Mrisho Gambo atenguliwa Ukuu wa Mkoa wa Arusha

Mrisho Gambo atenguliwa Ukuu wa Mkoa wa Arusha

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
UTEUZI WA RC ARUSHA NA DC ARUSHA WATENGULIA

Rais Magufuli, leo ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta

Pia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro na nafasi yake imechukuliwa na Kenan Kihongosi wa UVCCM Iringa

Aidha, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni na kumteua Dkt. John Pima kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri

#JFLeo #Magufuli
photo_2020-06-19_20-31-28.jpg


Soma pia:

1) Arusha: RC Gambo aibua sintofahamu Soko la Samunge, abeza taarifa ya DC na Mkurugenzi

2) Nini tatizo la RC Mrisho Gambo na wasaidizi wake?

3) Ugomvi baina ya RC Gambo na Mkurugenzi wa Jiji Arusha lashika kasi

4) RC Gambo aumbuka vijana wa CCM Arusha wamshambulia mitandaoni, aamua “ku left “

5) Kauli yake baada ya kilichotokea hapo #4: Mrisho Gambo: UVCCM kumejaa vijana wanafiki ambao wakizeeka watakuwa Wachawi!

6) Ntibenda: Kama kuondolewa kwangu kama RC Arusha kuna mkono wa mtu; Mungu atalipa

7) Oktoba 2016 iliwahi kuandikwa: Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, akanusha uvumi wa kutenguliwa kwa Gambo
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha atenguliwa. Juzi kati Mrisho alienda Dar kumuomba Makonda amuombee msamaha kwa Magufuli lakini akakwama. Waliongozana kwenye kikao cha UVCCM pale Mnazi mmoja akajifanya kumsifia Magufuli.. Yote yameshindikana.

TAKUKURU walipoenda Arusha nikasema kuna watu wanaondoka.

Nmekumbuka Maneno ya Godbless Lema. Hakika Mungu ndo anapanga kesho yetu.

Nomba wafikishwe Mahakamani pia. Hii aione DPP

Mbunge wa Arusha G.Lema na Mke wake wafikishwa mahakamani leo

Taarifa kwa umma: Matumizi mabaya ya madaraka ya Mrisho Gambo, Arusha
IMG_20200613_115027_996.jpg
 
Wamepewa nafasi ya kugombea ubunge majimboni. Tegemea tengua nyingi sana msimu huu. Cha msingi vaa jezi za ccm uvune rushwa. Jamaa yangu mpaka sasa kashajipatia laki kadhaa za rushwa kwenye kura za maoni. Na kuna laki kadhaa zingine zinamsubiria bado. Yajayo yanatajirisha.
 
Gambo juzi kaacha Mkoa wake kaja Dsm kwa UVCCM na Makonda. Katibu Mwenezi wake kaenda Arusha kasema Arusha CCM wanagombana sbb ya kutaka ubunge.

Huyu Kihongosi ni Mkimbiza Mwenge, lakini ndiye siku kadhaa zilizopita alitoa kauli ya vitisho dhidi ya Wapinzani. Alisikika akisema vijana wamteketeze Zitto.

Hii team inaenda ku-deal na Lema,Usalama wa Chama umejiridhisha katika majimbo magumu ya Upinzani,Arusha ni namba moja.

Unaweza kumpa mtu offer ya chakula lakini kumchagulia nini cha kula baada ya offer ni kinyume cha offer uliokusudia. Acheni watu waamue
 
Back
Top Bottom