Mrejesho: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Nakwambia kwa uzoefu kama unaamua mke wako kila.kitu uandike kwa jina lake umejiroga.bora ungeandika kwa majina ya watoto.

Kama una hela tafuta na mali zako za siri lakini usisahau ilitokea la kutokea mnagawana pasu.

Aisee ndoa ni majanga.
😅😅😅 Wacha tu nicheke ,ila Mwenyezi Mungu anijaalie maisha marefu angalau watoto-wakue na kujitegemea.
 
Hivi mwanamke mwenye mali na utajiri huwa wanafuata nini kwa Mwanaume?

Kwanini mwanamke tajiri naye huolewa?

Maana kama vile Kuna tatizo kwa mwanamke masikini akipata kitu kwenye mapenzi/mahusiano/ndoa.
 
Shukrani sana mkuu kwa uzoefu. Labda nikupe tu sababu chache za kumuamini.
1. Namfahamu tokea kitambo kidogo (2006). Sijawahi sikia skandali.

2. Wakati namuoa seven years nilimkuta akiwa bado sealed. Hope you understand

3. Hana mambo mengi. Anaweza akakuachia simu yake ukakaa nayo hata siku nzima. Akikosea akaelekezwa, huwa anakiri makosa na kuomba msamaha, maisha yanaendelea.

4. Ana hofu kidogo ya Mungu. Huwa anajitahidi kufunga na kuomba.

5. She has brains you can trust. Siyo elimu ya darasani tu (PhD) lakini ana akili ya maisha pia.

6. Ni mpole na mkimya sana.
7. She has her own salary na sio mara moja au mbili alishaniboost project zangu zilipogoma.

Sio kwamba hana madhaifu, anayo, ila tokea nimemuoa mpaka sasa yanavumilika. Siwezi sema hatobadilika, I'm not a prophet. Will deal with the future kadri itakavyokuja.
 
Mfumo dume bado upo na utaendelea kiwepo, kuna nchi tendo ya ndoa mwanamke ndio anaamua akipe au asikupe na ukim force akienda police umekwisha
 
Watu mnajiamini aisee.

Kwanini basi msiandike majina ya watoto!??
 
Mpe pesa yenye thamani ya kiwanja chake ndiyo heshima itafuata mkondo wake,wanawake akili zetu tunazijua wenyewe
 
mi najua hati huwa ni ya kiwanja, mmiliki wa kiwanja ndo mwenye haki
sasa wewe jombaa unajengaje kwenye kiwanja cha mwanamke
 
mi najua hati huwa ni ya kiwanja, mmiliki wa kiwanja ndo mwenye haki
sasa wewe jombaa unajengaje kwenye kiwanja cha mwanamke
Acha tu sikujua hizo changamoto zingetokea. Ila hili limenivuruga kabisa. Yaani aliposema sema tuandike Majina yetu wote akapendekeza pia na kile kiwanja changu tufanye hivyo hivyo pia. Aise ni mtihani mkubwa.
 
Akikubali ushauri wa kurejeshewa pesa aliyonunulia kiwanja, mpe haraka sana kabla hajabadili wazo, kisha muandikishane upya mauziano (ingawa ni mkeo). Hakawii kukugeuka. Nawasilisha
 
Nimeona michango mingi ya watu ila sijaona ushauri wa Kisheria
Kama kuna mwanasheria Mbobezi na mzoefu naomba atuletee ufafanuzi wa kisheria juu ya hili
(nimesema Mwanasheria Mbobezi na mzoefu ni kimaanisha, kuna baadhi ya sheria huhitaji uzoefu zaidi ya mistari mtu aliyokaririshwa darasani)
 
Fangs kymwachia hio nyumba

Kwanza itakuwa ya wanao kwa vyovyote vile .. wewe Anza mchakato tafuta kiwanja chenye Jina lako na ujenge nyumba Yako ingine uwe na umiliki wa 100% utairithisha kwa wanao vile vile
 
Nakwambia kwa uzoefu kama unaamua mke wako kila.kitu uandike kwa jina lake umejiroga.bora ungeandika kwa majina ya watoto.

Kama una hela tafuta na mali zako za siri lakini usisahau ilitokea la kutokea mnagawana pasu.

Aisee ndoa ni majanga.
At least nashukuru Mungu wanawake wenye akili BADO wapo!
 
Kwa sasa amekubali tuandike Majina yetu Mimi na yeye hataki tuwaandike watoto. Lakini anataka tuandike hivyo halafu na kile kiwanja changu tuandike hivyo pia. Nyumba yenyewe sijamalizia naanza kufikiria kumwachia japo nawafikiria wanangu.
 
Safi Sana mkuu maamuzi mazuri
 
Kwa sasa amekubali tuandike Majina yetu Mimi na yeye hataki tuwaandike watoto. Lakini anataka tuandike hivyo halafu na kile kiwanja changu tuandike hivyo pia. Nyumba yenyewe sijamalizia naanza kufikiria kumwachia japo nawafikiria wanangu.
Usikubali mkuu!

Andika Watoto TU!!

Kama ndoa ina migogoro usikubali huo mkenge!!!



Mtaviziana kama wachawi vile!


Mwanamke anayepinga wanawe wasiandikwe kwenye hati ni hatari Sana!!

Kinachomfanya aogope kufanya Hivyo Ndio hatari Zaidi!

Wachout!
 
Wanaume tunapitia magumu sana, mm sikupi pole ila nakushauri uendelee kuwa na msimamo wa unachokitaka.

Ukijilegeza tu UMEKWISHA.
Alikosea jambo moja.
Ni onyo kuchangia fedha au mali na mwanamke.
Alikosea sana kujenga nyumba kwenye kiwanja cha mwanamke.
Mimi mwanamke akiniambia tuchangie fedha kwa ajili ya jambo fulani, yeye afanye yake na mimi yangu.
Tulikutana ukubwani kwahiyo lolote linaweza kutokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…