Mrejesho mtaji wa laki 3: Nimeamua kuuza biashara ya matunda na genge

Mrejesho mtaji wa laki 3: Nimeamua kuuza biashara ya matunda na genge

Mimi alikua ni mdada😃,, aliandika Uzi mrefu Sana kwamba kwa tatizo lake lilipofikia anaona tu bora afe.... Nikaguswa nikamfata pm kumuuliza Shida Nini akaniambia amepata ajali amevunjika mguu hawezi hata kutembea na hela hana ya kwendea hospital, nikaona story Kama haimake sense flani hivi,, nikamuhoji hoji akabadili akasema ni mama yake kijijini na sio yeye.. nikaanza kuwaza huyu atakua ni tapeli,, nikamwambia nitakusaidia hatakama ni wewe na mama yako wote mpo ndani ya uwezo, nendeni hospital wawape control namba niwalipieni, akakataa akaanza na kunisema eti Kama Sina hela au Kama sitaki kumsaidia nisimchoshe anaadika huku anaumwa... Nikamwambia tu sawa nikaachana nae., Baada ya sikumbili nafungua pm nakutana na matusi hayo page nzima
😊😊Anaweza kuwa me pia,yaani wanatufanya watu wenye empathy kuishi kwa shida sana.
 
S
Habari Za uzima Wana jamii wenzangu Mimi ni Yule mdada nilieleta wazo langu kuhusu biashara Kwa mtaji mdogo WA laki tatu Tu..mashukuru nmepata mawazo mazuri nmefatilia Kwa utulivu nanimesoma maoni ya kila mtu ..maoni yangu Ni nmeamua sasa kuuza biashara ya Matunda Na genge mpaka sasa nmefatilia process ya kupata eneo nmepata sasa nafatilia utengenezaji wa Banda la kawaida Tu ambalo naomb Mungu lisimalize laki moja Na mtaji wangu Nataka ubaki Kama laki moja Tu iyo ndo nitaanza nayo matengenezo mengin ntatengeneza Kadri Mungu atavyonijalia Asante San mmenifungua mawazo nilikuwa Nawaz Sana ...kitu chakufanya kila nikiwaza nashindwa kutoka Na mtaji kuwa Ni changamoto.. NB tuweni Makini umu ndani sio wote wema wakati nipo kwenye mchakato alitokea mtu uku DM akahaidi kunipa kazi nilifurahi Sana kazi yenyew Ni ya sheli Na akadai IPO arusha Kama kawaida mimi nilimsikiliza ..akaniunganisha Na meneja feki ILi wanitapeli ela Ni story ndefu siwez kueleza Lakin mwisho wa siku uyu boss akaomb ela ya uniform Kama sh laki 1 Na elf 30 ..Dah Mungu Yuko upande wangu sikufanikiwa kutuma nadhani ningetuma Leo ningekuwa Na majonzi mapya ...my take ..mtu kaomba ushauri afanye nini ILi ajikomboe Na Maisha Na utegemezi sasa usiwe Tena chanzo cha kumrudisha nyuma uyu mtu Asanteni Na nawatakia siku njema
Pole sana , ila kuna watu wa hovyo ndio maana unakuta mtu siku zote ana majanga au anakufa kifo kibaya ndio hivi mtu ana shida na wewe unataka kumdhulumu

Huyo tapeli anika ID yake tumjue
 
Kwa screen shots ulizoweka,jamaa kasema kama huamini,alikutaka uende Arusha,ila ukiwa na hiyo pesa,lakini pia aliandika kua yawezekana baadhi ya watu wa uongozi pale sheli,wanataka walau pesa ya kula,ndomaana wamesema laki na 30 ya yunifom.Anyway huyo wiztech,aje ajitetee hapa kama hakua na nia ya kutapeli.Hii itamsafisha.
 
Back
Top Bottom