Mrejesho: Safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Habarini za jioni wanajanvi, ni jioni nyingine tena baada ya shuruba za siku nzima, nimelejea tena tuendelee na mrejesho wangu. Lakini kuna watu humu wenyewe ni watu wa kuongea maneno ya kukatisha tamaa, ohhh mara uyu sio mkulima, mara uyu hakuna kitu.
Ngoja nikwambie ndugu yangu, kama humu tungefahamiana Kwa majina ungecheka sana, maana Kuna watu humu akitoa comment unaweza kudhani maisha ameyapatia kumbe nae bado anajitafuta na pengine bado anazungusha Cv na kulilia ajira, kumbe hajui kazi zipo lakini ajira hakuna.
Tunaendelea....... Nipo mwanza sasa baada ya kumaliza kusafishia SHAMBA na nikaona muda bado mrefu nikaamua kurudi mwanza kwaajiri ya kufanya kufanya manunuzi ya vitendea kazi lakini pia kwenda kumuona mtaalamu furani aweze kurekebisha mambo flani [emoji16],kumbuka unaingia vitani.
Basi tarehe za mwanzo wa mwezi wa tisa safari ikaanza kurudi KATAVI. Hapo mimefanya manunuzi ya Kila kitu kuanzia majembe, panga, solo pamp, madawa ya wadudu, mbegu za mahindi aina ya DK 719 TEMBO BABA LAO,dawa za magugu, maturubai kwaajili ya kambi, vyombo vya kupikia, dawa za aina mbalimbali kama Malaria, tumbo, dawa za vidonda, nyembe, sindano za viatu na nyuzi, sindano ya mkono,kumbuka kule ni shambani hakuna chereani, kwaiyo hata nguo ya kazi ikichanika nashona mwenyewe, au Farm boots imepasuka nashona mwenyewe like that wadau. Ndo maisha ya SHAMBA hayo.
Yani ni kwamba sikutaka kuwa napoteza muda kitu kidogo tu hadi niende MWESE NO4, kumbuka kule ni shambani ukiingia umeingia, maitaji kuyapata Yako mbali, Yani nilifungansha Kila kitu ambacho kingeitajika kwenye kambi yangu, kumbuka hapo nikifika ni kujenga kambi yangu kule shambani yani nikae kule shamba, maana nilifikiria mvua zikianza kunyesha ningesumbuka sana kuwa natoka kule kuja shambani pili kingine kilichonifanya kujenga kambi ni kitendo Cha Jamaa yangu Kasukari ninapotoka SHAMBA unakuta nae amekwenda shambai na tunapisha muda wa kurudi. Lakini kikubwa zaidi ni mtu ambae tulikuwa hatujazoena maana alihisi pengine ni wale vibaka wa Town kumbe Mimi Sina iyo tabia.

11.SAFARI YA KURUDI MPANDA KUTOKEA MWANZA HAWAMU YA PILI.
Basi ndugu zangu zafari ikaanza kutoka mwanza kwenda Mpanda, wakati wa kurudi nilipanda Bus ya Nyehunge Express, majira ya jioni tukaingia Mpanda, sasa nikafikiria nikisema niende Kwa Jamaa yangu yule wa hapo Town nitahangaika na mizigo kwenda kwake,maana kulikuwa ni mbali.Nilimpigia simu tu akaja pale stand tukasalimia nikampa zawadi ya dagaa wa mwanza, Yani jamaa yangu alishukuru sana.
Kumbuka nimefika jioni na magari ya kwenda MWESE NO4 hayakuwepo muda huo maana yake ni kwamba hadi kesho yake asubui, hivyo nilikesha pale stand na ndugu zangu wasukuma, Yani nyomi ya wasukuma wanahama kutoka mikoa mingine kuja Mpanda Yani ni vurugu tu Kila mahari.
Nilikesha hapo, hatimaye kukapambazuka salama. Kwakuwa Kuna vitu baadhi sikununua mwanza niliona tiaenda kununua kule, mfano misumari ya kujengea kambi, nyundo na vitu kama nyanya, vitunguu, mafuta ya maweze nk. Maana kule mafuta ya maweze yanatumika sana ukanda ule na pia yana Bei nafuu.
Basi mnamo majira ya saa3 asubui nikawa nimemaliza manunuzi yangu na nikachukua bajaji ya kwenda hadi kule Stand ya Mizengo pinda kwenye ofisi za Nyehunge Express nilipoacha mizigo yangu. Tulichukua na kuelekea stand kunakopaki magari madogo ya kuelekea vijijini, nilipandisha mizigo yangu na baada ya muda mchache gari ikaanza mwendo.
Labda niseme kwamba Yani nilifanya manunuzi ambayo Kuna vitu baadhi Hadi namaliza kilimo Kuna vitu nilikuwa navyo na niligawaia rafiki zangu kama vile Dotto Msukuma, Mfipa wa sumbawanga, ndugu yangu Kasukari na Mzee mwenye SHAMBA, hao nilio wataja utaona mbeleni ni jinsi gani waligusa maisha yangu njkaamua kuwapa baadhi ya vitu nilivyo bakiza kambini.

