Mrejesho: Safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Mrejesho: Safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Mkuu we upo huko kijijini?
13.KAZI YA KUANZA KUJENGA CAMP KULE SHAMBANI KWANGU.
Wadau baada ya kuwa tumefika na mizigo yetu na wale madogo, ilikuwa ni siku ya Mimi kuandaa vitu flani ambavyo nilipewa na mtaalamu wangu na sikutaka jamaa yangu ajue chochote kuhusu ilo ila niliambiwa Hadi nifanye ilo jambo kule shambani ndio nianze kazi Yani Kwa ufupi nisifanye chochote kule shambani hadi niakikishe SHAMBA limekuwa na walinzi wa Babu, nikisema ivyo wakubwa mnaelewa na kazi iyo ilitakiwa nifanye majira ya alfajiri sana Yani kabla ya watu kuamka napia utakiwi kuongea na mtu hata kama umekutana nae Kwa bahati mbaya.
Nashukuru zoezi nilimaliza na kazi ya ujenzi wa kambi ukaanza.
Siku iliyo fuata baada ya kumaliza lile zoezi nilienda SHAMBA nikiwa na panga, jembe na vifaa vingine kwaajiri ya kwenda kuchora ramani ni wapi nitaiweka kambi yangu na pia kuanza kukata miti na kuchimba mashimo na kusimika miti ya nguzo. Swala la miti haikuwa tatizo maana humo humo kwenye SHAMBA la Mzee kulikuwa na miti kwenye Yale mashamba ambayo hayajalimwa kwaiyo unajikatia tu. Hivyo baada ya kuchora ramani ya kambi yangu ni wapi itakaa nilianza survey ya kuzungukia miti mizuri ambayo ingefaa kama nguzo nilifanikiwa kupata miti mizuri na imara kwaiyo nilikata na kukusanya pamoja na kuanza kusomba kusogeza pale site ambapo nitajenga camp yangu.
Kwa siku iyo nilikamilisha kazi iyo ya kukata miti, maana haikuwa ni miti mingi ilikuwa kama ishirini hivi kwani ukubwa wa kambi yangu ilikuwa ni chumba na sebule lakini vidogo tu sio vikubwa sana, Pia nilimpatia kazi jamaa mmoja Mfipa wa sumbawanga kazi ya kunikatia MIANZI ambayo ningetumia kuzungushia pembeni na kupiga juu Kwa kutumia misumari.Mlio Kaa shambani mtaelewa miti ya mianzi. Kumbuka sikutumia kamba maana nilikuwa nime nunua misumari kilo mbili mchanganyiko kulingana na Kila kazi. Nilimaliza kukata miti na kusogeza na nikarudi magetoni kwenda kurekebisha msosi Ili kwamba saa tisa nirudi kuendelea na kazi ya kuchimba mashimo na kusimika nguzo.
Around saa tisa nilirudi shambani Ili kunza kuchimba mashimo na kuweka nguzo wakati huo yule Mfipa wa sumbawanga anakata mianzi na watoto wake wanasogeza pale site. Uyo jamaa nilimkubali na nilikuwa nampa kazi zangu nyingi maana alikuwa na familia kubwa ya watoto kwaiyo ukimpa kazi muda mchache anakukabidhi,yani alikuwa ni mtu poa sana maana na yeye ndo alikuwa ameamia pale akitokea sumbawanga. Hivyo hakuwa na sehemu ya kupata pesa na pia alikuwa Hana,maana yake ndio wakati alikuwa amefika na alikuwa ajalima mazao kwaiyo alikuwa akitegemea apate kazi ndio apate maitaji ya kuhudumia familia yake.Alipambana jioni iyo lakini akumaliza idadi ya mianzi niliyo itaka ilikuwa ni mingi sana Kwa sababu ingefanya kazi ya kuzungushia uzio kwenye kambi yangu. Sikutaka camp yangu ikae vibaya Yani nilitaka niwe ndani ya usalama ukizingatia kule ni maporini.
Siku iyo nilifunga kazi na kurudi nyumbani kwani Jua lilizama na Kazi ikaishia pale.

Asubui nitaendelea wadau ......Ngoja nilale.
Jing'olongo.
 
Mzee baba Jifunafu

Umeupiga mwingi kwa kutuletea hamasa kwa vitendo

Nna swali moja tuu

Ulilima ekari 3 ukavuna gunia 41,
Mbona ni kidogo sana?

