Naona mmoja mmoja wanaanza kuamka sasa, wale kina Kigwangala na Lusinde iko siku wataona aibu tu, Rais lazima aambiwe ukweli ili kumuamsha ajue changamoto zilizo mbele yake na namna ya kuzikabili, kusifia sana kunadumaza akili.
Kwa namna Gambo alivyoongea na jinsi alivyoshangiliwa na wananchi wengi kwa sauti kubwa hivyo, naamini huu ni wakati mzuri kwa Samia kujiuliza kama kweli anaona Makamba bado anafaa kwenye hiyo wizara.