12.NIMEFIKA MWESE NO4 HAWAMU YA PILI TENA.
Baada ya kuwa nimefika mwese nilichukua pikipiki tukafunga mizigo kupeleka Kwa yule Jamaa niliefikia mara ya kwanza wakati namsubiri Jamaa yangu Kasukari kuja kunipokea, kama unakumbuka mwanzo siku nafika Mwese mara ya kwanza. Basi tukafika Kwa uyo jamaa nikamkuta, kwakweli pia ni poa sana. Baada ya kufungua mizigo nilitoa mfuko wenye dagaa kilo Moja na mafuta ya maweze Lita Moja na chumvi nikamkabidhi mke wake. Yani walifurai sana, sometimes unajiongeza Ili kujenga urafiki,sio unakaa kaa tu kama kama mzoga.Kumbuka wakati naanza safari ya kutoka kule Mpanda nilikuwa niwasiliana na Jamaa yangu Kasukari kwamba atakuja kunipokea na kunisaidia mizigo kushusha kule IGONGE na nilimwambia ningempa chochote na alikubali lakini kitu cha kushangaa nilipofika nikipiga simu haipatikani hapo imefika sa kumi na moja na nusu, alafu kumbuka kuelekea kule unapita msituni ingawa hakukuwa na wanyama wanaodhuru. Basi nikaona uyu jamaa pengine amekwama kuja hivyo nikapangua zile mizigo miepesi nikafunga na begi langu mgongoni na Toch Kali yenye mwanga safari ikaanza wakati huo Nina redio yangu nikipiga wimbo wa Rose mhando.... Woga ndo umaskini wako mwanangu.. malengo yako utakamilisha vipi we kijana... Kila kitu unasema uwezi uwezi.. kwani wengine waliweza vipi we kijana... Kutwa kucha unashindana na Jua, Jua likisogea na wewe unasogea.... Kivuri kikisogea na we we unasogea... haujui kupambanua nyakati we kija... Jifunze Kwa walio fanikiwa kijana..... Umejiloga mwenyewe ehheeeeeeee... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.
Hatimaye nikafika Kwa ndugu yangu Kasukari, nilikuta amefunga geto naona alikwenda pia shambani, maana alikuwa amelima maharage ya bondeni ambayo wanamwagilia kutumia mifereji kutoka kwenye mto. Basi muda si mrefu akawa amefika na akaanza kuniambia Mwamba!! Yani nilishindwa kuja nilikuwa napulizia sumu ya wadudu kwenye maharage pole sana Mwamba. Namimj hakuna shida, nikamwambia Jamaa yangu chukua mazaga humo upike maana Mimi nimechoka sana.Kumbuka baada ya muda wa wiki kadhaa mbeleni niliamia kambini kwangu na niliondoka na mizigo yangu na zile dagaa nilizo mpa ilikuwa ni mboga yake,hivyo nilimwambia hizo dagaa zake atunze tu maana yake ni kwamba tungekula dagaa zangu Hadi naondoka pale kwake nilikuwa na dagaa wengi sana.
Tulimaliza kula na kujiegesha , maana yake Ile sio kulala yani unaamka asubui mbavu zikiwa zinauma kinoma, kumbuka kitanda Cha miti ya mianzi na juu ni godoro la nyasi yani mwanaume unatakiwa ujikubali popote na kwalolote katika maisha.
Kukapambazuka salama lakini kumbuka Kuna mizigo zangu zilibaki kule kijijini, hivyo Kuna wajukuu wa yule Mzee Yani ni watoto wa vijana wa yule Mzee.Kwaiyo niliongea na baba yao nikachukuwa vijana wawili tukapandadisha kijijini. Nikisema kupandisha acha kushanga[emoji3064][emoji3064] ni msemo ambayo inatumika kule mashambani.Utasikia oya Mwanangu unapandisha kijijini? Na Mimi ndio!! jamaa ngoja nikuagize chumvi na kiberiti Kwa GAMA. Uyu Gama ni Mangi mmoja maarufu sana pale kjjijini Yani uwezi kwenda kwenye Duka lake ukakoswa kitu Yani hata pilipili utaipata inauzwa na Huduma zote za miamala ya kifedha Kijiji kizima hadi vijiji vya jirani wote ni Pale. Anauza Jumla na reja reja, yani anapiga pesa ni balaaa.
Basi ikabidi niwape pesa wale madogo tukapandisha kijijini, tulifika nikawapeleka kwanza mgahawani kunywa chai yani madogo walivyo rudi kwao walikwenda kusimulia makwao, maana chai ni kitu hadimu kule mashambani. Baada ya kumaliza kupata chai tulienda kuchukua mizigo na safari ya kurudi ikaanza, kabla ya hapo tulipotoka kupata chai tulikwenda Kwa uyo Mangi mwenye duka Ili kwamba niweze kuweka Salio la kutosha kwenye simu yangu iwe vyepesi kuwa nanunua muda wa maongezi juu Kwa juu maana kule hakuna vocha na pia niliweka Salio la M PESA Kwa kunilaisishia kuwa nalipia mtambo wangu wangu Solar kutoka kampuni x maana niliununua Kwa mkopo unalilipia kidogo kidogo. Niliuchukua Kwa ajiri ya Matumizi ya kambini kwangu, kuchaji simu na kupata mwanga. Kumbuka kule hakuna umeme.Safari ya kurudi shambani iliwadia na wale madogo Kila mtu akabeba Mzigo wake na tukafika salama Kwa jamaa yangu Kasukari.
Jifunafu asante sana kwa story yako. Najifunza mengi. Ushauri: naona kama unatumua muda mrefu sana kuelezea matukio kw undani hivyo inaweza kuchukuwa muda wako kuelezea mambo yote. Jaribu kusimulia maeneo muhimu bila ku-compromise utamu wa simulizi.
 
