Doji MD
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 1,770
- 3,552
SSa
Sahii kama huku nilipo..vijijiji ukienda unakuta hekari inauzwa elfu 70 mpaka laki,..ukijiwekeza mbona kutoboa nirahisiMkuu kipindi nasoma hii reply yako kuna muda picha ilikuwa inanijia kichwani vile ulikuwa unaelezea. Sio siri kijijini ukiwa muaminifu na ukaishi poa na kila mtu hakika utaishi maisha poa sanaaaa.
Nimewahi shuhudia mzee mmoja alikuwa peace sana kwa kila mtu yule mzee watu walimpenda sana na alikuwa maarufu sana kwa kile alikuwa anafanya mpaka vitoto vidogo ni vinamfahamu kwa namna alivyo kuwa.
Ulicho kiandika ni ukweli mtupu, ujue kuishi maisha mazuri sio lazima ukae mjini. Ata kijijini unaweza ishi maisha uyatakayo muhimu ni kutumia akili uliyo pewa. Hongera sana una kitu na fikra nzuri sana, nikwambie tu yote yanawezekana muhimu ni kujitambua tu.
Hii Tanzania kwa kijana unae jitambua, nikisema kujitambua namanisha uko vizuri kichwani na mwenye ndoto na uchu wa kutaka mafanikio. Achana na hawa mabishoo, namanisha mwanaume kweli na una kiasi cha million 1.5 tafuta kijiji chenye rutuba nzuri kwa kilimo huko ndani ndani kisha piga kambi yako ndani ya miaka mitatu utakuja kuleta ushuhuda hapa.
Shida asilimia kubwa ya vijana wanapenda maisha ya kufumba na kufumbua matokeo yake ndio maana leo hii tuna wimbi kubwa la vijana wavivu na wa hovyo kabisa. Hii Tanzania ukiwa makini huko vijijini kutoboa ni kugusa tu na umaarufu, vijana badilikeni maisha hayapo kukusubili kila siku zinasogea. Leo una miaka kadhaa mwaka ujao ni miaka kadhaa pia na kila siku uko pale pale, badilika sasa na uchukue maamuzi sahihi bado hujachelewa. Anaekupenda zaidi ni wewe mwenyewe, tubadilike vijana.