Mrema: Kikwete aendelee kuongoza Tanzania

Mrema: Kikwete aendelee kuongoza Tanzania

Kiukweli namkubali Dr Slaa...ila kinachonifanya nimyime kurayangu ni huyo "the so called first lady to be"...comments zake facebook zinanipa mashaka sana na uwezowake...kwa capacity ya boyfriendwake, nilishauri sana kuwe na watu wanaopitia hizo post kabla ya kuwa released!

VP issue ya kagenzi imeishia wsp
 
Tuna bahati mwaka 1995 hatukumchagua kuingia ikulu, maana tusingeweza kumtoa tena kwa kura! Utamjua tu dikteta kwa vitendo na maneno yake! Asante baba wa taifa kwa kutuokoa na balaa hili.

Uenyekiti wa TLP anasema jeneza ndio litamtoa
 
Sasa hapo kuna mpinzani,si arudi tu CCM ,maana ameshindwa kujificha kabisa,ameona tu alipe fadhira waziwazi
 
Kwanza hata kipengele cha ukomo wa madaraka tukitoe maana nchi bado changa,JK aendelee tu mbona ndani ya chama chetu pendwa Chadema tuliona kichanga tukaona tutoe kwanza mambo ya demokrasia.CHADEMA na DEMOKRASIA ni kama MBOWE na ELIMU(mbali mbali).Chadema oyeeee......

Una Mimba ya Mbowe wewe sio Bure
 
Mrema ataka JK aendelee na urais Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema amesema hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiacha kuongeza nchi kwa muda ili akamilishe mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja na Daftari la Kudumu la Wapigakura.

======================================

Mrema hana habari kuwa JK alishasema kuwa amechoka na anatamani muda wake wa urais umalizike?!

Kama hali ndiyo hiyo, akiongezewa muda tunategemea afanye kazi kwa ufanisi wa kuridhisha?!

Mrema anajipendekeza tu kwa JK, kwa sababu anazozijuamwenyewe!
 
Huyu kiumbe wala si wa kumjadili tena,hakuna mtu humo ni kasha tu hilo...!!
 
Hapa Sasa Naanza Kulia Na Babu Wa Liliondo, Huyu Mzee Alidai Amepona Sasa Mbona Kimemludia?
 
Uenyekiti wa TLP anasema jeneza ndio litamtoa
Ukimsikiliza hata anavyo lalamina kuhusu ubunge jimboni kwake kuingiliwa, utajua kujimilikisha ni yaleyale ya kujimilikisha. Labda anadamu ya kimangi Mangi.
 
Mkuu Mbaga Jr nimeamini maneno yako. Uzi wenyewe ni huu?

Sema mzee Mrema kuna muda alitukosea sana 😁
Sasa pia kuna video za wabunge wa ccm wanasema aongezewe muda, nmeingia YouTube sijaiona.

Ila ndo hvy, za JPM zipo nyingi kutokana na aina ya utawala wake ulivyokuwa tofauti na Kikwete ndo mana hapakuwa na kelele nyingi.
 
Back
Top Bottom