Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Toka mke wangu amenishauri kuwaondoa huko na kuja st. Kayumba akili za watoto zimekuwa fire mmoja anaongoza na mwinine hakosi top 10. Watoti wamekuwa ngangali tofauti na mwanzo. Na sijawahi juta kwa uamuzi huu!
Una mke brooo ..asikuambie Mtu hongera Sana
Wanawake Ndo tunaongoza kulazimisha watoto waende English Medium na Kununa juu plus kushindana Yaani na ufakhari wa kushuka kwenye school bus
 
Ila english medium za siku hizi michosho sana kipindi zinaanza st marys green acres academic etc walimu wengi walikuwa ni wakenya kidogo ilikuwa angalau 😄
Yes angalau sio hizi za leo yani mtoto afundishwa English kwa kiswahili.

"Watoto leo tunajifunza kuhusu tense.
Zipo tense za aina tatu. Kuna past tense, present tense na future tense"
Ndo nikalipe milioni hivi kweli? Tuheshimiane tafadhali
 
Una mke brooo ..asikuambie Mtu hongera Sana
Wanawake Ndo tunaongoza kulazimisha watoto waende English Medium na Kununa juu plus kushindana Yaani na ufakhari wa kushuka kwenye school bus
Nakazia
 
Yes angalau sio hizi za leo yani mtoto afundishwa English kwa kiswahili.

"Watoto leo tunajifunza kuhusu tense.
Zipo tense za aina tatu. Kuna past tense, present tense na future tense"
Ndo nikalipe milioni hivi kweli? Tuheshimiane tafadhali
Na hii ni hadi chuo bruh 😄😆 kingereza kwa kiswahili
English medium zimepata nguvu kutokana na kutokuwa na mazingira mazuri kwa shule za serikali wakirekebisha hilo tu wengi watazikimbia
 
Safi sana . Nyie ndio wanawake mnaojitambua
 
Ila tofautisha wahindi na wabongo, mhindi anaishi juu chini ana biashara kwa hiyo mtoto anaanza kumsadia baba yake biashara angali mdogo na anajua jinsi ya kuongea na wateja. Angalia mbongo anaishi bunju biahara gerezani karikoo ukiona amefika kwenye hiyo biashara ujue kuna shida ya mhimu hata kama utamuandalia biashara gani ni hakika itamshinda .

Cha msingi ni kwamba tuondakane na huu ujina wa watoto kusoma muda wote hata wakati wa likizo .

Mwachie biashara asimamie mpaka likizo iishe arudi shule sio kila siku tuition
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…