Mrithi wa Samia ana kazi nzito kurudisha uchumi wa Tanzania kwenye Mstari

Mrithi wa Samia ana kazi nzito kurudisha uchumi wa Tanzania kwenye Mstari

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Katika Jambo linalotishia uhai wa taifa Letu ni kuelemwa na madeni huku pesa yetu ikikosa thamani kabisa, Hakuna juhudi zozote Za makusudi zinazofanywa na seriakli ya Samia kuokoa uchumi wa Taifa letu...

Ni masikitiko makubwa Kwamba Sasa watu wanchota mihela Kwa kadri wawezavyo nakukopa mikopo mikbwa mikubwa huku nchi ikiwa Hoi bin taabani . Mfumuko wa bei uliopo Nchini Siyo wa kitoto, wakati huo huo purchasing power ya hela yetu ikiwa Chini Sana,. Pia serikali ikizalisha mikodi ya kila Aina kukandamiza mwananchi wa kawaida...

Samia siyo Raisi wa Kwanza kuvuruga uchumi wa nchi yetu, wapo watangulizi wake waliowahi kufanya hivyo, Sina haja ya kuwataja Maana wanajulikana. Ila Kwa Bahati Nzuri maraisi waliokuwa wanafutia walikuwa wazalendo kiasi ambacho walirudisha uchumi Kwenye mstari.... .

Wasiwasi wangu je tutakuja kupata mtu mzalendo ambae atakuja kuweka uchumi wetu imara, Tuombe iwe hivo kama hatapatikana basi Taifa la Tanzania linaenda kuangamia kama mrithi wa Samia atakuwa na akili hizihizi Tunazoshuhudia Sasa.....

Tukae tukijua seriakli yoyote dhaifu huambatana na mambo yote ya hovyo hovyo, Kama migomo, Rushwa, matajiri kuiendesha serikali, manyanyaso kwa raia, hudumaa za jamii kuwa mbovu etc. etc..

My Advice
"When you're choosing a Top leader of the government, choose wisely." By me.
 
Acha Umbea; mama anafungulia nchi na ameongeza pesa kwenye mzunguko.

Umesikia juzi kulikuwa na bajeti ya wizara fulani ambayo sehemu kubwa inategemea mikopo na misaada kutoka nje, lakini ndani yake kuna 40b za posho kwa ajili ya kuongeza kwenye mzunguko!!
 
Acha Umbea; mama anafungulia nchi na ameongeza pesa kwenye mzunguko.

Umesikia juzi kulikuwa na bajeti ya wizara fulani ambayo sehemu kubwa inategemea mikopo na mkisaada kutoka nje, lakini ndani yake kuna 40b za posho kwa ajili ya kuongeza mzunguko!!
Wizara ya Ardhi Posho ni Bilioni 47 kutoka kwenye Mkopo wa Bilioni 330 kutoka Bank ya Dunia
 
mzalendo ambae atakuja kuweka uchumi wetu imara, Tuombe iwe hivo kama hatapatikana basi Taifa la Tanzania linaenda kuangamia kama mrithi wa Samia atakuwa na akili
Kwa akili yenu walinda legacy uzalendo ni kupora mali za matajiri na wenye bidii ya kazi na kutafuta mali huku mkipewa ahadi ya uongo mnaojiita wanyonge. Uchumi uliparaganyika sana kipindi kile.

Kwa kusaidia angalia ongezeko la deni la taifa kipindi kile na sasa. Mabenki ya biashara ya mabeberu yalikuwa yanafuata humu humu ndani kuingia nae mikataba ya kifedha ya mikopo ya riba kubwa na inayoiva haraka.
 
Samia kwa miaka michache kamzidi hayati Magufuli kwenye uchumi na diplomasia. Pia kwenye demokrasia na haki za binadamu kamzidi kwa mbali.

Udhaifu wake mkubwa uko kwenye usimamizi - hana basic skills. Competence yake kwenye good leadership ni ndogo.

Ila sasa afanye kazi moja tu muhimu, atupe Katiba Mpya. Akifanya hilo ataandika jjna lake kwa wino wa dhahabu katika historia ya Tanzania. Pia atakuwa na heshima na baraka hapa na milele
 
Aliharibu Mwinyi, Mkapa akapata kazi nzito kurudisha nchi kwenye mstari.

Akaja Msoga, ufisadi ukatamalaki. Magufuli akainyoosha kwa kasi.

Kaja mama, afanye yake. Alafu akimaliza aingie Mgalatia kusawazisha.

Ukweli ni kuwa, Wagalatia ndiyo hufanya kazi nzito mno. Na pengine vifo vyao huwahi kwa sababu ya mizigo mizito wanayojitwisha kwa maslahi ya nchi.
 