Radi zipo Kila mahali, lakini kama hauna baya na mtu haikufanyi chochote. Lakini kunavitu vya kukinga kama imekuja Kwa ubaya inapita kushoto.
Kule ni kali tokana na uwepo wa madini ya "Blue Tommerin". Tulikuwa tukiendaga na Pinda, tukuona Mawingu tu tunamkimbiza haraka haraka kumtoa ukanda ule wa Mwese.
 
13.KAZI YA KUANZA KUJENGA CAMP KULE SHAMBANI KWANGU.
Wadau baada ya kuwa tumefika na mizigo yetu na wale madogo, ilikuwa ni siku ya Mimi kuandaa vitu flani ambavyo nilipewa na mtaalamu wangu na sikutaka jamaa yangu ajue chochote kuhusu ilo ila niliambiwa Hadi nifanye ilo jambo kule shambani ndio nianze kazi Yani Kwa ufupi nisifanye chochote kule shambani hadi niakikishe SHAMBA limekuwa na walinzi wa Babu, nikisema ivyo wakubwa mnaelewa na kazi iyo ilitakiwa nifanye majira ya alfajiri sana Yani kabla ya watu kuamka napia utakiwi kuongea na mtu hata kama umekutana nae Kwa bahati mbaya.
Nashukuru zoezi nilimaliza na kazi ya ujenzi wa kambi ukaanza.
Siku iliyo fuata baada ya kumaliza lile zoezi nilienda SHAMBA nikiwa na panga, jembe na vifaa vingine kwaajiri ya kwenda kuchora ramani ni wapi nitaiweka kambi yangu na pia kuanza kukata miti na kuchimba mashimo na kusimika miti ya nguzo. Swala la miti haikuwa tatizo maana humo humo kwenye SHAMBA la Mzee kulikuwa na miti kwenye Yale mashamba ambayo hayajalimwa kwaiyo unajikatia tu. Hivyo baada ya kuchora ramani ya kambi yangu ni wapi itakaa nilianza survey ya kuzungukia miti mizuri ambayo ingefaa kama nguzo nilifanikiwa kupata miti mizuri na imara kwaiyo nilikata na kukusanya pamoja na kuanza kusomba kusogeza pale site ambapo nitajenga camp yangu.
Kwa siku iyo nilikamilisha kazi iyo ya kukata miti, maana haikuwa ni miti mingi ilikuwa kama ishirini hivi kwani ukubwa wa kambi yangu ilikuwa ni chumba na sebule lakini vidogo tu sio vikubwa sana, Pia nilimpatia kazi jamaa mmoja Mfipa wa sumbawanga kazi ya kunikatia MIANZI ambayo ningetumia kuzungushia pembeni na kupiga juu Kwa kutumia misumari.Mlio Kaa shambani mtaelewa miti ya mianzi. Kumbuka sikutumia kamba maana nilikuwa nime nunua misumari kilo mbili mchanganyiko kulingana na Kila kazi. Nilimaliza kukata miti na kusogeza na nikarudi magetoni kwenda kurekebisha msosi Ili kwamba saa tisa nirudi kuendelea na kazi ya kuchimba mashimo na kusimika nguzo.
Around saa tisa nilirudi shambani Ili kunza kuchimba mashimo na kuweka nguzo wakati huo yule Mfipa wa sumbawanga anakata mianzi na watoto wake wanasogeza pale site. Uyo jamaa nilimkubali na nilikuwa nampa kazi zangu nyingi maana alikuwa na familia kubwa ya watoto kwaiyo ukimpa kazi muda mchache anakukabidhi,yani alikuwa ni mtu poa sana maana na yeye ndo alikuwa ameamia pale akitokea sumbawanga. Hivyo hakuwa na sehemu ya kupata pesa na pia alikuwa Hana,maana yake ndio wakati alikuwa amefika na alikuwa ajalima mazao kwaiyo alikuwa akitegemea apate kazi ndio apate maitaji ya kuhudumia familia yake.Alipambana jioni iyo lakini akumaliza idadi ya mianzi niliyo itaka ilikuwa ni mingi sana Kwa sababu ingefanya kazi ya kuzungushia uzio kwenye kambi yangu. Sikutaka camp yangu ikae vibaya Yani nilitaka niwe ndani ya usalama ukizingatia kule ni maporini.
Siku iyo nilifunga kazi na kurudi nyumbani kwani Jua lilizama na Kazi ikaishia pale.

Asubui nitaendelea wadau ......Ngoja nilale.

Tunaendelea ndugu zangu lakini nitafupisha hii story kulingana na maoni ya wadau wengi.Hivyo nitasimulia vipengele mhimu mengine nitayaacha kulingana na mazingira niliyonayo muda wa kuandika full time unakuwa ni mchache sana.

14.UJENZI WA CAMP UMEKAMILIKA.
Baada ya kuwa ujenzi umekamilika na kazi ya kukandika tope niliwapa familia ya yule mfipa wa sumbawanga, walimaliza siku iyo na baada ya siku ya nne nikaweka tulubai.Niliweka zile tulubai nyeusi kama nailon yani zile hata kama mvua ingekesha inanyesha hakuna tone la maji litaingia ndani,ila kuna siku mvua ya mawe ilinyesha nilitaka kuchanganyikiwa.
Basi baada ya kukauka nikapiga tulubai ju na kutengeneza mlango kwa kutumia mianzi pia nikachimbia miti ya kitanda na kupigilia misumali yani kitanda kikamilika na godoro yangu ya wanafunzi juu,yani life likaanza fresh tu..
Wakati mfipa amemaliza kukata mianzi na kusogeza nikampa kazi ya kutengeneza uzio kuzunguka kambi yangu,kwakweli camp yangu ilikuwa ni mfano tosha yani raia walikuwa wanajua uyu mwamba ni mwanajeshi.Tayari campimekamilika na baada ya siku tatu nikaamia kwangu.

