Kama uzi wangu niliyowahi kuutoa kuhusu kukutana na mrembo wa Malta
Niliondoka tarehe 12 February na Qatar air na kufika tarehe 13 Malta airport na baada ya taratibu zote za uhamiaji
Nilifanikiwa kukutana na mwenyeji wangu,akiwa ameambatana na mabinti wawili na Kijana wa kiume mmoja
Waliponipokea walinipeleka resting point moja karibu na airport na kuagiza vinywaji fulani hivi,sikupata ladha ya kile kinywaji, nikakataa na kuagiza soda
Wakiwa wanaongea kiingereza kidogo wakichanganya kilugha fulani, nilihisi kama kijana wa kiume hakufurahishwa mimi kufika kuonana na binti huyo, wengine wa kike wenyewe walikuwa wanafurahi kuona shemeji yao
Binti Sarah ambaye ndiye mwenyeji wangu alinikaribisha vizuri na niwe na amani na akaniambia wanaishi Saint Julian's hivyo, tukanyenyuka tupanda basi ya kuelekea huko
Baada ya kufika huko licha ya kufika huko na kukaa na binti Sarah hotelini huko Julian's,makubwa yalipata baada ya siku tatu, makubwa mnooo
Nahitaji daktari wa saikolojia anitibu ndo nije kuendelea na simulizi,nikipona nitakuja kuendelea ,kwa sasa sipo vizuri ...........
Pia soma: