Mrejesho mtaji wa laki 3: Nimeamua kuuza biashara ya matunda na genge

Mrejesho mtaji wa laki 3: Nimeamua kuuza biashara ya matunda na genge

Mimi alikuwa ni mdada, aliandika Uzi mrefu Sana kwamba kwa tatizo lake lilipofikia anaona tu bora afe.... Nikaguswa nikamfata pm kumuuliza Shida Nini akaniambia amepata ajali amevunjika mguu hawezi hata kutembea na hela hana ya kwendea hospital, nikaona story kama haimake sense flani hivi, nikamuhoji hoji akabadili akasema ni mama yake kijijini na sio yeye.

Nikaanza kuwaza huyu atakua ni tapeli, nikamwambia nitakusaidia hatakama ni wewe na mama yako wote mpo ndani ya uwezo, nendeni hospitali wawape control namba niwalipieni, akakataa akaanza na kunisema eti Kama Sina hela au Kama sitaki kumsaidia nisimchoshe anaadika huku anaumwa... Nikamwambia tu sawa nikaachana nae., Baada ya sikumbili nafungua pm nakutana na matusi hayo page nzima
Heeeee 😂😂😂😂
 
Habari Za uzima Wana jamii wenzangu,

Mimi ni Yule mdada nilieleta wazo langu kuhusu biashara Kwa mtaji mdogo WA laki tatu Tu. Nashukuru nmepata mawazo mazuri nmefatilia Kwa utulivu na nimesoma maoni ya kila mtu. Maoni yangu Nimeamua sasa kuuza biashara ya Matunda Na genge mpaka sasa nmefatilia process ya kupata eneo nmepata.

Sasa nafatilia utengenezaji wa Banda la kawaida tu ambalo naomba Mungu lisimalize laki moja Na mtaji wangu nataka ubaki Kama laki moja Tu hiyo ndo nitaanza nayo, matengenezo mengine nitatengeneza Kadri Mungu atavyonijalia.

Asante sana mmenifungua mawazo nilikuwa Nawaza Sana kitu cha kufanya, kila nikiwaza nashindwa kutokana mtaji kuwa Ni changamoto.

NB: Tuweni Makini humu ndani sio wote wema wakati nipo kwenye mchakato alitokea mtu huku DM akaahidi kunipa kazi nilifurahi Sana kazi yenyewe ni ya sheli Na akadai IPO Arusha. Kama kawaida mimi nilimsikiliza akaniunganisha Na meneja feki ili wanitapeli hela.

Ni story ndefu siwezi kueleza lakini mwisho wa siku huyu boss akaomba hela ya uniform kama sh laki 1 na elfu 30. Dah Mungu Yuko upande wangu sikufanikiwa kutuma, nadhani ningetuma leo ningekuwa Na majonzi mapya.

My take: Mtu kaomba ushauri afanye nini ili ajikomboe na Maisha Na utegemezi sasa usiwe Tena chanzo cha kumrudisha nyuma huyu mtu.

Asanteni na nawatakia siku njema

Pia, soma=>Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?
Mkuu! Usiweke wazi mambo yako! Ongea kwa ujumla na chambua tekeleza kisirisiri! Waliofanikiwa kibiashara hawawezi kukwambia wamefanyaje mpaka wakatoboa! Watakwambia kiujumla! Sasa wewe jianike utatuletea mrejesho!
 
Kwa screen shots ulizoweka,jamaa kasema kama huamini,alikutaka uende Arusha,ila ukiwa na hiyo pesa,lakini pia aliandika kua yawezekana baadhi ya watu wa uongozi pale sheli,wanataka walau pesa ya kula,ndomaana wamesema laki na 30 ya yunifom.Anyway huyo wiztech,aje ajitetee hapa kama hakua na nia ya kutapeli.Hii itamsafisha.
Alisema hivyo sababu alijua hawezi kufumga safari toka Dar mpaka Arusha kwenda kupeleka hela tuu, so lazima option ingekuwa kumtumia pesa tuu. Hiyo ni strategy ya kumwaminisha ili dada aone kweli ni serious
 
Nilishenzi sana hili lijitu linajiona eti linajua kuungishia watu kazi lina shida sana oh nakampuni sijui nini naweza kukupa kazi na yupo arusha nilikitu lishenzi sana nilitapeli liliniahidi kazi mwezi 6 na 11 kila muda ukifika ananiblock anadai humu nimtu tajiri sana kumbe marioo tu bora hata huyu mwingine alikuwa mshirikina ila hakuwa mwongo
 
V
Nilishenzi sana hili lijitu linajiona eti linajua kuungishia watu kazi lina shida sana oh nakampuni sijui nini naweza kukupa kazi na yupo arusha nilikitu lishenzi sana nilitapeli liliniahidi kazi mwezi 6 na 11 kila muda ukifika ananiblock anadai humu nimtu tajiri sana kumbe marioo tu bora hata huyu mwingine alikuwa mshirikina ila hakuwa mwongo
Vipi tena dada
 
Back
Top Bottom