Changamoto ilikuwa nini
Changamoto ni kwamba, kumbuka sijatumia mbolea yoyote ndugu, kwaiyo ningekuwa na uwezo wa kuweka mbolea hakika ningepata mahindi mengi sana, Kama nilivyo elezea mwanzo mtaji wangu ulikuwa ni mdogo sana, hivyo ningeweka na gharama za mbolea ningekwama vitu vingine. Kwakile nilichokipata sisemi vibaya kwangu niliupiga mwingi.
 
Wakuu habari natumaini mu wazima wa afya njema na muendelezo wa sikuu hizi.
Nimelejea baada ya siku mbili tatu hizi kuwa kmy kulingana na harakati za hapa na pale.
Tunaendelea wakuu............

Maisha ndani ya shamba yakaendelea nukapuliza dawa ya magugu iyo ni palizi ya pili sasa,piga dawa ya viutalifu na mahindi yakawa yanaendelea vizuri kabisa yani shamba likawa linapendeza hadi wenyeji wakawa wanashangaa uyu jamaa amepanda mbegu gani?
Maisha yakaendelea yani sikutaka kupoteza muda kabisa.

Muda wa mavuno ukawadia,ukweli ni kwamba kwangu mimi nasema nilipata faida maana sikutumia mbolea yoyote,sikutumia gharama ya kulima shamba.Kwaiyo gharama niliyotumia ilukuwa ni kukodi shamba,palizi ya kwanza,madawa ya kuua wadudu na dawa za magugu.
Jumla nikipiga mahesabu laki 8 ilitumika hadi kumaliza kazi kabisa hadi kuvuna maana ndio pesa nilikuwa nimeitenga kwenye account.

Mavuno niliyopata zilikuwa gunia 42,nikatoa gunia tatu za msosi nyumbani nikauza 39,nilipata 2730000/= iyo ndio pesa niliokunja kwa kiwango changu.
Niliuza kwa bei ya70000 kwa gunia,yani sikutaka kutunza maana niliona nitaingia gharama tena za utunzaji na pengine bei ikapolomoka.

KITU MHIMU UNACHOTAKIWA KUELEWA.
Mimi sio mkulima mkubwa,na sukuwa na mataji mkubwa kwaiyo kwanafasi yangu mimi naona nilipata faida kulingana na kile kidogo nilicho wekeza.Ingiwa na jua wengine mtakuja na hesabu zenu hapa lakini ukweli ndo huo.
Nimeamua ku share experience yangu kwa sisi tusio na mitaji mikubwa ya kuanzia,hivyo ukiamua kuanza hata na kidogo kinakutoa.Kikubwa uende ukiwa na nia na kupenda kile unachofanya.

UZURI WA KILIMO NI KWAMBA.....
Vitu ambavyo nimeviona ni kwamba katika kilimo ukiamua kujiweka kutoka kimaisha ni haraka sana maana pesa ya kilimo unaikamata kwa pamoja na unafanya kile ulichokusudia.Sawa msoto unakuwepo lakini ukiipata inafanya lengo lako kwa wakati mmoja.Nina mifano mingi za jamaa zangu tulio anza nao kilimo wakati huo wao walipambana na wako katka viwango vikubwa.

ACHA KUSIKILIZA MANENO YA WATU.
Kijana mwenzangu acha kusikiliza maneno ya watu,kila mtu anashida zake,tambua shida zako na hakuna atakae kusaidia katika kujikomboa kutoka kwenye huu umasikini tulionao.Unapoamua kufanya maamuzi ya utafutaji jiangalie mwenyewe maana leo hao hao watakuponda haaa mara umeona maisha yamemshinda ameamua kwenda kulima,kikubwa angalia je uyu anaekusema anatoa mchango gani katika maisha yako? au akikusema utapungukiwa nini?.Katika kilimo hizi mitaji za milioni moja, mbili,tatu na kuendelea ukiamua kupambana ni msimu mmoja tu unaipata.
Mhimu,kama mtaji wa kianzio ni mdogo kama ulivyokuwa wangu,tafta kuwekeza maeneo ambayo bado mvua ni za kutosha,aridhi ina rutuba na pia mshamba yana bei nafuu.Hii itakusaidia kupunguza gharama kwa sisi tusio na mitaji mikubwa ya kuendesha kilimo.

