Mimi alikua ni mdada😃,, aliandika Uzi mrefu Sana kwamba kwa tatizo lake lilipofikia anaona tu bora afe.... Nikaguswa nikamfata pm kumuuliza Shida Nini akaniambia amepata ajali amevunjika mguu hawezi hata kutembea na hela hana ya kwendea hospital, nikaona story Kama haimake sense flani hivi,, nikamuhoji hoji akabadili akasema ni mama yake kijijini na sio yeye.. nikaanza kuwaza huyu atakua ni tapeli,, nikamwambia nitakusaidia hatakama ni wewe na mama yako wote mpo ndani ya uwezo, nendeni hospital wawape control namba niwalipieni, akakataa akaanza na kunisema eti Kama Sina hela au Kama sitaki kumsaidia nisimchoshe anaadika huku anaumwa... Nikamwambia tu sawa nikaachana nae., Baada ya sikumbili nafungua pm nakutana na matusi hayo page nzima