15.MAISHA NDANI YA CAMP YANGU YAMEANZA.
Nikaamia rasimi shambanj kwangu,basi maisha yakaanza kabla kuingia kunza kuandaa shamba nililima matuta kadhaa karibu na mto ili niwe napata mboga za majani,nilipanda mchicha,nikasia mbegu za chainizi na mbegu za cabages.Niljfanya hivyo iwe raisi kuwa nabadirisha mboga kwani mboga yangu kubwa ilikuwa ni dagaa.
Maandalizi ya kuchimba mashimo shambani yakaanza,kumbuka sukuweka watu wa kima kwanj shamba lilikuwa ni tifutifu mno kwaiyo nilianza kazi ya kuchimba mashimo nikitumia kamba na vipimo sahihi.
Wenyeji walikuwa wakinishanga mno uyu jamaa amechanganyikiwa? yani jua lote hili hata mvua bado yeye anaweka mashimo kumbe hawajui mimi nilikuwa na plan B kichwani.Nilifanya kazi iyo kila siku asubui na jioni hadi nikamaliza ekari mbili zikawa tayari.
Mchicha unaendelea vizuri nikaanza kuchuma na mbegu za chainizi na cabage zikiendelea vzr pi.
Kuna ekari moja ambayo ilikuwa sijaisafisha na ilikuwa na magugu yale magumu,nilikuwa na round up ile ya kuua magumu nikapuliza shamba zima baada ya wiki moja yote yakakauka nikachapa moto,kazi ya kuchimba mashimo ikaendelea pia.Najua wengi mtabisha sana lakini ukweli ni kwamba kazi yoyote ukiingia kwa kuifanya na kuipenda hakika hakuna kazi ngumu,yani kuna wakati unatamani jua lisingezama niendelee kufanya kazi tu.
Nilipambana na kipande kile na hatimaye na chenyewe nikamaliza,kuna siku alikuja jamaa yangu msukuma akanisaidia kuchimba.Kazi ile ilikamilika na hatimaye dalili za mvua zikawa zinakaribia ,wenyeji wanaanza kuangaika kusafisha mashamba mimi nimetulia nawachora tu.
Kuna siku moja yule mzee mwenye shamba akaniuliza kijana utapamba mbegu gani? nikaona uyu mzee anataka kunichora kwanini ananjuliza ili swali? nilimdanganya kwamba nitapanda hizi mbegu zenu za kienyeji maana nimenunua mahindi ya kula kwa flani nitatoa debe moja la mbegu nitapanda iyo.Kumbe mimi mbegu imo geto imetulia BABA LAO TEMBO 719 ni hatariiii..ogopa.
Majira ya mvua yakafika nakumbuka mvua ilianza kunyesha mwezi wa kumi,siku iyo imepiga mchana lakini haikuwa nyingi nikasema kesho naanza kuchomeka mbegu.Jioni nilienda kwa mfipa nikamwambia kwamba,kabla wewe kwenda kuanza kulima shamba lako nakupa kazi ya siku mbili kupanda,jamaa alinielewa na moja ya mashariti niliyo mpa sikutaka kuona watoto wakiusika kwenye zoezi la upandaji kwani ilijua wangeusika watoto mbegu ingepotea nyingi kwasababu hawako makini hivyo alikuja yeye na mke wake na kijana mkubwa na binti pamoja na mimi,jumla tukawa 5,siku iyo niliandaa kuku na mchele yani ni hatari ogopaaaa.
Moja ya vitu ambavyo niliamwambia siku anakuja kupanda,ni bora mbegu moja iende kwenye shimo kuliko mbegu tatu kwenye shimo moja yani nilikuwa makini kwenye mbegu.Nilikuwa nimenunua Mbegu kilo 30 Sawasawa na viroba 15 vya kg2 .Siku iyo tulipambamba na mida ya saa nne ilibidi nimwambie yule mke wa jamaa aende kufanya maandizi ya msosi na binti yake sisi watatau tukaendelea kupambana.
Chakula kilikuwa tayari tukeanda kula na hatimaye baada ya mapumziko mafupi tukarudi kupambana tena hadi muda wa saa kumi na mbili wakatawanyika hapo zile eka mbili tukamaliza,Asante Mungu usiku huo huo mvua igagonga tena yani kwangu ikawa ni sherehe.
Najua ndugu msomaji pengine uelewi au unaona ni uongo basi endelea kuamini ivyo ivyo na pengine muda huu unaandaa cv nyingine kwaajiri ya kupeleka ofisi za DP WORLD kutafuta kazi.
Asubui niliamka mapema sana nikaanza kupanda ile ekari iliyobaki yani nilikuwa sitaki mchezo wala kupoteza muda.Nilipambana ndani ya siku mbili nikamaliza lakini kuna nusu eka ilibaki maana mbegu ilikwisha.Maana lile shamba lilikuwa limezidi zaidi ya ekari tatu,ilibidi asubui nipandishe kwenda kijiji kutafuta mbegu ya kumalizia.Nilipata mbegu ya DK 9089 nikanunua kilo4 za kwenda kumalizia,wakati raia sasa wanapambana kulima mimi mahindi yakaanza kuota.Hapo raia bado hawaelewi somo wanajisemea uyu afiki popote lazima atakwama tu.
Nilifika na mbegu yangu jioni kesho yake asubui nikaendelea kupanda lakini niliweka alama za kutenganisha kati ya mbegu ya Tembo na Dk ili kwamba nione ni mbegu gani itafanya vizuri zaidi.
Hakika nilimaliza kupanda vizuri na atimae sasa,nikageukia bustani yangu kupandikiza cabage na chainizi.
Baada ya wiki mbili na nusu nilimwambia yule mfipa aanze kupalilia lakini palizi yake nilimwambia apalilie kwa kutifulia ili kwamba kuinulia udongo kumbuka sijalima nilikatia tu kwaiyo niliona ni vema apalilie kwa style iyo.Yule jamaa na familia yake nulikuwa nawakubali yani akishika kazi yako hadi amalize ndo aendelee,alipambana wiki mbili akamaliza.
Kazi ya kupuliza sumu ya wadudu ilianza na hapo nilipambana mwenyewe sikutaka kuweka mtu,kumbuka mji yako jiranj na shamba ivyo nilikuwa nasomba mji naweka kwenye soro pump nachanganya dawa napuliza,wiki moja nikamaliza izo ekari mbili nakuru sasa kupalilia ile eka nyingine na kuna kipande cha nusu eka nilimkatia yule jamaa yangu msukuma maana alikuja akidai hana pesa ivyo nimpe kazi.Tulikuwa tunapambana kwa pamoja yeye kipande chake na mimi kipande changu,tulimaliza ndani ya wiki na nusu nikaingia kupuliza sumu.Yani kwa ufupi mahindi yalisimama hadi raia wanaopita hapo wakawa hawaelewi somo uyu jamaa vipi? Usiniulize nilitumia mbolea gani,jibu ni kwamba sikutumia mbolea yoyote nilitumia dawa za kuuwa wadudu na palizi basi.Yani kama ningeweka mbolea dukani hata mara moja yani nimengapata mara mbili zaidi.

