Mkurugenzi wa jiji Dkt John Pima ni miongoni mwa viongozi 9 walioangukia mikononi mwa Gambo katika vita wasioshinda.
Viongozi wengine ambao Gambo aliowatengenezea ajali na kuondolewa Arusha ni pamoja ,Mpanda aliyekuwa katibu mkuu wa ccm mkoa wa Arusha, Ntibenda aliyekuwa Arusha,Daqaro aliyekuwa DC Arusha, Dkt Maulid Madeni aliyekuwa Ded jiji la Arusha pamoja na viongozi kibao ndani ya CCM, pamoja Shana aliyekuwa RPC Arusha.
Tabia ya Gambo anataka kuabudiwa na kutukuzwa kama aliyokuwa akiabudiwa na marehemu Shana aliyekuwa RPC Arusha,Joseph Masawe M/kiti wa CCM Wilaya ya Arusha. Tabia hii lazima ccm wajifunze kuchagua viongozi watakaowaunganisha wananchi na viongozi na sio kuwagawa.
Unatuhumu kwa hoja za hewani...
Laiti ungekuwa unaweka na ushahidi wa namna walivyoonewa, ingeleta maana sana...
Lakini mpaka hapo unapiga mayowe tu kama mbwa koko yasiyo na ushahidi..
Mathalani kwa tukio la Pima na wenzake kusimamishwa kazi, lilikuwa televised live na kuonyesha kuwa kuna makosa ya wazi kabisa wameyafanya...
✓ Mkurugenzi na wenzake amelipa pesa kwa miradi isiyokuwepo..!
✓ Pesa ya mkandarasi x analipwa mtumishi wa halmashauri katika akaunti yake binafsi...!
✓ Mkurugenzi na mlipaji fedha wa Jiji wanasimamishwa mbele ya kadamnasi wakiwemo madiwani wawakilishi wa wananchi na kuulizwa iweje pesa ya mtu mkandarasi aliyefanya kazi ya serikali TZS 65,000,000 iingizwe kwenye akaunti ya mtu binafsi tena mtumishi wa halmashauri? Badala wajitetee kwa mantiki, wameishia kujiuma uma tu kuonyesha kuwa wamekosea na hawana la kujitetea..!!
✓ Ona hili pia. CED Pima na mlipa fedha na Afisa Mipango wa Jiji wanasimamishwa mbele ya kadamnasi, wanaulizwa mradi wa barabara wa TZS 65,000,000 uko mtaa na kata gani?
Cha ajabu anasema uongo kwa Diwani wa kata ile kukataa mbele yao kuwa hakuna mradi wa namna hiyo katani kwake...!!
Sasa hapa hata kama ungekuwa wewe ni PM, utajifunza nini? Moja kwa moja, utatambua kuwa pana upigaji, ufisadi..!!
Katika mazingira haya unapata wapi ujasiri wa kusema kuna uonevu hapo??
Umechemka..!!