Mrejesho: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga

Mimi nashauri andikeni majina yenu wote wawili.
Umiliki usomeke Mke na Mume hii itapunguza malumbano na mvutano usio na maama pia siku umeondoka(siombei utangulie kufa) Mkeo hatopata usumbufu au dhuluma kutoka kwa ndugu
 
Sure!! Kuna jamaa alimfuma mwanamke na mwanaume ndani. Akaanza kumfokea yaani wewe unafanya ufuska ndani ya nyumba yangu.... Mwanamke akamuuliza una nyumba wewe?? Ugomvi mpk Serikali ya mtaa. Mwanamke akatoa vielelezo jamaa kaja kumsumbua kwake kwakua amezaa nae anataka ahamie kwakw. Kiukweli jamaa ndo aliyetoa pesa za kununua kiwanja na ujenzi ila alikua anamtuma mwanamke asimamie.
Aiseh jamaa aliondoka mikono nyumaa.
 
Hapo muandike majina yenu wawili wote ni wamiliki wa hiyo nyumba au muandike watoto.
 
Aisee pole sana (ingawa hii mada sijaiona kwa wakati muafaka ila lazima nichangie kidogo pia ili wadau wengine wapate uzoefu kwa yanayotukuta sisi wanaume.
Kwanza kwa ushauri kuhusu mgogoro wenu aisee naomba ukomae NA msimamo wako.Mimi nilioa mwaka 1999 mke ambaye alikuwa NA mtoto wake wa kiume.
Yeye alikuwa anafanya biashara NA Mimi ni mtumishi.Kwa vile tulikuwa hatukai sehemu moja Siku moja week end nilikuja nyumbani tulipokuwa tumepangisha nakumbuka ulikuwa mwaka 2010! Akaniambia mume wangu nimesikia kuna kiwanja kinauzwa naomba twende tukakiangalie basi tukafuatana nikakiona NA nikaridhika nacho ila nikamuambia kwa sasa sina fedha akadai anayo akiba kdg tukinunue nikaridhia lakini nikamwambia usije ukaniletea matatizo baadae! Akasema hakutakuwa na shida yoyote BASI tukatafuta mashahidi tukaweka utaratibu tukakinunua kwa fedha yake.
Tulianza ujenzi kwa kishirikiana akipata fedha inatumika kwenye ujenzi NA Mimi Hali kadhalika.
NYUMBA iliisha tukaweka umeme tukahamia.Siku za baadae kidogo nakumbuka tulikuwa uani tunawapa chanjo kuku akanitamkia ya kuwa Nioe nimuache pale NA watoto wake (Yaani wawili
tuliozaa pamoja NA yule wakufikia) Nilistaajabu nikamwambia umri huu!
Siku zilizofuata nilishtuka nikanunua kiwanja kwa fedha yangu nikakiacha kilikuwa NA msingi wa vyumba vitatu !
Watoto walipokua NA kuajiriwa mke akaanza ujeuri NA nahisi aliwa feed watoto kuwa NYUMBA ni yake. Siku moja nilipokuwa nakagua nyaraka mbali mbali nikagundua ameiba hati ya kiwanja NA kuihamisha.....Nilichukia nikaanza ujenzi kwenye kiwanja changu mwaka 2021 January! Ile NYUMBA imeisha kiasi nimeweka umeme NA kuondoka pale nyumbani. Hakuridhika ila niliona niache ile NYUMBA tusije mwisho tukauana bure!
MY TAKE Wanawake sio wakuamini sana nakushauri uweke msimamo wa kutumia jina lako kwenye hicho kiwanja kwa kuwa dalili zinaonesha uzeeni utanyang'anywa hiyo NYUMBA.Au kama unaweza iache ilivyo utafute kiwanja ujenge nyingine hata kama ndogo Heshima itarudi!
 
Pole sana mkuu.
 
Sakata lako linafanana na la kwangu. Hapa naanza kudunduliza nikatafute sehemu yangu nitoke hapa nimwachie nyumba yake. Maana nishadhalilishwa hapa ninapoishi sema navumilia kwa sababu nipo kwenye mchakato wa kutafuta hela niondoke.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu soma maelezo yangu hapo juu ujifunze kitu maana tumekutana kwenye shida zinazofanana .Au nitafute in box .
 
Huo ndio uamuzi wa busara Mimi mungu ameona kilio changu nilipanga matofali kwa hasira nikasepa bila kuchukua chochote ,furniture zangu niliona isiwe shida nimeanza upya.Umeme nilifungiwa mwezi wa name mwaka Jana.Unajua yatakayokukuta?
(1) Heshima kwa hao watoto wako kwako itapungua
(2)Unaweka maisha yako rehani ni rahisi kufanyiwa lolote ili utoe nafasi ya umiliki huria wa NYUMBA.Chunga sana chukua tahadhari.
(3) Ukikubali kuishi hapo itakubidi uwe bwege fulani mnyenyekevu kupita kiasi .Utadeki,utafua bikini,utapeleka maji bafuni,mbaya zaidi kama mkeo katangaza hii issue kwa marafiki,majirani n.k utadharaulika kila mahali.
Yote hayo ya nini?
 
Baada ya kumaliza kusoma bado naendelea kujiuliza wewe ni mwanaume au ni mtu mwenye maumbile ya kiume?
 
Haaa! Mungu anawaona!!!
 
Hao watoto wako Leo ni watu wazima kesho.Kumbuka katika malezi mama Yuko karibu zaidi NA watoto kuliko wewe! Atawajengea taraaaatibu concept hao watoto kuwa baba hukushiriki kujenga chochote hapo then watoto watakudharau sana.Then hilo penzi litapungua kadiri age inavyopanda uzeeni hakuna mke NA mume kuna mwenza.!kwa sababu huwezi kumringia chochote.Huwezi mtuma apeleke maji bafuni kwa sababu wote magoti yanawauma n.k Utageuzwa mgeni kwenye hiyo NYUMBA believe or not....Talk through experience.Kuumizwa ktk mahusiano hakujaanza Leo fainali ni uzeeni.Udhaifu wowote utaulipia uzeeni! (Any way napita tu!!!)
 
Je huyo mtoto akiwa mkiritimba si atawadhulumu ndugu zake on the way?
 
Jiandae kufukuzwa siku ukifulia 😀😀😀 najua una lengo zuri ila huwajui wanawake wewe. Ipo siku huna nguvu tena za kujenga wala kutmba atakutoa kama mbwa hapo kwako.
 
Akipata jamaa tu nje akakolezwa vizuri ndugu yetu atafurahia show🤣 katika kosa ambalo siwezi kuafiki ni nyumba iwe kwa jina la mke. Bora tumuandikie mtoto tu ili iwe yake kama atakuja kuiuza shauri yake.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Jamaa anataka kutesti sumu kwa kuilamba
 
Wanawake ni vichwa maji sana. Yani kubadilika ni dakika 0 tu anaweza akachotwa akili na mpuuzi flani tu huko nje. Akavuruga na ndoa yenyewe ili abakie na nyumba na watoto wewe uondoke maana unambana bana kuspend na mshenzi mwenzie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…