Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mwanangu najua inakuuma sana kukosea kuandika kiingereza ndo maana unatoa maelezo mengi ya kutaka kuonewa huruma. Mimi nisingehoji kama na wewe usingejimwambafy kwamba ulikuwa unajua kiingereza kuliko hata waliotoka medium. Siku nyingine acha sifa za kijinga.
Wala hainiumi,mie Ni kilaza mmoja mzuri,kukosea is part of human being none is perfect, unadhani labda eti najaribu kujitetea kwa kukosea. Ila lengo langu Ni kuwa Kama mtu Ana uwezo wa kujifunza kitu anajifunza haijalishi kuwa yupo. Kwanza lazima uwe proud na kukosea ama kufeli Mana aliyejaribu na akafeli sio sawa sawa na ambaye hajajaribu. Kwanza wanangu Wana encourage mno wawe proud kufanya mistakes later Wana analyse why they did mistakes. Katika maisha mistakes,kuanguka,kufeli,kufiliska, biashara fulani imebuma,yaani life or so called success is constant falling down and stand up ,fall down seven times wakes up eight times.
I don't entertain perfectionism katika kizazi changu. Bali nawaambiwa wawe bold kufanya mistakes na kujaribu kila kitu yaani washinde Ile aibu ya kuwa mie nimekosea,ama nitaonekana mjinga. One Chinese proverb " the one who asks the quesTion is the stupid for one second but the one who never asks is the full for lifetime.
Yaani elewa mie Ni kilaza mmoja mzuri mkuu,hayo niliyoyandika Kama kuelimisha jamii kwanza sio Mimi Sasa kwa taarifa yako. Kwanza mie napenda wanaonionyesha my weakness all the time ndio marafiki zangu Mana wananifanya na grow,thrive, survive and prosper.
Mie kwanza nimeishia fomu Foo nikapata zero nikapata cheti nikashindwa kuchukua diploma.

Yaani mie Ni kilaza tu Basi,naomba uwe na amani
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa JF wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakaonipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (Huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.

MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa laki tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Tangu nijiunge JF sijawahi kuona thread ya kipumbavu kama hii.
 
Unajidanganya, umedanganywa na umedanganyika zaidi.

Shule za serikali sio tu kwamba mtoto hatojua lugha pia ataenda kujazwa ujinga. Hao walimu ni nadra sana kuingia darasani wanachojali wao kuwakamua watoto pesa za twisheni kilazima.

Kama tu watoto wanahitimu mpaka darasa la saba ila kusoma na kuandika hawajui je kuna maarifa mengine watakuwa wameyapata kama kusoma tu imekuwa mbinde?

Kaa na wanafunzi wanaosoma Kayumba uwasikilize maongezi Yao na usafi wao wa mwili na mavazi kiujumla halafu kakae na wanafunzi wanaosoma shule binafsi kisha na wao uwasikilize maongezi yao na utazame usafi wao wa mwili na mavazi.
 
Uko sahih watoto wengi pia wa level za English medium wengi wanakuwa walaini sana na hawajui hesabu wengi, wengi ni vilaza wa hesabu mno
Unajidanganya.

Wanafunzi wa Kayumba somo angalau wanajitahidi kufaulu ni kiswahili ikizidi sana maarifa ya jamii na sayansi.

Ukija kwenye somo la hisabati na kiingereza wanaangukia pua sana.
 
Kwa ada ya 2M ni fear hata kama watoto 4 fresh jumla 8M tena kwa standard ya shule ya msingi.

Akifika secondary hata umpeleke kayumba angalau kingereza anajua na atafanya vizuri na pia atakuwa kiakili kashakuwa.

Msingi mzuri kuwekeza akiwa mdogo na pia kama kwa sasa maisha yapo fresh mpeleke tu kwa vile maisha hayaeleweki ,ynaweza kubadilika mda wowote ule.

Japo kwa mtoto mdogo kwa shule hizo ni changamoto anaweza kupotea kimaadili kabisa.
Kuna kupotea kimaadili pia suala la usafi wanafunzi wa Kayumba kwao ni zero kabisa.
 