17.PALIZI YA PILI IMEWADIA.HAPA NITATUMIA KIUA GUGU CHA HANGZHOU HAMOXONE 200 SL.
Nilitumia iyo dawa kwa sababu ya kupunguza palizi maana mvua ilikuwa inanyesha na nyasi zinakimbia kweli kweli,yani nilipambana hadi mabega yakazoea kabisa.Ebu fikiria pampu ya lt20 unajaza full ikiwa chini unachanganya dawa then unavaa pumb unapuliza.Uzuri nilikuwa nimetengeneza kama uchanja kwaiyo naipandisha pale ndio naivaa nikiwa nimesimama,nilifanya kujiongeza ivyo kwasababu hakukuwa na mtu wa.kunisaidia kuinyanyua.
Asikwambie mtu ndugu yangu kazi yoyote utaifanya kwa umakini kama ukiipenda kutoka moyoni.Nilipambana hatimae nikamaliza ekari zote na mahindi yakaanza kuchanua.

Leo nitamaliza ndugu zangu,ila nimeona mengine nisieleze maana itakuwa story ndefu sana.Pia tuvuliane katika uandishi pengine kuna makosa yanatokea.
Jioni itaendelea...............
 
Wakuu natumaini mnaendelea vyema,
Napenda kusema hili kwenye wengi Kuna mengi. Nilichojionea hapa Jukwaani Kuna watu Wana comment mengine ni kucheka tu na kuya angalia yalivyo na kuyaacha. Wewe kama kijana ukiamua kupambana pambana.

Tunaendelea tuliopo ishia........
Maisha ndani ya IGONGE yakaendelea, kumbuka baada ya lile sekeseke la yule bubi likiwa limekwisha akaondoka, lakini moyoni nikabaki najiuliza uyu Bibi ameamua kutoa kauri hiyo pengine Kuna jambo atafanya, lakini Kwa kuwa na Mimi nilienda kujitafuta na nikielewa Changamoto kama hizo zinatokea nikasema Kwa Hali yoyote nitapambana nae sio kupiga bali nitamshinda Kwa njia njingine. Nikisema ivyo wakubwa mtaelewa, watato hawatanielewa. Basi ndugu zangu nikaendelea kuchapa kazi.
Kumbuka wakati huo nipo Kwa jamaa yangu Kasukari na yeye pale alipokuwa amekita kambi halikuwa eneo lake alipewa nyumba na kijana wa yule Mzee alienikodishia SHAMBA akae, maana yale maeneo ni kama wote walioko pale ni familia Moja ya yule Mzee. Yule Mzee alikuwa ameoa wanawake watatu na wote na wote alizaa nao, kwaiyo anawatoto wengi wa wanawake totauti tofauti na Jumla ya wototo wake wanafikia 35,Kwa wale wanawake walioachana na akaoa tena bi mdogo ambae anaishi nae sasa pia amezaa nae watoto wawili Jumla ya watoto 37 hayo ni maelezo ya yeye mwenyewe aliniambia. Kwaiyo vijana wake wote hao wanaishi humo , Kila kijana alimkatia eneo lake na wote wanakaa humo, na mabinti zake pia wengine wameolewa humo humo na wanaishi na waume zao humo.