VIJANA,KUKAA MJINI WAKATI HATUNA KAZI ZA KUELEWEKA NA KUOMBA OMBA NI UJINGA NA UJINGA MKUBWA SANA.
Ndugu yangu ebu tuambizane tu ukweli sio kwamba natukana ndio hali alisi kabisa,hivi unataka kuniambia kwa kufanya kazi kama hizi tutafikia malengo yetu au kutoboa maisha? Siku moja nimefika stand ya mabasi Nyamuhongoro hapa mjini yani hadi unaskitika ingawa na wewe unashida yani ushanga kuona umati wa vijana hadi wazee wakiwa katika foleni ya kudandia abiria apeleke kwenye bus apate chochote yani hadi huruma.Unataka kuniambia hata kama kwa siku utapata 20000,kiuhalisia ni pesa tu itaishia kulipa kodi ya chumba,kula na nauli za dalala.Hata kwenye uwezo wa kununua debe la mahindi ukaweka ndani uwezo huo haupo,zaidi ya kwenda kupima robo kilo au nusu kwa Mangi.
Mjini tutaweza kukaa lakini kwa akili kubwa,msimu unaenda unalima mazao yako,meingine chakula mengine unauza kufanyia maendeleo yako.Kati ya vitu katika familia vinavyochukua bajeti kubwa ni chakula,tukiweza kuthibiti hapa maisha unatoboa.Ebu tujiwekeze mashambani ndugu zangu,kuna wakati hata unatembea mjini unabaki kujiuliza hivi mimi niko kundi gani? au ninasindikiza wengine tu.
Usione watu wanatembelea magari makali,wengi wanamashamba uko vijijini,lakini mimi na wewe kutwa ni kupinga tu ohhh kilimo ni cha masikini ohhh mara kilimo hakina faida.Aya ngoja tuendeele kulaumu serikali kwamba haitoi ajira.
CHANGAMOTO KATIKA KILIMO ZIPO.
Usiende katika kilimo ukiamini kupata tu,tambua kilimo ni kama kazi nyingine au biashara zingine lakini kikubwa ni kutokata tamaa na pia upende kile unachokifanya.
Ukifanya kazi ya kilimo kwa kuipenda unaweza kuchelewa lakini lazma ufanikiwe siku moja.Kila kazi yaitaji uvumilivu.Hata waliofanikiwa katika kilimo walijitoa.
Epuka sana katika kilimo habari ya wewe kukaa uko ukiamini kuna mtu umemuweka anasimamia,hakikisaha umepata mtu sahihi na atakae fanya kazi hile kama yake,lakini eti wewe umekaa mjini ukiamini kazi inaendelea kwa kupiga simu tu.
Kilimo kinaitaji Physical supervision,maana yake ni kwamba muda mwingi unatumia kuzunguka shambani na kukagua namna mazao yanavyo endelea na changamoto zipi zinakabili mazao yako.

KITU NILICHOJIFUNZA NA KUJIONEA.
Katika wilaya Tanganyika Mkoa wa Katavi ni wilaya ambayo bado ina maeneo makubwa sana ya uwekezaji katika kilimo na ufugaji,utake kufuga Nyuki sawa,ufuge nguruwe sawa,mbuzi sawa yani ufugaji wowote unakubalika.Pia kuna mito mikubwa ambayo hata ukiamua kufanya kilimo cha umwagiliaji inawezekana.
Ninataka sasa kurudisha majeshi kijijini maana haiwezekani kukaa mjini wakati maisha yanaendelea kunichapa.Yani nataka nikawekeze maisha yangu huko,siku nikirudi mjini lazima niwe na kitu cha kuonekana kwamba nimefanya nini.

Ndugu zangu niwatakie maandalizi mema ya sikukuu ya Mwaka mpya,lakini pia tukikumbuka je mwaka unaonza una tumejipanga vipi kuhakikisha tunafikia malengo yetu.Tusikalili tu maisha ya sehemu moja,ukiona sehemu uliopo mambo hayaendi badili upepo nenda mahali pengine pambana.
Kama una swali lolote karibu uniulize nitakujibu bila hiyana yoyote.

Mafundi mitambo wa Jamiiforums mnisaidie kupanga huu uzi kwa mtiririko.
Wakondya bhwafuu.
 
Back
Top Bottom