Mrejesho wa yale niliyosema kuhusu kijana wa hovyo Majaliwa aliyeidanganya nchi na wasomi wake

Mrejesho wa yale niliyosema kuhusu kijana wa hovyo Majaliwa aliyeidanganya nchi na wasomi wake

Huyo jamaa uliyemhoji hana tofauti na shabani kaoneka, roho ilimuuma kuwa ameshinda ila hapati endorsement za maaana wakati aliyempiga mashavu kibao kila siku interview.

Bahati nzuri nnachopenda watanzania wenzangu, wakimshikilia mtu hata umsagie kunguni buku na kuleta shujaa wako hawageuzi maneno wataendelea kumpa mashavu aliyetrend first.

Tupunguze roho mbaya.
 
INASIKITISHA SANA TENA SANA 😭

WALIOOKOLEWA WAKANA KUSAIDIWA NA MAJALIWA, WADAI WALITUMIA JUHUDI ZAO KUJIOKOA.

Furaha ya Majaliwa Shujaa aliyeokoa watu kwe ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Bukoba mkoani Kagera huenda ikageuka huzuni baada ya abiria waliookolewa kwenye ajali hiyo kudai walitumia juhudi zao wenyewe kufungua mlango na kisha kutoka.

Akizungumza mmoja wa abiria hao amesema yeye ndiye angeweza kuwa kinara wa tukio hilo kwani baada ya ndege kutua kwenye maji, yeye na muhudumu mmoja wa ndege hiyo waling'ang'ana kufanya jitihada za kufungua mlango wakati huo mitambo ya umeme ilikuwa imezima na mlango ulikuwa umejilock.

"Baada ya ndege kutua kwenye maji nilianza kutapatapa kutafuta mlango wa kutokea, haikuwa rahisi lakini kwakuwa mimi nilikuwa viti vya nyuma nilijitahidi kutafuta namna ya kutokea, tulikuwa tunaenda kufa, nikawambia wenzangu "kwahiyo tunakufa huku tunajiona" hapo maji yalikuwa yamejaa, lakini baadae niliona mlango unajifungua kidogo baada ya muhudumu wa ndege kuuchokonoa kwa chini ndipo nilipotumia upenyo ule kuusukuma mlango nikatoka nje"

Abiria huyo ameongeza kwa kusema "baada ya mimi kutoka nilianza kuwaokoa wenzangu, na kila aliyekuwa anatoka alikuwa anakaa juu ya ndege maana maboti ya wavuvi yalikuwa bado kufika, nilijawa na ujasiri mkubwa ingawa hali yangu ilikuwa mbaya, nikawa nawavuta watu kuwatoa nje akiwemo mama mmoja na mwanae ambao pia niliwaokoa mimi nikisaidiana na mchina, baadae watu waliisha kwenye ndege nikajua wote wametoka ndipo wavuvi walipoanza kuja kutuchukua kutupeleka hospitali";- ameeleza mmoja wa waliookolewa.
Ushujaa wa majaliwa ni kuwabeba abiria kutoka kwenye maji kuwapeleka nchi kavu na hakuwa peke yake alikua na wavuvi wenzie,pia mlango hajafungua yeye kama ilivyodaiwa awali kuwa amefungua yeye
 
Stories nyiiiiingi. Mwingine anasema yeye afungua mlango akakutana na kijana mdogo akamwomba aingie kwenye ndege akusanye mabegi, mwingine anasema alipitia bawa lilipokatikia. Kama umeme ulikata na lock inategemea umeme na Majaliwa anasema aligonga kwa kasia kuondoa lock na mwandishi anasema mhudumu alichokonoa mlango ukafunguka na kuna abiria anasema kuna kijana nilimwomba aingie ndani kuokoa mabegi, na majaliwa anasema nikaita wenzangu wakanipatia kamba niende kuifunga sehemu ili tuvute ndege na kwamba kuna waokoaji walipoteza uhai wakijaribu kufanya uokoaji. Kwa nini tunapenda kupoteza hii picha ya Majaliwa na wenzake waliozama hadi ndani hadi mmoja wapo akapoteza maisha?
Kwa hiyo nawe unaamini kabisa hayo maelezo ya mtu kusema alimuomba kijana kuingia ndani ya ndege ili kuokoa mabegi?

Kwa hiyo Majaliwa akaokoa mpaka mabegi ya abiria?

Bongo sihami ng'oo.
 
huo ni uzushi wenye lengo la kuficha uzembe wa wafanyakazi wa Uwanja wa ndege Bukoba.
vyovyote itakavyo kuwa kuna uzembe wa hali ya juu ambao haupaswi kufumbiwa macho.

Majaliwa na kundi lake la uvuvi walijitahidi kufanya walicho kifanya lkn wafanyakazi wa Uwanja wa ndege Bukoba walibaki kushangaa!!

hata kama mlango ulifunguliwa na abiria lakini pia majaliwa na wavuvi wenzake walihangaika kujaribu kufungua, huenda jitihada za pande mbili zilifanikisha mlango kufunguka. wote walifanya jitihada abiria na kundi la Majaliwa.

Ushujaa wa Majaliwa unabaki palepale, kwani alithubutu kufanya alicho kifanya kuokoa maisha ya wengine.., ila ushujaa wake umekuwa mwiba mkali kwa wenye dhamana walio chelewa kufika kwenye uokoaji, nadhani hao wanatamani hata majaliwa angekufa kabisaa!!
 
