Haya ni maoni yako na unaruhusiwa kuwa nayo. Ukiuliza wafanyabiashara halisi watakwambia namna SSH anavyoufufua uchumi uliokufa kipindi cha awamu ya tano.
Nenda kaongee na wenye frames zao kula Masaki , Kinondoni na katikati ya jiji watakwambia ahueni wanayoipata kipindi hiki cha Samia kulinganisha na cha JPM.
Sijui ulikuwa na umri gani wakati wa Magufuli kiasi cha kupitwa na ule unyama aliokuwa anawafanyia wafanyabiashara wa kanda ya kaskazini mpaka wakafunga mashamba ya maua wakati soko likiwa bado lipo kule Uholanzi.
JPM pengine alikuwa na nia njema lakini kuonyesha ule utayari wa kuumiza baadhi ya watu na wakati huo huo akawa na utayari tena wa wazi wazi kabisa wa kuwabeba baadhi, ule ulikuwa ni ufa mkubwa sana wa uongozi wake.
Ukosefu wa hekima ya kuishi na watu haswa jamii ya wafanyabiashara. Hakuwa na kule kujali vilio vya wadau wake muhimu wa maendeleo pia akawa na ukosefu wa busara za kuongoza taifa la Tanzania.
Samia anao uwezo wa kusikiliza na hafanyi maamuzi bila ya kufanya utafiti wa kina juu ya faida na madhara ya maamuzi atakayofanya.