Mrema: Kikwete aendelee kuongoza Tanzania

Mrema: Kikwete aendelee kuongoza Tanzania

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,905
Reaction score
4,054
Mrema ataka JK aendelee na urais Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema amesema hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiacha kuongeza nchi kwa muda ili akamilishe mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja na Daftari la Kudumu la Wapigakura.

======================================

"Simfanyii mtu kampeni, ninachosema ni kwamba, mambo hayajakamilika na tunataka yakamilike na michakato yote aliyeianzisha ni Rais Kikwete, ni vyema akaimaliza," Augustino Mrema

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema amesema hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiachwa kuongeza nchi kwa muda ili akamilishe mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja na Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Hivi karibuni viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), walidai kuwa Serikali na Tume ya Uchaguzi (NEC) inachelewesha uboreshaji wa Daftari la Wapigakura kwa lengo la kutaka kumwongezea Rais Kikwete muda wa kukaa Ikulu.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema ni miezi mitatu imebaki kabla ya kampeni za uchaguzi, lakini mpaka sasa ratiba, majimbo yaliyogawanywa, watumishi wala vituo vya uchaguzi bado haviwekwa bayana na wala haifahamiki kazi ya uandikishaji katika Daftari la Wapigakura halijakamilika katika mikoa miwili.

"Hiyo ni hatari sana kwa Taifa. Tunaionya NEC isijaribu kufanya mbinu zitakazosababisha kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu," alisema Mbowe.

Akizungumza na gazti hili jana, Mrema alisema yeye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutoa wazo la kutaka Rais Kikwete aongezewe muda zaidi wa kukaa Ikulu kwa kuwa kuna mambo mengi ambayo ni ya muhimu kwa Taifa yanayotakiwa kukamilika kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Mrema alisema alitoa maoni hayo mwaka jana wakati viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) walipokutana na Rais Kikwete mjini Dodoma, lakini alishangaa kuona viongozi wengine wakipinga wazo hilo.

"Nilitoa ushauri Rais Kikwete akiwepo. Nilisema tusogeze Uchaguzi Mkuu mbele kwa miaka miwili ili atuachie nchi ikiwa salama, lakini wapinzani wamejiandaa kuingia Ikulu waliniona mimi kama bundi," alisema Mrema.

Aliongeza kuwa hata Rais Kikwete hakuonekana kufurahishwa na hali hiyo iliyojitokeza baada ya kauli yake na kwamba, hivi sasa amebaini kuwa kiongozi huyo wa nchi hataki kuongezewa hata siku moja ya kuendelea kukaa Ikulu.

"Sema kwa sababu wenzangu wamejiandaa kuingia Ikulu mwaka huu, wameshawaandaa hata wake zao kuwa ‘ma-first lady', lakini ukweli ni kwamba hata Katiba Inayopendekezwa ikipitishwa lazima kuwe na muda wa mpito.

"Simfanyii mtu kampeni, ninachosema ni kwamba, mambo hayajakamilika na tunataka yakamilike na michakato yote aliyeianzisha ni Rais Kikwete, ni vyema akaimaliza," alisema Mrema.

Akihutubia kwenye sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani jijini Mwanza juzi, Rais Kikwete alisema hana mpango wa kuongeza muda kama baadhi ya wanasiasa wanavyodai.

"Nawashangaa wanaodai kuwa Serikali ina mpango wa kuongeza muda wa urais, sina mpango wa kufanya hivyo, tarehe imepangwa na uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa Katiba," alisema Rais Kikwete
.

Chanzo: Mwananchi
 
Kumbe kuzeeka ni kuchanganyikiwa! Loh! Ni Mrema yupi jamani? Ni yule mzee wa kiraracha au? Yoote hayo ni ili JK ampe kiinua mgongo cha unaibu waziri mkuu?? Ama kweli, pesa yaweza kukufanya ukamkataa mamako.
Mwambiye hata JK akiibadili katiba. Oktoba ni karibu mno. Apishe jimbo la vunjo, tumekaa mda mrefu mno tukiongozwa na taayahiraaaaaa
 
Hivi nani anajua ugonjwa wa huyu mti plz
 
Ili Mrema naye aendelee kuwa mbunge wa vunjo, maana anajua bunge likivunjwa tu, Mrema hawezi kamwe kurudi bungeni labda kupitia viti maalum kama vitaendelea kuwepo.
 
Mrema ataka JK aendelee na urais
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour
Party (TLP), Augustino Mrema amesema
hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiachwa
kuongeza nchi kwa muda ili akamilishe
mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja
na Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Anazeeka vibaya huyu mzee bora akalime kahawa huko Vunjo
 
Kumbe kuzeeka ni kuchanganyikiwa! Loh! Ni Mrema yupi jamani? Ni yule mzee wa kiraracha au? Yoote hayo ni ili JK ampe kiinua mgongo cha unaibu waziri mkuu?? Ama kweli, pesa yaweza kukufanya ukamkataa mamako.
Mwambiye hata JK akiibadili katiba. Oktoba ni karibu mno. Apishe jimbo la vunjo, tumekaa mda mrefu mno tukiongozwa na taayahiraaaaaa

mtu mzima dawa mrema umenena mzee jk aendelee tu raha tupu
 
Sijui mrema amekula maharage ya wapi mpaka amevimbiwa na anaharisha tu
 
Kumbe kuzeeka ni kuchanganyikiwa! Loh! Ni Mrema yupi jamani? Ni yule mzee wa kiraracha au? Yoote hayo ni ili JK ampe kiinua mgongo cha unaibu waziri mkuu?? Ama kweli, pesa yaweza kukufanya ukamkataa mamako.
Mwambiye hata JK akiibadili katiba. Oktoba ni karibu mno. Apishe jimbo la vunjo, tumekaa mda mrefu mno tukiongozwa na taayahiraaaaaa

Huo msitari wa kwanza ufute kwani sio wazee wote wako kama Mrema. Huyo shida yake ni kufilisika kisiasa na wala sio uzee.
 
Kumbe kuzeeka ni kuchanganyikiwa! Loh! Ni Mrema yupi jamani? Ni yule mzee wa kiraracha au? Yoote hayo ni ili JK ampe kiinua mgongo cha unaibu waziri mkuu?? Ama kweli, pesa yaweza kukufanya ukamkataa mamako.
Mwambiye hata JK akiibadili katiba. Oktoba ni karibu mno. Apishe jimbo la vunjo, tumekaa mda mrefu mno tukiongozwa na taayahiraaaaaa
Omba radhi ,hajazeeka ki hivyo anaumwa na kale kaugonjwa ka siku hizi kanatafuna ubongo
 
Mrema ataka JK aendelee na urais
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour
Party (TLP), Augustino Mrema amesema
hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiachwa
kuongeza nchi kwa muda ili akamilishe
mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja
na Daftari la Kudumu la Wapigakura.

Punda wa kisiasa huyo.
 
Back
Top Bottom