Msaada aliyewahi kupata changamoto hii kwenye ajira

Msaada aliyewahi kupata changamoto hii kwenye ajira

BROTHER OF BROTHERS

Senior Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
113
Reaction score
159
Habari ndugu zangu, wakubwa shikamooni na wadogo habari zenu. Nasimama na kuleta hoja hii kwa niaba ya Ndugu (Brother from another Mother).

Mwaka jana 2023 huyu ndugu alifanikiwa kuomba ajira (Ajira Potal) na kufanikiwa kuitwa kufanya usaili alifanikiwa kufanya written na baadaye oral na hivyo alifaulu na kupata barua ya kuitwa kazini na Utumishi. Baada ya muda mfupi, kabla ya kufika kituo cha kazi aliombwa cheti halisi cha Form IV alikipeleka Necta, Baada ya hapo, aliombwa kutoa maelezo ya cheti chake alifanya hivyo kwa asilimia mia moja

Alitumiwa barua yenye kuonyesha wasiwasi wa matokeo ya masomo yake, hivyo akaombwa aende shule ya sekondari aliyosoma alifanya hivyo na alipewa yale yale matokeo ya awali ni zamani kidogo 2002. aliweza kufanya comparison na aliona somo moja lililoandikwa Agriculture Science badala ya Agricultural Science, Huyu ndugu anateseka sana hivi sasa ukizingatia muda aliosota kwenye masomo ni mwingi, pia Umri umesonga anategemewa na familia .

Tunatafuta msaada kwa wenye uwezo watusaidie kupata Suluhu ya hili Tatizo na kama kuna Sehemu sahihi ya kufika. Mpaka hivi sasa huyu bwana amepata Frustration na ufanisi wake wa kazi umeshuka kwani hajui pakuanzia na ni kweli alisoma na alifanikiwa kupata cheti na kuendelea na masomo ya Elimu ya Juu.

Kwa heshima na Taadhima naomba Msaada wa Mawazo, Ushahuri chanya juu ya nini chakufanya kufanikisha hili jambo. Naomba Kuwasilisha
 
Kwani msemaji wa mwisho kuhusu cheti cha sekondari ni nani?
Shule na NECTA, nani anatoa cheti?
Somo laweza kuwa Agriculture au Agricultural Science.
 
Naam, kwa tafsiri ya maelezo hayo kunaonekana kuna kamchezo kalichezwa Necta 2002 vyeti vyao havikuwa na picha ni index number pekee, Utata Necta ni somo la AGRICULTURAL Science kuandikwa AGRICULTURE Science kwa waliosoma masomo haya wanaelewa sana......
KWanza hata hiyo grammar ya Agriculture science haipo.
 
Hatua za kuchukua katika lipi!? Ajira au agriculture science? Katika hoja Yako umeeleza mambo makuu mawili na hujasema lipi linataka msaada
Ndugu yangu YOTE hapo yanataka maajibu au msaada wakina wa Hatua gani zakufuata bila kuvunja sheria
 
Back
Top Bottom