Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mkuu ni a nice story,kama wewe ni mtu wa kujifunza unaweza kujifunza kitu.My own story kwa watoto wangu is as follows:
1.STD I-VII-Shule za kawaida.
2.Form I-IV -Private Schools
3.Form V-VI-Government Schools
4.Katika watoto wangu ambao nimewapitisha Shule hizo,Wawili wamemaliza MSc.Mmoja Mzumbe University yuko Bank,na mwingine UDSM naye yupo Bank.Mtoto mwingine
amemaliza Muhimbili ni Surgeon.Watoto wengine wawili wamemaliza SUA wana BSc.Agri.Business na wote ni employed,mmoja yuko Bank,mwingine yupo World Vision.Mtoto mwingine amemaliza Second Year IFM anakwenda Third Year,huyu anachukua Economics and Finance.Wa mwisho amefaulu kwenda Form V atachukua CBG(Chemistry,Biology and Geography).So you see,obviously kutopitia Shule za English Medium haiwajawaathiri kabisa,na wameniambia categorically,baba,it is wastage of resources kuwapeleka watoto English Medium Schools,na nime-prove it first hand.
Hongera sana mkuu aisee . I am so inspired.
 
Mkuu ni a nice story,kama wewe ni mtu wa kujifunza unaweza kujifunza kitu.My own story kwa watoto wangu is as follows:
1.STD I-VII-Shule za kawaida.
2.Form I-IV -Private Schools
3.Form V-VI-Government Schools
4.Katika watoto wangu ambao nimewapitisha Shule hizo,Wawili wamemaliza MSc.Mmoja Mzumbe University yuko Bank,na mwingine UDSM naye yupo Bank.Mtoto mwingine
amemaliza Muhimbili ni Surgeon.Watoto wengine wawili wamemaliza SUA wana BSc.Agri.Business na wote ni employed,mmoja yuko Bank,mwingine yupo World Vision.Mtoto mwingine amemaliza Second Year IFM anakwenda Third Year,huyu anachukua Economics and Finance.Wa mwisho amefaulu kwenda Form V atachukua CBG(Chemistry,Biology and Geography).So you see,obviously kutopitia Shule za English Medium haiwajawaathiri kabisa,na wameniambia categorically,baba,it is wastage of resources kuwapeleka watoto English Medium Schools,na nime-prove it first hand.
Asante sana mkuu
 
Umasikini mbaya sana.( Torono enkokishu)
Kutumia pesa kizembe ni umasikini pia..

Huwezi kuniita Mimi masikini kwa sababu nimeamua kuachana na mwanamke anae taka nimuhonge milioni moja kwa mwezi na kwenda ku settle na mwanamke ambae matumizi yake ni laki moja kwa mwezi...

Hiyo ni busara na sio umasikini
 
Kutumia pesa kizembe ni umasikini pia..

Huwezi kuniita Mimi masikini kwa sababu nimeamua kuachana na mwanamke anae taka nimuhonge milioni moja kwa mwezi na kwenda ku settle na mwanamke ambae matumizi yake ni laki moja kwa mwezi...

Hiyo ni busara na sio umasikini
Naheshimu maamuzi yako, Fanya uwafundishe mwenyewe mkuu uta save Muda na pesa.
 
Sio kweli

Mfano una Hospitali au kampuni ya wanasheria au ya engineering au uhasibu inayohitaji certification ya elimu au unamiliki chuo kikuu private au unamiliki shirika la ndege unataka wanao wawe ma pilot hoja yako haina mashiko labda unaongelea.biashara za umachinga

Serious business mtoto mtoto anatakiwa kusoma sana sio utani

Watoto wa wahindi,waarabu kama ASAS, Bakheresa, Dewji wamesoma sio utani hasa kwenye vyuo best universities in the world baada ya kfauku sana shule Tanzania na walipomaliza wakaja ku.run family business
Dunia nzima matajiri wenye lengo la uendelezaji wa mali lazima wasomeshe kwenye shule kubwa na za ghali ili kujenga connection.

Matajiri wote Tz watoto wao wapo IST, hapo hutamkosa mtoto wa MO, GSM, Azam, Cello, Camel
 
Maneno kama ya mwanamke shangingi. Huu Uzi ni wanaume wanao tafuta hela na ambao wana jua ugumu wa hela. Wewe unakaa kwa shemeji huwezi elewa chochote
Mbona matusi jomba? Kama huna hela usijilazimishe kuingia gharama zilizo juu ya uwezo wako. Halafu kama ni hela hata wanawake wanazitafuta. Kuna wanawake kibao wanakuzidi uwezo wewe na ukoo wako combined. Acha matusi ya kingese jomba.
 
Dunia nzima matajiri wenye lengo la uendelezaji wa mali lazima wasomeshe kwenye shule kubwa na za ghali ili kujenga connection.

Matajiri wote Tz watoto wao wapo IST, hapo hutamkosa mtoto wa MO, GSM, Azam, Cello, Camel
Umesema IST . IST huwezi kufananisha na hizi English Medium zetu za kufundishwa na walimu walio soma kayumba akina Teacher Kaju ( Kajunjumele)..

