu Bora kwa mtoto.

Huko St Kayumba ni bora liende tu.
Watoto wachache sana wawezao kuwaamhia wazazi wao asante kunisomesha Kayumba

Waliosoma Private watoto wengi asilimia kubwa hushukuru sana wazazi wao kwa kuwasomesha private.Sababu wanaona kabisa mzazi Ali sacrifice na alifanya maamuzi sahihi kwa future yake
 
Unamaanisha St Kayumba haifai kwa watoto wadogo ?
Ndio ila sio kwa wote kama una uwezo ni bora waanze English medium ili wapate mwanzo mzuri wa lugha huko sekondari fresh tu hata st.kayumba wanapeta maana lugha ile ile.
 
Algore shule za private walimu huwa wanapika matokeo ili kuwa brain wash wazazi.

pride darasa linapo kuwa na watoto wengi inasaidia pia kumchallenge mtoto kwa sababu huo ndio uhalisia katika maisha halisi. Darasa lenye watoto wachache mfano watoto 10 au 20 mtoto hapati changamoto kwa watoto wenzake.

Plus private school watoto wanakuwa spoon fed.

Kumbuka Lengo pekee la kumpeleka mtoto shule ya Msingi sio tu ili afaulu kwenda secondary lakini pia ajifunze kuhusu maisha.

Kumpeleka mtoto kwenye shule ambayo darasani wanakaa watoto watano tu kwanza atakuwa selfish, atakosa network ya watu ( kujuana na watu wengi: It is a proven fact that ur network is ur networth)..

Mtoto aliesoma kwenye shule yenye watoto wengi hawezi kutishwa na uwingi wa candidates lets say kwenye interview ambayo wamekuwa shortlisted watu elfu moja. Jambo hilo linaweza kumu intimidate mtoto alie soma kwenye shule ambayo darasa moja wanakaa watoto8

Kuhusu kujiamini kwenye maisha experience inaonyesha watoto walio soma kayumba hujiamini mara mia ya wale walio soma English Medium.

Wana uthubutu wa kufanya na kujaribu mambo mengi kwa sababu mazingira magumu " tough environment" ya st kayumba yamewashape,tofauti na wa English Medium ambao hawana uthubutu wa kujaribu kwa sababu walizoea kuwa spoon fed na kurahisishiwa mambo.

Mifano: Diamond, Shilole, Mobetto etc.

Mwisho: ni ujinga kumpeleka English Medium mtoto ako akafundishwe na mwalimu ambae amesoma kayumba.
Unasema watoto walisoma Kayumba wanajiamini kuliko wale wa private.

Embu wachukue hao watoto wa Kayumba na hao wa private kila mmoja azungumze mbele ya umati wa watu uone nani anaweza kujieleza mbele za watu na nani hawezi.
 
Kati ujinga siwezi kufanya ni kumpelekea mtoto hizo shule za washua, watoto wa huko huwa wa hovyo sana kuanzia ukakamavu hata kuongea.

Mimi ni kijana bora na nilisoma kayumba.

Pili hizo shule za mboga 7 hazionyeshi wala kifundisha uharisia.

Ukifa ghafla wakarudi kayumba wanaona wanateseka na watalia maisha yao yote.
Mawazo ya kimaskini.
 
Umasikini mbaya sana mkuu

Ungangali wa mtoto inategemea na wewe mzazi nyumbani, mtoto akirudi shule mpigishe kazi ndogondogo kama kujifulia nguo mwenyewe kulimalima vinyasi vinavyo zunguka nyumba,sio junia kaangalie katuni

anakomaa,kwasababu hata huko kayumba unako mpeleka ukimdekeza wenzake watamshika makalio
Inaonesha umeshikwa sana matako
 
Ndio ila sio kwa wote kama una uwezo ni bora waanze English medium ili wapate mwanzo mzuri wa lugha huko sekondari fresh tu hata st.kayumba wanapeta maana lugha ile ile.
Mkuu kuna watu wanaendaga kusoma udkatari urusi hajui hata neno moja la kirusi. Mwaka wa kwanza anasoma lugha tu na mwaka wa pili ndo anaanza kusoma udkatari kwa kirusi na mwisho wa siku anaondoka na G.P.A ya 4 plus.

Tuliosoma miaka ya tisini asilimia kubwa tumesoma shule za kiswahili na seco tukatusua kama kawa.

Shule za kiswahili watoto wanaanza kufundishwa kiingereza darasa la.tatu. so wana soma kiingereza kwa miaka mitano. Kwa usimamizi bora wa mzazi,miaka mitano inatosha sana kwa mtoto kujua basics za lugha ya kiingereza ambazo ata zi apply akifika sekonndari.

Isitoshe siku hizi mambo mengi sana yamerahisisha usomaji kwa watoto.

Kuna programmes nyingi like Ubongo Kids. Kuna Vitabu, kuna videos kuna taasisi zinahusika na kusimamia maendeleo ya kitaaluma.ya wanafunzi, kuna tuitions etc.

So suala la lugha wala sio ishu kabisa kwa mtoto anaependa kusoma na ambae yupo chini ya usimamizi wa mzazi ambae yupo serious na maendeleo ya kitaaluma ya mtoto wake.
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa JF wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakaonipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (Huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.

MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa laki tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
walikuwa shule gani kabla hujawaamisha? kama utaweza kujib llakini
 
Mkuu kuna watu wanaendaga kusoma udkatari urusi hajui hata neno moja la kirusi. Mwaka wa kwanza anasoma lugha tu na mwaka wa pili ndo anaanza kusoma udkatari kwa kirusi na mwisho wa siku anaondoka na G.P.A ya 4 plus.

Tuliosoma miaka ya tisini asilimia kubwa tumesoma shule za kiswahili na seco tukatusua kama kawa.

Shule za kiswahili watoto wanaanza kufundishwa kiingereza darasa la.tatu. so wana soma kiingereza kwa miaka mitano. Kwa usimamizi bora wa mzazi,miaka mitano inatosha sana kwa mtoto kujua basics za lugha ya kiingereza ambazo ata zi apply akifika sekonndari.

Isitoshe siku hizi mambo mengi sana yamerahisisha usomaji kwa watoto.

Kuna programmes nyingi like Ubongo Kids. Kuna Vitabu, kuna videos kuna taasisi zinahusika na kusimamia maendeleo ya kitaaluma.ya wanafunzi, kuna tuitions etc.

So suala la lugha wala sio ishu kabisa kwa mtoto anaependa kusoma na ambae yupo chini ya usimamizi wa mzazi ambae yupo serious na maendeleo ya kitaaluma ya mtoto wake.
Sahihi
 
T
Yes angalau sio hizi za leo yani mtoto afundishwa English kwa kiswahili.

"Watoto leo tunajifunza kuhusu tense.
Zipo tense za aina tatu. Kuna past tense, present tense na future tense"
Ndo nikalipe milioni hivi kweli? Tuheshimiane tafadhal
Tafuta hela uache makasiriko.
Maskini mnafarijiana au sio. Waza madogo upate kidogo waza makubwa upate makubwa. Somesheni watoto shule bora ni haki yao ya msingi.

Sitaki povu
Yani mzazi ni mjinga anataka na vizazi vyake vibaki kwenye ujinga.
 
Back
Top Bottom