Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Puberty hata private anaharibika tu. Hyo ni akili yake atapokea vp hyo stage
Yes kweli halafu kama kuharibikiwa puberty huwa haichagui haibagui. Awe kayumba awe English Medium wote inazoa.
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa JF wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakaonipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (Huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.

MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa laki tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Una kitu, usikilizwe
 
Msisahau pia kila mtu ana destiny yake kwenye maisha bila kujali alisoma wapi. Mfano Paula Kajala alisoma English Medium kuanzia darasa la kwanza hadi la 7 then akaenda Tusiime form one hadi Six. Now look at what she is doing. Hicho anacho kifanya ndicho ambacho kilimpeleka shule?
 
Mziki uko sekondari

Akikutana na masomo.kingereza kitupu atadorora hata kama msingi alikuwa mzuri sana matokeo ya form.four lazima atachemka labda awe vipaji maalum
ni kweli lakini niliposema akiwa mna msingi mzuri kuanzia std1-7 nilimanisha asome hizi shule za kingereza ...badae mpeleke shule za serikali zinazo jielewa mfano kunashule maja inaitwa URU sekondari ya kayumba lakini ni kiboko kwa kiasi chake kwani matokeo yake mwaka jana hakuna 4 wa 0..ipo huko kilimanjaro na hilo darasa lilikua na zaidi ya watoto 130
 
Basi kumbe wewe ni mbumbumbu wa pesa. Huna elimu ya pesa. Huna mahusiano mazuri na hela...

Ngoja nikusanue kitu ndugu yangu. Nikupe elimu ya mtaani kidogo kuhusu pesa..

Mjanja sio yule anae tumia ( spend) pesa nyingi ila ni yule anae ( tunza) pesa nyingi.

Mfano; kama Mimi mshahara wangu ni shilingi milioni tatu kwa mwezi ila matumizi yangu ni sh laki TANO kwa mwezi halafu natunza benki milioni mbili na laki tano kila mwezi.

Ila wewe mshahara wako ni shilingi milioni kumi kwa mwezi ila matumizi yako ni sh milioni tisa na laki nane kwa mwezi.

Baada ya miaka kumi Mimi nitakuwa tajiri wewe utakuwa masikini. Nktakuajjri Mimi.

So wewe kuspend milioni nane kwa mwaka kulipia kitu ambacho unaweza kukipata kwa sh laki moja kwa mwaka ni shobo zako tu na.umbumbumbu/ulimbukeni wako kwenye pesa.

Huna mahusiano mazuri na pesa. Pesa haitumiki kizembe namna hiyo.
Ungeniambia hiyo milioni nane unaitunza kila mwaka ninge ona unafanya kitu ila kumbe una spend? Khaaa

Hapo mjanja ni huyo ambae unaweka hela kwenye akaunti yake na sio wewe
Mipango siyo matumizi. Unaweza kutunza na mwisho wa siku ukaishia kuusikia tu utajiri.
 
ni kweli lakini niliposema akiwa mna msingi mzuri kuanzia std1-7 nilimanisha asome hizi shule za kingereza ...badae mpeleke shule za serikali zinazo jielewa mfano kunashule maja inaitwa URU sekondari ya kayumba lakini ni kiboko kwa kiasi chake kwani matokeo yake mwaka jana hakuna 4 wa 0..ipo huko kilimanjaro na hilo darasa lilikua na zaidi ya watoto 130
Muache kayumba mtafutie mwalimu wa English Medium amfundishe kiingereza
 
Msisahau pia kila mtu ana destiny yake kwenye maisha bila kujali alisoma wapi. Mfano Paula Kajala alisoma English Medium kuanzia darasa la kwanza hadi la 7 then akaenda Tusiime form one hadi Six. Now look at what she is doing. Hicho anacho kifanya ndicho ambacho kilimpeleka shule?
Sahihi
 
Shule sio kwenda kusoma tu pia unatengeneza network kwa mtoto wako, shule nliyo soma mimi imenisaidia ku interact na watoto wa watu wenye nafasi serikakalini na wafanya biashara kupitia ma classmates zangu kuna vitu hua sipati shida sababu nna walamba asali wananipa backup

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kama una kitu ndani yako connection itakufuata mahali popote utakapo kuwa. Kuna watu wana pata connection hapa hapa jf.
 
Kuwa na hela sio sababu ya kuitumia kizembe dada ake. Hela lazima uiheshimu pia.
kuna mtu mmoja aliwahi kusema " if you dont get serious with ur money, u will never get serious money " wabongo wamekariri wanadhani ukiwa na pesa lazima uzitumie bila mpangilio " kutapanya".

Kwa mfano kama kuna bidhaa naweza kuipata kariakoo kwanini nihangaike kulipa mamilioni ya shilingi kusafiri kwenda China kununua bidhaa hiyo hiyo ambayo naweza kuipata nikiwa kariakoo.

Kwanini nilipe milioni 4 kwa mwaka kwa ajili ya mtoto wangu kusoma English course ( of course English Mediums ni English course zilizo changamka. )
Wakati anaweza kusoma kayumba nikamtafutia walimu wa Tuition wakamfundisha kiingereza kama somo?
 
Kuwa na hela sio sababu ya kuitumia kizembe dada ake. Hela lazima uiheshimu pia.

Ukishasema kutumia kizembe hasa inapokuja swala la Elimu ni kwamba hauna hela.
Tafuta hela itosheleze mahitaji siyo ujibane bane ili mahitaji yafit kwenye hela [emoji23][emoji23]
 
Wewe hujamuelewa mtoa mada. Mtoa mada anacho kisema ni kwamba usitumie pesa nyingi kugharimia bidhaa ambayo unaweza kuipata kwa bei ya chini ya hapo kisa una hela. ( Hata ubepari unafundisha hivyo, minimize cost to maximize profit.)

Kwa mfano hakuna sababu yoyote ile kutoa milioni nne na ushee kwa mwaka ili mtoto wako ajifunze kiingereza kituo cha English course kilicho changamka( English Mediums school) wakati unaweza kumpeleka shule ya kayumba halafu ukamtafutia mwalimu mzuri wa kiingereza ikiwezekana anae fundisha huko huko English Medium akawa anamfundisha tuition ya KIINGEREZA kwa kutumia vitabu vile wanavyo tumia hao wanao soma shule za KIINGEREZA.
 
Back
Top Bottom