Katika Jambo linalotishia uhai wa taifa Letu ni kuelemwa na madeni huku pesa yetu ikikosa thamani kabisa, Hakuna juhudi zozote Za makusudi zinazofanywa na seriakli ya Samia kuokoa uchumi wa Taifa letu...

Ni masikitiko makubwa Kwamba Sasa watu wanchota mihela Kwa kadri wawezavyo nakukopa mikopo mikbwa mikubwa huku nchi ikiwa Hoi bin taabani . Mfumuko wa bei uliopo Nchini Siyo wa kitoto, wakati huo huo purchasing power ya hela yetu ikiwa Chini Sana,. Pia serikali ikizalisha mikodi ya kila Aina kukandamiza mwananchi wa kawaida...

Samia siyo Raisi wa Kwanza kuvuruga uchumi wa nchi yetu, wapo watangulizi wake waliowahi kufanya hivyo, Sina haja ya kuwataja Maana wanajulikana. Ila Kwa Bahati Nzuri maraisi waliokuwa wanafutia walikuwa wazalendo kiasi ambacho walirudisha uchumi Kwenye mstari.... .

Wasiwasi wangu je tutakuja kupata mtu mzalendo ambae atakuja kuweka uchumi wetu imara, Tuombe iwe hivo kama hatapatikana basi Taifa la Tanzania linaenda kuangamia kama mrithi wa Samia atakuwa na akili hizihizi Tunazoshuhudia Sasa.....

Tukae tukijua seriakli yoyote dhaifu huambatana na mambo yote ya hovyo hovyo, Kama migomo, Rushwa, matajiri kuiendesha serikali, manyanyaso kwa raia, hudumaa za jamii kuwa mbovu etc. etc..

My Advice
"When you're choosing a Top leader of the government, choose wisely." By me.
Nchi inapigwa kama ngoma, bila kujali chama dini n.k , sasa tunamwitaji mtu makini sana , nami nasema lazima badilisha kwanza mfumo wa kiongonzi kuiodoa ccm madarakani, tusitegemee kuwa na mtu bora pitia ccm ,wale Ni shida
 
Tuondolee uongo wako hapa. Benki ya Dunia pamoja na shirika la Fedha la kimataifa wote kwa pamoja wameipongeza Tanzania kwa kufanya vizuri katika uchumi,Wameonyesha hayo kwa Takwimu za ukuaji wetu wa uchumi pamoja na kuutabiria makubwa uchumi wetu. Sasa wewe Ni Nani Hadi upingi ripoti za kiutafiti kutoka Taasisi zinazoheshimika Duniani kwote? Kwanini usiweke nawewe ushahidi wako wa kitafiti kuliko kukurupuka na kuropoka Kama ulivyo fanya hapa?

Suala la Deni la Taofa. Katika hili pia Kama nchi na Taifa tupo katika Hali nzuri,kwa kuwa Deni letu Ni himilivu na bado tunao uwezo wa kukopa na kulipa bila shida. Lakini pia kukopa siyo shida maana Cha muhimu unapokopa uangalie na kuzingatia malengo ya mkopo,mahali unapowekeza,faida za mradi unapowekeza mkopo wako,masharti ya mkopo,riba ya mkopo husika, muda wa kufanya marejesho ya mkopo.

Serikali yetu ya mh Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania mama Samia suluhu Hassani imekuwa ikichukua na kupokea mikopo yenye masharti nafuu na ya muda mrefu na kuwekeza katika miradi yenye tija kwa Taifa letu.

Suala la mfumuko wa Bei .Hapa naona pia umejiandikia tu bila utafiti Bali kwa kuongozwa na mihemuko ,chuki binafsi na njaa yako kichwani, kwa kuwa kwa Sasa hatuna mfumuko wa Bei katika nchi yetu na pale ulipojitokeza serikali yetu ilikabiliana nao vyema,mfano wakati pembejeo za kilimo hasa mbolea zilipopanda Bei serikali ya Rais Samia ilitoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni, mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu. Lakini pia serikali ya Rais Samia ilikuwa inatoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi katika mafuta na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mafuta maeneo mbalimbali nchini na hivyo kuleta ahueni katika maisha ya watanzania,hasa kwa kuzingatia kuwa mafuta Ni injini ya uchumi wetu.

Watanzania wan Imani na mh Rais wetu mama Samia na serikali yake na ndio maana wamekuwa na wanaendelea kuiunga mkono kwa nguvu zao zote.
 
Nchi inapigwa kama ngoma, bila kujali chama dini n.k , sasa tunamwitaji mtu makini sana , nami nasema lazima badilisha kwanza mfumo wa kiongonzi kuiodoa ccm madarakani, tusitegemee kuwa na mtu bora pitia ccm ,wale Ni shida
Watanzania Wana imani kubwa Sana na serikali ya CCM , ndio maana wanaendelea kuiunga mkono kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka Unaogusa maisha Yao ya kila siku
 
Back
Top Bottom