Kumbuka maisha yakaendelea naamka alfajiri naenda shamba kusafisha mchana narudi Kwa Jamaa yangu Kasukari, lakini nikawaza mbona nitaangaika sana, maana kutoka Kwa kambi ya Kasukari kwenda shambani kwangu ilikuwa ni nusu saa tu unafika shambani kwangu lakini niliona kabisa mvua zikianza kuonyesha Nita fell kabisa, maana kule shambani hakukuwa na nyumba yoyote ni mashamba tu, kwaiyo nikawaza lazima nijenge camp yangu huko shambani. Kitu kingine kilichonifanya nipate Mawazo ya kujenga camp yangu, maana baadae nilikuja kuona tutakapo elekeza jamaa yangu Kasukari tutakosana maana kumbuka jamaa hakuwa na mke kwaiyo sometimes unatoka SHAMBA unanjaa unakuta jamaa amefunga geto na haujui aliko na anarudi time zimekwenda wakati huo wewe una njaa ya kufa mtu, akirudi ni story ndefu sana. Maana nilikuja kuelewa hakutaka kunipa funguo za geto, siunajua for the first time mtu kukuamini ni ngumu hadi akujue vizuri, kwaiyo Kwa Hali Ile niliona Malengo yangu hayata timia.
Kazi ya kusafisha SHAMBA ikamalizika, kumbuka hapo nilipiga kazi wiki mbili tu SHAMBA likawa kama kiwanja Cha Mpira, watu walikuwa hawanielewi kabisa, wengine wanasema anavuta bangi, lakini nikitu ambacho sijawi kutumia kabisa maishani yangu. Nikamaliza kusafisha na nikaamua kurudi tena mwanza kwenda kujipanga kikamilifu sasa na kununua Kila kitu ambacho kitafaa katika kilimo na maitaji yangu yote,na pia kwenda kumuona mkali wa tiba, kumbuka kilimo nacho kimeingiliwa, ni vita kama vita nyingine. Kumbuka tena vile vitisho vya yule bibi, kwamba tutaona kama utavuna kwenye hili shamba. Kumbuka wakati huo niliwai sana maana muda wa majira ya mvua ulikuwa Bado kabisa ilikuwa ni mwezi wa nane Jua linawaka sana.

Habarini za jioni wanajanvi, ni jioni nyingine tena baada ya shuruba za siku nzima, nimelejea tena tuendelee na mrejesho wangu. Lakini kuna watu humu wenyewe ni watu wa kuongea maneno ya kukatisha tamaa, ohhh mara uyu sio mkulima, mara uyu hakuna kitu.
Ngoja nikwambie ndugu yangu, kama humu tungefahamiana Kwa majina ungecheka sana, maana Kuna watu humu akitoa comment unaweza kudhani maisha ameyapatia kumbe nae bado anajitafuta na pengine bado anazungusha Cv na kulilia ajira, kumbe hajui kazi zipo lakini ajira hakuna.
Tunaendelea....... Nipo mwanza sasa baada ya kumaliza kusafishia SHAMBA na nikaona muda bado mrefu nikaamua kurudi mwanza kwaajiri ya kufanya kufanya manunuzi ya vitendea kazi lakini pia kwenda kumuona mtaalamu furani aweze kurekebisha mambo flani [emoji16],kumbuka unaingia vitani.
Basi tarehe za mwanzo wa mwezi wa tisa safari ikaanza kurudi KATAVI. Hapo mimefanya manunuzi ya Kila kitu kuanzia majembe, panga, solo pamp, madawa ya wadudu, mbegu za mahindi aina ya DK 719 TEMBO BABA LAO,dawa za magugu, maturubai kwaajili ya kambi, vyombo vya kupikia, dawa za aina mbalimbali kama Malaria, tumbo, dawa za vidonda, nyembe, sindano za viatu na nyuzi, sindano ya mkono,kumbuka kule ni shambani hakuna chereani, kwaiyo hata nguo ya kazi ikichanika nashona mwenyewe, au Farm boots imepasuka nashona mwenyewe like that wadau. Ndo maisha ya SHAMBA hayo.
Yani ni kwamba sikutaka kuwa napoteza muda kitu kidogo tu hadi niende MWESE NO4, kumbuka kule ni shambani ukiingia umeingia, maitaji kuyapata Yako mbali, Yani nilifungansha Kila kitu ambacho kingeitajika kwenye kambi yangu, kumbuka hapo nikifika ni kujenga kambi yangu kule shambani yani nikae kule shamba, maana nilifikiria mvua zikianza kunyesha ningesumbuka sana kuwa natoka kule kuja shambani pili kingine kilichonifanya kujenga kambi ni kitendo Cha Jamaa yangu Kasukari ninapotoka SHAMBA unakuta nae amekwenda shambai na tunapisha muda wa kurudi. Lakini kikubwa zaidi ni mtu ambae tulikuwa hatujazoena maana alihisi pengine ni wale vibaka wa Town kumbe Mimi Sina iyo tabia.

