Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Shida inapokuja unataka kuishi kama tajiri wakati ni masikini. Una fake maisha.
Shule za wenye hela, na wewe unapata vihela vihela unataka upeleke shule ya wenye hela matokeo yake unaishia kwenye madeni na kuwarudisha nyumbani.
Kuna watoto wazazi wao wanasowasomesha Fedha boys, akimaliza anaenda kusoma chuo nje ya nchi.
Tusifake maisha, ishi kwa uhalisia wako. Ukimpeleka za wenye hela lazima siku moja uumbuke.
Usijifariji kwasababu umepata faida, sema hauna hela. Kuna watu watoto wao wako kwenye shule za hela, na maendeleo anafanya na hakopi wala hawawezi ada. Amini hilo
Nimekuwa ndio nimekuja kugundua kuna watu walikuwa wanalipa ada
Kuna jirani watt wake wa5 wote ni st constantine arusha na vyuo ni nje aisee
 
Matajiri wanawasomesha watoto wao kwenye shule za gharama ili waje warithi na kusimamia kampuni zilizoanzishwa na familia; kama wewe unatengeneza kizazi cha kuajiriwa, usiangaike na mashule ambayo chekechea unalipa milioni 12+
 
wakati mwingine,umaskini unasababisha uwe na moyo wa chuki bila sababu.
Hebu tuchangie kidogo, unamsomesha mtoto English Medium kuanzia chekechea mpaka form six, vyuo vikuu bora kwa sasa nchini mwetu ni vya serikali vikiongozwa na UDSM. Chuoni fani za kusoma kwa mfano ni MD(udaktari wa binadamu), Sheria, Uhasibu, Uhandisi, Uchumi, Sayansi ya kompyuta, ufamasia, udaktari wa mifugo, kilimo n.k Fani zote hizi kila moja ina lugha yake, vile vikiingereza vya kawaida havipo tena kule. Kimsingi kiingereza cha kawaida kinaishia shule ya msingi, baada ya hapo Physics ina lugha yake, Chemistry, Biology, Mathematics hali kadhalika. Mimi sioni mchango wa kiingereza kivile. Cha msingi hiyo shule ya serikali ifundishe vizuri. Shule km Mzumbe, Tabora boys and girls, Kibaha, Masalato, n.k ni shule nzuri sana. Cha maana serikali iboreshe shule zake, iwalipe walimu vizuri na kuwapatia motisha mbalimbali hakuna haja ya kulipa milioni nzima eti ada ya chekechea. Elimu ni mtu mwenyewe km ana nia. Unaenda kusoma computer science/engineering hivyo vikiingereza vyako unavipeleka wapi, kule ni code na logic. Hata vichaa kule kwao uingereza wanaongea kiingereza
 
sasa upambane kutafuta za nini kama hutaki zitumike kwa wanao,ukifa mashamba na majumba watanyanga'nywa na baba wadogo,warithishe kitu ambacho hawawezi nyang'anywa.acha uwoga wa maisha...

Watanzania mnapenda sana kupigwa aisee.

Yani nikatoe milioni 4 ili mtoto wangu afundishwe A for Apple? Mwisho wa siku Hesabu sifuri sayansi sifuri ila anajua tu KIINGEREZA cha kubabaisha.


Pesa haitumiki kizembe namna hiyo.. Muweke st kayumba weka usimamizi kama.msingi wa KIINGEREZA mtafutie walimu na programme nzuri za KIINGEREZA ili anapoingia form one masomo ya secondary yasimsumbue.


Acheni utoto nyie...


Kwanza hampo hata smart mngekuwa smart mngewauliza kwanza watoto wenu wanataka kuwa nani ndo muwapeleke kwenye shule inayo toa programme husika. Sio una hangaika kumkaririsha English Medium kumbe mwenzako anataka kuwa kama Konde Boy..

vinginevyo nyie na wanao somesha watoto wao st kayumba wote mpo sawa ila wenzenu wajanja nyie mnapigwa mamilioni wenzenu hawapigwi
 
Watanzania mnapenda sana kupigwa aisee. Yani nikatoe milioni 4 ili mtoto wangu afundishwe A for Apple? Mwisho wa siku Hesabu sifuri sayansi ila anajua tu KIINGEREZA cha kubabaisha.
Si kweli. Hakuna shule inayotoza gharama hizo ukaikuta hata na division three moja
 
Wengi watakuponda, ata waliosoma kwenye hizo shule sijaona wakifanya cha maana, sijawaona wakichimba au kumiliki visima vya mafuta wala gesi
 
Hizi ni kauli za kujaribu kubalance tu mabaya na mazuri. Lakini ukweli unabaki, huwezi kupata elimu bora katika shule ambayo mwalimu hana cha kupoteza
Unachanganya elimu bora na matokeo mazuri kwenye mitihani ya mwisho.

Tanzania hakuna elimu bora on the first place.
 
Ngoja uje upingwe kabuni yangu Primary Kayumba Sec private kwa kua watoto wangu wa kike na Niko busy kidogo na maisha advance boarding Gvt Inshaa Allah..
Na mwanangu std 7 alipata A ,ameenda huko seminary anaburuza akiwaambia ametoka Kayumba hawaamini,haka kadogo Nako nakaandaa na Kingereza kakifika std 6 naanza kukaprooni vzr Ili kaweze kufaulu vzr na kakapambane huko Kwa masista
Lengo ajue tu Kingereza maana huku Kayumba Secondary kama mtoto mzembe hatoboi na kama mzazi uko busy ni changamoto (kunahitaji uangalizi na ushirkiano mkubwa kati ya mzazi ,mwl na mtoto)
 
Mimi English Medium kama haimilikiwi na Mzungu ( Mmarekani, mwingereza au Mu Australia) sipeleki mtoto wangu n'go.

Yani mtoto wangu afundishwe kwa KIINGEREZA na mtu ambae lugha yake ya mawasiliano kila siku ni kiswahili?

Endeleeni kupigwa mkuu.

Wajinga ndio waliwao
Ila english medium za siku hizi michosho sana kipindi zinaanza st marys green acres academic etc walimu wengi walikuwa ni wakenya kidogo ilikuwa angalau 😄
 
Back
Top Bottom