Inategemeana una nunulia wapi au Kijiji gani, lakini Kwa upande wa mahindi Kuna center maalufu sana ya mahindi na apo ndo wanunuzi wa Mahindi wanapo kuja wanafikia hapo. Wanunuzi kutoka nchi za jirani na Mikoani wote wanapenda kufikia hapo. Maana yake ni kwamba hapo ndipo yalipo mghara ya kuhifadhia nafaka kwaiyo Kuna wale wanao enda kununua uko Kwa wakulima na kuleta kuuzia hapo, au ukipenda uwende kununua huko ni sawa.
Mara nyingi kama unataka Mzigo mkubwa unaingia huko ndani ndani unanua Kisha unachukua Trektor ya kusogeza pale. Kulingana na miundo mbinu uwezi kupeleka Semi trailer uko ndani ndani itakwama, Magari makubwa Yana park pale na kunakuwa na matrector ya kutoa kule mashambani na kusogeza pale.
Kuhusu miundo mbinu ya Barabara, kwakweli Barabara ni nzuri tu kama unatokea mikoa mingine kufika Mpanda mjini. Kutoka mjini kuja wilaya ya Tanganyika Barabara ni rough road lakini inapitika vizuri hadi kufika kwenye hizo center.. Kama Kuna kitu nimesahau kujibu uliza. Asante sana.