Toka mke wangu amenishauri kuwaondoa huko na kuja st. Kayumba akili za watoto zimekuwa fire mmoja anaongoza na mwinine hakosi top 10. Watoti wamekuwa ngangali tofauti na mwanzo. Na sijawahi juta kwa uamuzi huu!
Anaongoza kundi la wajinga😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Yaani nimeingia la kwanza naongea my mother tongue pekee Sasa shangaa tunaingia la Pili nakuwa wa kwanza na shule nimetoka bush nikaenda kusomea town ,yaani lugha is of immaterial linapokuja suala la kichwa kuelewa kitu. Unaweza ukafundishwa kwa kabila yako ukawa daktari mzuri mno. Yaani wachina wanasoma kwa lugha yao Ni Engineers na leo nilikuwa nao wanaseti foundation ya road underpass,yaani technical drawings anaisoma na anaweka vipimo. Yaani hufanyi kazi kwa kuongea Bali kwa vitendo na uelewa wako
Upo sahihi kabisa mkuu
 
Ni juzi tu mjukuu wa Azam kaoa, picha waliyoitoa alipiga Yeye, Mtoto wa MO, GSM na mwingine hatumjui, na wote wamesoma shule moja IST
Kufikiri kwamba ukisoma shule ya kishua utapata connection na watoto wa kishua ni sawa na kuamini kwamba ukienda kwenye bar ya kishua wanakouza bia elfu kumi basi wale washua wanao kunywa kwenye hiyo bar watakuwa rafiki zako kwa sababu unakunywa nao bar moja wakati wenzako wanakuona mwizi tu.

Wakishua wanawadharau sana watoto wa kimasikini. Na hawapendi kuchangamana nao.

Mfano mzuri ni pale Shaaban Roberts, ngozi nyeusi wana baguliwa sana. Sio wanafunzi tu bali hata walimu. The same as Agha Khan.

Hata USA ndivyo inavyo kuwaga mara nyingi. Mtoto mweusi akipelekwa kwenye shule ya wazungu tu atabaguliwa mpaka maka.

Kuna mitaa mingine Marekani akihamia mtu mweusi hata mmoja wazungu wanauza nyumba zao wanahamia mitaa mingine.

Njoo kwenye mpira, Konde Boy kaenda Ahly hapo kaishia kubaguliwa kwa sababu anatoka nchi ya kimasikini.

Ukiwa mtoto wa kimasikini ukaenda shule ya kishua, kampani yako watakuwa masikini wenzako tu wanao soma kwenye shule hiyo ambao wazazi wao "wamejibana" wameuza mashamba ili kuwaonyeshea walimwengu kwamba wanaweza kumudu gharama za shule ghali. Huwezi kuupinga huu ukweli.

Jiulize Mtaani kwenu kuna matajiri wangapi? Are they ur friends . Wamesha connection ngapi za maana ?
 
Una program subconscious mind yake kuwa wa kusukumwa ,ama kuelekezwa kila kitu,yaani unamtengenezea behavior ya kusimamiwa ama kulishwa like spoon feeding.
Sasa njoo Hali halisi ya maisha ,he maisha yako Kama huko saint English ama Kama saint kayumba. Kuwa atasimamiwa na kuelekezwa how to fight in the jungle full if wolves, wild dogs, bulls and Black mamba. Binafsi napenda mwanangu afundishwe shule ya kijeshi,yaani Ni mchakamchaka baadaye akuja kuwa automatic kufanya Mambo ya kijeshi bila ya kusukumwa. Alime bustani,apapalie,atengeneze fanicha,ajenge nyumba,atengeneze gari,ajue kutengeneza sabuni etc,Kama anapena mchezo fulani akomae nayo,atoke huko anajua kuchora ramani za nyumba,anajua kutumia vifaa vya saveya,awe anajua vitu vingi ama awe na skills za maisha na sio eti kufaulu na kuongea English Basi kuwa ndio amefaulu maisha.

Yaani when mental and physical are trained or exposed under stress and pressure then they grow stronger than how they were before.
Ikiwekazana atembee kwenda shule, what I trust Ni kuwa binadamu huwa haihangaiki Kama hapati any hardship.
Am a student of mind and brain. Yaani we're always driven by either pleasure or pains.
Yaani mtu anafanya kitu kukwepa maumivu ama kupata Raha Basi. Na ubongo kazi yake Ni kukwepesha kutoka kwenye habari ama kitu ambacho kinakupa maumivu ya kimwili na mentally
Sahihi kabisa mkuu
 
Unamshaurije mwanajf mwenzetu, sababu hata si tuliosoma kayumba, kwenda seko tulikuwa tunakimbia morning talk, na debaite,/seko nikapelekwa ya private bwana we tulipelekwa hasa, japo imenisaidia kwa kiasi fulani.
Cha kumshauri atafute pesa.

Ukiwa maskini hata uwezo wa kufikiri unapungua.
 
Ukiwa mtoto wa kimasikini ukaenda shule ya kishua, kampani yako watakuwa masikini wenzako tu ambao wazazi wao wameuza mashamba ili kuwaonyeshea walimwengu kwamba wanaweza kumudu gharama za shule ghali. Huwezi kuupinga huu ukweli.
Ndio maana kuna mdau mmoja nikamwambia peleka mtt huko ukiwa na uwezo na kwasabb ya mazingira mazuri ya kujisomea
 
Back
Top Bottom