11.SAFARI YA KURUDI MPANDA KUTOKEA MWANZA HAWAMU YA PILI.
Basi ndugu zangu zafari ikaanza kutoka mwanza kwenda Mpanda, wakati wa kurudi nilipanda Bus ya Nyehunge Express, majira ya jioni tukaingia Mpanda, sasa nikafikiria nikisema niende Kwa Jamaa yangu yule wa hapo Town nitahangaika na mizigo kwenda kwake,maana kulikuwa ni mbali.Nilimpigia simu tu akaja pale stand tukasalimia nikampa zawadi ya dagaa wa mwanza, Yani jamaa yangu alishukuru sana.
Kumbuka nimefika jioni na magari ya kwenda MWESE NO4 hayakuwepo muda huo maana yake ni kwamba hadi kesho yake asubui, hivyo nilikesha pale stand na ndugu zangu wasukuma, Yani nyomi ya wasukuma wanahama kutoka mikoa mingine kuja Mpanda Yani ni vurugu tu Kila mahari.
Nilikesha hapo, hatimaye kukapambazuka salama. Kwakuwa Kuna vitu baadhi sikununua mwanza niliona tiaenda kununua kule, mfano misumari ya kujengea kambi, nyundo na vitu kama nyanya, vitunguu, mafuta ya maweze nk. Maana kule mafuta ya maweze yanatumika sana ukanda ule na pia yana Bei nafuu.
Basi mnamo majira ya saa3 asubui nikawa nimemaliza manunuzi yangu na nikachukua bajaji ya kwenda hadi kule Stand ya Mizengo pinda kwenye ofisi za Nyehunge Express nilipoacha mizigo yangu. Tulichukua na kuelekea stand kunakopaki magari madogo ya kuelekea vijijini, nilipandisha mizigo yangu na baada ya muda mchache gari ikaanza mwendo.
Labda niseme kwamba Yani nilifanya manunuzi ambayo Kuna vitu baadhi Hadi namaliza kilimo Kuna vitu nilikuwa navyo na niligawaia rafiki zangu kama vile Dotto Msukuma, Mfipa wa sumbawanga, ndugu yangu Kasukari na Mzee mwenye SHAMBA, hao nilio wataja utaona mbeleni ni jinsi gani waligusa maisha yangu njkaamua kuwapa baadhi ya vitu nilivyo bakiza kambini.

12.NIMEFIKA MWESE NO4 HAWAMU YA PILI TENA.
Baada ya kuwa nimefika mwese nilichukua pikipiki tukafunga mizigo kupeleka Kwa yule Jamaa niliefikia mara ya kwanza wakati namsubiri Jamaa yangu Kasukari kuja kunipokea, kama unakumbuka mwanzo siku nafika Mwese mara ya kwanza. Basi tukafika Kwa uyo jamaa nikamkuta, kwakweli pia ni poa sana. Baada ya kufungua mizigo nilitoa mfuko wenye dagaa kilo Moja na mafuta ya maweze Lita Moja na chumvi nikamkabidhi mke wake. Yani walifurai sana, sometimes unajiongeza Ili kujenga urafiki,sio unakaa kaa tu kama kama mzoga.Kumbuka wakati naanza safari ya kutoka kule Mpanda nilikuwa niwasiliana na Jamaa yangu Kasukari kwamba atakuja kunipokea na kunisaidia mizigo kushusha kule IGONGE na nilimwambia ningempa chochote na alikubali lakini kitu cha kushangaa nilipofika nikipiga simu haipatikani hapo imefika sa kumi na moja na nusu, alafu kumbuka kuelekea kule unapita msituni ingawa hakukuwa na wanyama wanaodhuru. Basi nikaona uyu jamaa pengine amekwama kuja hivyo nikapangua zile mizigo miepesi nikafunga na begi langu mgongoni na Toch Kali yenye mwanga safari ikaanza wakati huo Nina redio yangu nikipiga wimbo wa Rose mhando.... Woga ndo umaskini wako mwanangu.. malengo yako utakamilisha vipi we kijana... Kila kitu unasema uwezi uwezi.. kwani wengine waliweza vipi we kijana... Kutwa kucha unashindana na Jua, Jua likisogea na wewe unasogea.... Kivuri kikisogea na we we unasogea... haujui kupambanua nyakati we kija... Jifunze Kwa walio fanikiwa kijana..... Umejiloga mwenyewe ehheeeeeeee... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.
Hatimaye nikafika Kwa ndugu yangu Kasukari, nilikuta amefunga geto naona alikwenda pia shambani, maana alikuwa amelima maharage ya bondeni ambayo wanamwagilia kutumia mifereji kutoka kwenye mto. Basi muda si mrefu akawa amefika na akaanza kuniambia Mwamba!! Yani nilishindwa kuja nilikuwa napulizia sumu ya wadudu kwenye maharage pole sana Mwamba. Namimj hakuna shida, nikamwambia Jamaa yangu chukua mazaga humo upike maana Mimi nimechoka sana.Kumbuka baada ya muda wa wiki kadhaa mbeleni niliamia kambini kwangu na niliondoka na mizigo yangu na zile dagaa nilizo mpa ilikuwa ni mboga yake,hivyo nilimwambia hizo dagaa zake atunze tu maana yake ni kwamba tungekula dagaa zangu Hadi naondoka pale kwake nilikuwa na dagaa wengi sana.
Tulimaliza kula na kujiegesha , maana yake Ile sio kulala yani unaamka asubui mbavu zikiwa zinauma kinoma, kumbuka kitanda Cha miti ya mianzi na juu ni godoro la nyasi yani mwanaume unatakiwa ujikubali popote na kwalolote katika maisha.
Kukapambazuka salama lakini kumbuka Kuna mizigo zangu zilibaki kule kijijini, hivyo Kuna wajukuu wa yule Mzee Yani ni watoto wa vijana wa yule Mzee.Kwaiyo niliongea na baba yao nikachukuwa vijana wawili tukapandadisha kijijini. Nikisema kupandisha acha kushanga[emoji3064][emoji3064] ni msemo ambayo inatumika kule mashambani.Utasikia oya Mwanangu unapandisha kijijini? Na Mimi ndio!! jamaa ngoja nikuagize chumvi na kiberiti Kwa GAMA. Uyu Gama ni Mangi mmoja maarufu sana pale kjjijini Yani uwezi kwenda kwenye Duka lake ukakoswa kitu Yani hata pilipili utaipata inauzwa na Huduma zote za miamala ya kifedha Kijiji kizima hadi vijiji vya jirani wote ni Pale. Anauza Jumla na reja reja, yani anapiga pesa ni balaaa.
Basi ikabidi niwape pesa wale madogo tukapandisha kijijini, tulifika nikawapeleka kwanza mgahawani kunywa chai yani madogo walivyo rudi kwao walikwenda kusimulia makwao, maana chai ni kitu hadimu kule mashambani. Baada ya kumaliza kupata chai tulienda kuchukua mizigo na safari ya kurudi ikaanza, kabla ya hapo tulipotoka kupata chai tulikwenda Kwa uyo Mangi mwenye duka Ili kwamba niweze kuweka Salio la kutosha kwenye simu yangu iwe vyepesi kuwa nanunua muda wa maongezi juu Kwa juu maana kule hakuna vocha na pia niliweka Salio la M PESA Kwa kunilaisishia kuwa nalipia mtambo wangu wangu Solar kutoka kampuni x maana niliununua Kwa mkopo unalilipia kidogo kidogo. Niliuchukua Kwa ajiri ya Matumizi ya kambini kwangu, kuchaji simu na kupata mwanga. Kumbuka kule hakuna umeme.Safari ya kurudi shambani iliwadia na wale madogo Kila mtu akabeba Mzigo wake na tukafika salama Kwa jamaa yangu Kasukari.