Hao abiria wapumbavu, na kuna uwezekano ni mashoga.
Kila mmoja anajifanya yeye ndiye alikuwa kinara wa uokoaji.
Sisi tunamjua Majaliwa
 
huo ni uzushi wenye lengo la kuficha uzembe wa wafanyakazi wa Uwanja wa ndege Bukoba.
vyovyote itakavyo kuwa kuna uzembe wa hali ya juu ambao haupaswi kufumbiwa macho.

Majaliwa na kundi lake la uvuvi walijitahidi kufanya walicho kifanya lkn wafanyakazi wa Uwanja wa ndege Bukoba walibaki kushangaa!!
Kweli kabisa aisee
 
Hao abiria wapumbavu, na kuna uwezekano ni mashoga.
Kila mmoja anajifanya yeye ndiye alikuwa kinara wa uokoaji.
Sisi tunamjua Majaliwa
Hivi una habari kuwa, Majaliwa naye alikuwa miongoni mwa watu waliookolewa?
Majaliwa naye anawashukuru watu asiowajua kwa kuweza kumuokoa!
 
Ni sawa walitoka nje ya ndege kwa juhudi zao, na vipi huko nchi kavu walifikaje? Bila msaada wa kina Majaliwa wangekaa huko kwenye mabawa ya ndege mpk wangezamia hapo hapo.
 
Hao waliokuwa abiria bado wamepagawa, tuwape muda tu.

Hii ishu sio yakushabikia, itavunja watu moyo wa kuokoa watu ajali zikitokea.

Inakuwa kama ile kukitokea ajali ukajipendekeza kumsaidia mhanga polisi wanakung'ang'ania wewe hadi ukome.

Tuangalie madhara ya hili tunalolichochea.

Majaliwa kajitahidi kaonesha utu, bado watu wajinga hawataki, alafu unakuta wanaenda ibadani kutoa shukrani kwa kunusurika kifo.

Bongo nyoso!.
 
Majaliwa ilikuwa ni plan ya damage control.

Lasivyo angejiuzulu mtu
Bongo mtu ajiuzulu kwa jambo lisilomgusa moja kwa moja?? Haiwezekani

Hakukuwa na sababu ya kutengeneza damage control ili kuepusha kujiuzulu. Hiyo ndege hata kama muongozo angekuwa ni waziri wa ujenzi asingeweza kujiuzulu na hatungekuwa na cha kumfanya, sembuse kwa mazingira hayo ya ajali ndio itengenezwe damage control kuepusha mtu kujiuzulu!!!
 
Tutaongea mengi sana kuhusu ile ajali. Lakini ndio imeshatoka hiyo!
Waliotakiwa kuwajibika/kuwajibishwa kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wao ili kuzuia ajali isitokee au kuokoa abiria wote waliokuwamo kwenye ndege bado wanadunda.
"No body cares". Inasikitisha sana.
 
INASIKITISHA SANA TENA SANA 😭

WALIOOKOLEWA WAKANA KUSAIDIWA NA MAJALIWA, WADAI WALITUMIA JUHUDI ZAO KUJIOKOA.

Furaha ya Majaliwa Shujaa aliyeokoa watu kwe ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Bukoba mkoani Kagera huenda ikageuka huzuni baada ya abiria waliookolewa kwenye ajali hiyo kudai walitumia juhudi zao wenyewe kufungua mlango na kisha kutoka.

Akizungumza mmoja wa abiria hao amesema yeye ndiye angeweza kuwa kinara wa tukio hilo kwani baada ya ndege kutua kwenye maji, yeye na muhudumu mmoja wa ndege hiyo waling'ang'ana kufanya jitihada za kufungua mlango wakati huo mitambo ya umeme ilikuwa imezima na mlango ulikuwa umejilock.

"Baada ya ndege kutua kwenye maji nilianza kutapatapa kutafuta mlango wa kutokea, haikuwa rahisi lakini kwakuwa mimi nilikuwa viti vya nyuma nilijitahidi kutafuta namna ya kutokea, tulikuwa tunaenda kufa, nikawambia wenzangu "kwahiyo tunakufa huku tunajiona" hapo maji yalikuwa yamejaa, lakini baadae niliona mlango unajifungua kidogo baada ya muhudumu wa ndege kuuchokonoa kwa chini ndipo nilipotumia upenyo ule kuusukuma mlango nikatoka nje"

Abiria huyo ameongeza kwa kusema "baada ya mimi kutoka nilianza kuwaokoa wenzangu, na kila aliyekuwa anatoka alikuwa anakaa juu ya ndege maana maboti ya wavuvi yalikuwa bado kufika, nilijawa na ujasiri mkubwa ingawa hali yangu ilikuwa mbaya, nikawa nawavuta watu kuwatoa nje akiwemo mama mmoja na mwanae ambao pia niliwaokoa mimi nikisaidiana na mchina, baadae watu waliisha kwenye ndege nikajua wote wametoka ndipo wavuvi walipoanza kuja kutuchukua kutupeleka hospitali";- ameeleza mmoja wa waliookolewa.
Una akili kubwa sana; naomba msamaha kwa dislike ambayo niliwahi kukupa
 
Back
Top Bottom