Mrema: Kikwete aendelee kuongoza Tanzania

Mrema: Kikwete aendelee kuongoza Tanzania

Kwanza hata kipengele cha ukomo wa madaraka tukitoe maana nchi bado changa,JK aendelee tu mbona ndani ya chama chetu pendwa Chadema tuliona kichanga tukaona tutoe kwanza mambo ya demokrasia.CHADEMA na DEMOKRASIA ni kama MBOWE na ELIMU(mbali mbali).Chadema oyeeee......
Hivi weww upo ACT- YUDa ama CCM- Magamba maana kote naona unaunga mkono! Mna taabu kweli safari hii Maccm.
 
Mzee MREMA watanzania tunakuheshimu lakini kauli zako za hivi karibuni zinathibitisha UCHOVU wako kisiasa swali kwako KATIBA inasema RAIS aongezewe muda ili akamilishe katiba pendekezwa?au katiba ya TLP? Mzee nadhani ungerudi CCM tu
 
Ahahhaa nikikumbuka ile siku anahojiwa ITV kipindi cha Mzalendo yeye na mwenzake FAHMI DOVUTWA,Mrema alikuwa analalamika UKAWA wanataka kumtoa VUNJO na wanamsingizia kwamba ana HIV ikimlazimu mpaka kutoa cheti chake cha hospital kuthibitisha kwamba hana ukimwi.

Kikwete ndie anamlinda huyu mzee,sasa anajua kikwete akitoka tu madarakani na yeye Vunjo anaiaga!UKAWA muoneeni huruma huyu mzee na kisukari chake mtamuua na Pressure
 
Kutokana na kuwa na mlengo mmoja Mi nashaur ACT -Yuda, TLP na UDP waunde umoja wao wa PRO - CCM itawasaidia kutoa misimamo yao kama UKAWA wanavyofanya
 
Hivi Slaa akiwa rais nani atakuwa first lady, maana hajaoa bado yuko kwenye uchumba
 
Uzee una style nyingi jamani! huyu anaweza kuiona 6 akazani 9 kumbe yeye ndie kainama!
 
JK aongezewe miaka mitano mingine, Watanzania bado tunampenda sana
 
Ili Mrema naye aendelee kuwa mbunge wa vunjo, maana anajua bunge likivunjwa tu, Mrema hawezi kamwe kurudi bungeni labda kupitia viti maalum kama vitaendelea kuwepo.

Atabadilishana na James Mbatia. Mrema awe wa kuteuliwa na Mbatia awe wa jimbo!
 
Kikwete usikubali kabisa, ukiisha muda wako ondoka waachie wagalatia waendelee kuiba wapendavyo.
 
System ikitaka ataongezewa tu, labda waone haya kuingiza nchi ktk dhiki ya kihistoria.

Kikwete usikubali kabisa, ukiisha muda wako ondoka waachie wagalatia waendelee kuiba wapendavyo.
 
Hivi Slaa akiwa rais nani atakuwa first lady, maana hajaoa bado yuko kwenye uchumba

ahaha hilo nalo neno!!labda anajua hawezi kushinda,tukisema Tanzania hakuna Upinzani wa kweli watu wanakutukana,watu wamekalia Ruzuku tu.
 
.....Ili aendelee kuingamiza nchi yetu na Serikali yake dhalimu kwa kuongeza deni la Taifa na kuwa na sera muflisi ambazo zinachangia kushuka kwa thamani ya shilingi kwa kasi ya kutisha.

Ili aendelee kumpeleka India kwa matibabu! Njaa noma.
 
ahaha hilo nalo neno!!labda anajua hawezi kushinda,tukisema Tanzania hakuna Upinzani wa kweli watu wanakutukana,watu wamekalia Ruzuku tu.

Mchumba wake sijui ataitwa jina gani
 
Back
Top Bottom