13.KAZI YA KUANZA KUJENGA CAMP KULE SHAMBANI KWANGU.
Wadau baada ya kuwa tumefika na mizigo yetu na wale madogo, ilikuwa ni siku ya Mimi kuandaa vitu flani ambavyo nilipewa na mtaalamu wangu na sikutaka jamaa yangu ajue chochote kuhusu ilo ila niliambiwa Hadi nifanye ilo jambo kule shambani ndio nianze kazi Yani Kwa ufupi nisifanye chochote kule shambani hadi niakikishe SHAMBA limekuwa na walinzi wa Babu, nikisema ivyo wakubwa mnaelewa na kazi iyo ilitakiwa nifanye majira ya alfajiri sana Yani kabla ya watu kuamka napia utakiwi kuongea na mtu hata kama umekutana nae Kwa bahati mbaya.
Nashukuru zoezi nilimaliza na kazi ya ujenzi wa kambi ukaanza.
Siku iliyo fuata baada ya kumaliza lile zoezi nilienda SHAMBA nikiwa na panga, jembe na vifaa vingine kwaajiri ya kwenda kuchora ramani ni wapi nitaiweka kambi yangu na pia kuanza kukata miti na kuchimba mashimo na kusimika miti ya nguzo. Swala la miti haikuwa tatizo maana humo humo kwenye SHAMBA la Mzee kulikuwa na miti kwenye Yale mashamba ambayo hayajalimwa kwaiyo unajikatia tu. Hivyo baada ya kuchora ramani ya kambi yangu ni wapi itakaa nilianza survey ya kuzungukia miti mizuri ambayo ingefaa kama nguzo nilifanikiwa kupata miti mizuri na imara kwaiyo nilikata na kukusanya pamoja na kuanza kusomba kusogeza pale site ambapo nitajenga camp yangu.
Kwa siku iyo nilikamilisha kazi iyo ya kukata miti, maana haikuwa ni miti mingi ilikuwa kama ishirini hivi kwani ukubwa wa kambi yangu ilikuwa ni chumba na sebule lakini vidogo tu sio vikubwa sana, Pia nilimpatia kazi jamaa mmoja Mfipa wa sumbawanga kazi ya kunikatia MIANZI ambayo ningetumia kuzungushia pembeni na kupiga juu Kwa kutumia misumari.Mlio Kaa shambani mtaelewa miti ya mianzi. Kumbuka sikutumia kamba maana nilikuwa nime nunua misumari kilo mbili mchanganyiko kulingana na Kila kazi. Nilimaliza kukata miti na kusogeza na nikarudi magetoni kwenda kurekebisha msosi Ili kwamba saa tisa nirudi kuendelea na kazi ya kuchimba mashimo na kusimika nguzo.
Around saa tisa nilirudi shambani Ili kunza kuchimba mashimo na kuweka nguzo wakati huo yule Mfipa wa sumbawanga anakata mianzi na watoto wake wanasogeza pale site. Uyo jamaa nilimkubali na nilikuwa nampa kazi zangu nyingi maana alikuwa na familia kubwa ya watoto kwaiyo ukimpa kazi muda mchache anakukabidhi,yani alikuwa ni mtu poa sana maana na yeye ndo alikuwa ameamia pale akitokea sumbawanga. Hivyo hakuwa na sehemu ya kupata pesa na pia alikuwa Hana,maana yake ndio wakati alikuwa amefika na alikuwa ajalima mazao kwaiyo alikuwa akitegemea apate kazi ndio apate maitaji ya kuhudumia familia yake.Alipambana jioni iyo lakini akumaliza idadi ya mianzi niliyo itaka ilikuwa ni mingi sana Kwa sababu ingefanya kazi ya kuzungushia uzio kwenye kambi yangu. Sikutaka camp yangu ikae vibaya Yani nilitaka niwe ndani ya usalama ukizingatia kule ni maporini.
Siku iyo nilifunga kazi na kurudi nyumbani kwani Jua lilizama na Kazi ikaishia pale.

Asubui nitaendelea wadau ......Ngoja nilale.

Cookie
Comment No. 108, second para, nimeshindwa kui quote..!!
 
Back
Top Bottom