Hizi English Medium ni Kayumba zilizo changamka
 
Kuna akina mama nitilie wanaoishi chumba kimoja wanasomesha watoto English medium kwa Vikoba ukimuuliza kwa nini anakwambia mwingine anasema mimi sitaki mwanangu wa kike aje kuolewa kama mimi asiyejua neno hata moja la kingereza msumbufu huyu tulisoma wote kayumba

Nampeleka mwanangu huko English Medium aweza.kutana na mwanaume wa kueleweka waliyesoma wote kuliko.hawa waswahili wa kayumba

Anakwambia wengi huoa au kuolewa na wale walisoma wote kama ulisoma Kayumba uwezekano mkubwa kupata msoma Kayumba mwenzio mkubwa sitaki.Changamoto nimepitia zinatosha.Kayumba wasumbufu uelewa mdogo
Ila hii nchi bado ina watu wajinga mno.
 
Top 10 st kayumba ni wa mwisho private school. Halafu mtoto anakuwa top 10 na D zote halafu unajisifia anawaburuza wenzie? Ni CCM au watu wenye mawazo ya ki-CCM tu wanaothubutu kusifia ujinga
acha kuleta mambo ya vyama kwenye mada isiyo ya kisiasa. Kuna shule nyingi tu za serikali ziko vizuri. Ilboru, Kibaha, Tabora, Mzumbe, Kilakala, Msalato na nyinginezo.
 
Umesema IST . IST huwezi kufananisha na hizi English Medium zetu za kufundishwa na walimu walio soma kayumba akina Teacher Kaju ( Kajunjumele)..

Hizi English Medium ni Kayumba zilizo changamka
Binafsi English Medium ninayo ikubali ni Feza sababu hawana Tuition wala kukaririsha watoto, likizo watoto wanaenda kama kawaida.

Kama una pesa bora umpeleke mtoto hata Agakhan Primary, Secondary na IB
Maama gharama za jumla hadi anamaliza IB hazitafika Milioni 200 kwa miaka 13
 
Kuwajengea nyumba ni Investment? Wewe akili huna.Ungesema unawaanzishia biashara ungeeeleweka .Nyumba na viwanja vyako vya kipuuzi vitawasaidia nini?

Wahindi maisha yao wanapanga wanadomesha watoto.best schools na watoto wao wana maisha mazuri mno.pamoja na watoto wao hawaishi uswahilini wanaishi katikati ya miji maisha mazuri mno wote wazazi na watoto kuliko wewe mwenye viwanja vya hovyo nje ya mji huko uswahilini

Nyumba na viwanja.navyo ni vitu vya kujivunia kuwa ume sacrifice watoto wasome Kayumba kisa ubaki na vihela koko vya kuwajengea nyumba na kuwanunulia viwanja koko nje ya mji huko uswahilini?

Wewe akili zimo kichwani kweli?
Unaelewa maana ya sacrifice?
Ndugu yangu nakuunga mkono ila watu bado wanakazana kujifanya hawaelewi ila urithi wa nyumba unaharibu vijana.
 
Algore shule za private walimu huwa wanapika matokeo ili kuwa brain wash wazazi.

pride darasa linapo kuwa na watoto wengi inasaidia pia kumchallenge mtoto kwa sababu huo ndio uhalisia katika maisha halisi. Darasa lenye watoto wachache mfano watoto 10 au 20 mtoto hapati changamoto kwa watoto wenzake.

Plus private school watoto wanakuwa spoon fed.

Kumbuka Lengo pekee la kumpeleka mtoto shule ya Msingi sio tu ili afaulu kwenda secondary lakini pia ajifunze kuhusu maisha.

Kumpeleka mtoto kwenye shule ambayo darasani wanakaa watoto watano tu kwanza atakuwa selfish, atakosa network ya watu ( kujuana na watu wengi: It is a proven fact that ur network is ur networth)..

Mtoto aliesoma kwenye shule yenye watoto wengi hawezi kutishwa na uwingi wa candidates lets say kwenye interview ambayo wamekuwa shortlisted watu elfu moja. Jambo hilo linaweza kumu intimidate mtoto alie soma kwenye shule ambayo darasa moja wanakaa watoto8


Kuhusu kujiamini kwenye maisha experience inaonyesha watoto walio soma kayumba hujiamini mara mia ya wale walio soma English Medium.

Wana uthubutu wa kufanya na kujaribu mambo mengi kwa sababu mazingira magumu " tough environment" ya st kayumba yamewashape,tofauti na wa English Medium ambao hawana uthubutu wa kujaribu kwa sababu walizoea kuwa spoon fed na kurahisishiwa mambo.


Mifano: Diamond, Shilole, Mobetto etc.

Mwisho: ni ujinga kumpeleka English Medium mtoto ako akafundishwe na mwalimu ambae amesoma kayumba.
Wewe jamaa kwanini unatetea umaskini?
 
Kati ujinga siwezi kufanya ni kumpelekea mtoto hizo shule za washua, watoto wa huko huwa wa hovyo sana kuanzia ukakamavu hata kuongea.

Mimi ni kijana bora na nilisoma kayumba.

Pili hizo shule za mboga 7 hazionyeshi wala kifundisha uharisia.

Ukifa ghafla wakarudi kayumba wanaona wanateseka na watalia maisha yao yote.
Uharisia = uhalisia. Wewe ni maskini na fukara naona unajifariji.
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakao nipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.


MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa lako tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
upo sawa watoto wangu wa kwanza na wapili kayumba mpaka chuo kikuu. wa tatu mwezi huu form 5 kayumba huko huko.. wa nne yupo la 7 anamaliza muda mfupi ujao maendeleo yake sio mabaya na inshallah atafaulu. huko medium sitaki hata kusikia!
 
Back
Top Bottom