MSAADA - ambaye ameshadeal na kuachwa na ndege / “no show” na Turkish airlines anisaidie

Aisee
Waingereza poa sana
Wakati ule British Airways inatua bongo, nilichanganya madesa, kumbe ndege inaondoka saa moja asubuhi nikadhani ni saa7 mchana, mwenyewe natinga na mabegi yangu kwa madaha, kufika security wananiuliza unaondoka na ndege gani, mwenyewe kwa mikogo nikasema BA, wakanichekaaa...😀
Ila nilienda ofisi yao wakati huo Movenpick, wakaniambia next flight wewe nenda airport halafu subiri abiria wote wakipanda ndio unaiingia wa mwisho.
Nikajikuta na wazungu wengine wawili na wao wanasubiri hivyohivyo, bahati wote tulipata siti na nilipata ile legroom kabisa sikuamini na sikutoa hata senti ya kuongeza kwa kukosa ndege awali......
 
Bora aende ofisini kwao, customer care yao wabovu sana, na kiingereza kibovu hata hamuelewani.
Mimi kuna wakati nilikosea jina la waifu kwenye kukata ticket, si wakamtoa kwenye booking yangu na kumtengenezea yake tofauti ikawa mawenge kweli siku tunatoa boarding pass....maswali mengi
 
Hapo anapambana na muda, akienda kwa ofisi zao kama ni Dar nao watawapigia tena Istanbul na kama sikosei TR nyingine ni alfajiri ya kesho, Mara nyingi kwa no show (not normal cancellation) consideration hasa kwa economy class ni next available flight ili pia aweze ku preserve return/outbound flight kabla haijacancel kwenye system
 
Apige simu Call Center haraka na aongee na customer care wa Turkish Airlines, sio travel agents popote, wao wana access ya hizo information, kama imeshatua taarifa zinafutwa na kama ni round trip hata ya kurudia ataikosa,
Asante, amefanikiwa kuwapata kwenye call, fare difference ya kuondoka this week or next week ni double the ticket price, ila wamemsaidia na atatumia the same ticket next year and pay $250 fare difference.

But for this trip inabidi akate tu tiketi nyingine!
 
Aangalie kwenye ticket kama alikata hardcopy kuna terms and conditions ila hawezi kupata refund bali anaweza kubadilisha within 24hrs kwa kuomba ticket mpya na kulipia re-issue (rebooking) na tofauti (fare difference) kama ipo
Asante kiongozi, ni hivyo ila watareissue ila wamesema anaweza kubadili na kufanya safari tarehe yoyote mpaka next year August.

Kwa sasa inabidi akate tiketi nyingine tu, kwa sababu fare difference ni kubwa sana.
 
Na asiwe amekata go n return wohiii 😹😹😹
Ingekuwa New force unachukua boda unalifukuzia, pipa sasa likiyeya limeyeya baba Jeni bye bye 🤣
Mamie na machungu umenichekeshaje 😂 😂

Hapa nimemaliza kupiga simu naambiwa tofauti ya bei ya tiketi inayobidi iongezwe $1,700 na penalty dola 100, nimechoka 😂nikamkumbuka boda wangu tuliyewahi kukimbiza naye Kimbinyiko mpaka kibaha.
 
Asante kwa uzoefu, ulikua na bahati ukapata new tiketi kwa fare difference ndogo.
Hii pia ilikua ni international flight na wanareissue new ticket kwa penalty, ila unfortunately fare difference ni kubwa sana kwa kusafiri in the coming days.

Kwake hili ni somo la kufanya maandalizi kwa Umakini, amejifunza na naamini kosa halitajirudia tena!
 
Kama uko Dar watembelee ofini kwao au wapigie simu kwa maelezo sahihi.
👇
Turkish Airlines Dar es Salaam Office Address: Azikiwe St, Dar es Salaam, Tanzania Phone Number: +255222116683 Working Hours: 24 hour
Asante sana kiongozi 🙏
 
Akate upya kwa siku yenye usafiri, kurudishiwa salio itakuwa ngumu.
Inategemea aina ya tiketi. Kama tiketi yake inaonyesha gharama za no show au kubadilisha tarehe awasiliane na alikokata tiketi ( kwa kurahisisha) watampa tiketi mpya akilipa hiyo gharama. Tiketi nyingine za bei ya chini haziruhusu mabadiliko yeyote. Ukiwa na hizo inakula kwako. Na kuna zile za gharama ya juu ambazo zinakuruhusu kubadilisha bila gharama yeyote. Ndugu yako aandae 200 dola ajiondokee. Ila wanaweza kumwambia bei ya tiketi ya siku anayotaka kuondoka ni ya juu zaidi hivyo alipie ile tofauti na US 200. Inabidi awe makini anapoongea nao.

Amandla...
 
Msiwe mnaagaaga vijana mnaposafiri safari ambazo huku Africa tunaamini tayari umetoboa.

Unaweza ukajikuta hufiki airport, wewe kila ukifika Tazara unarudi kuelekea buguruni ndani ya mitaa ya Afghanistan.
Daah 😂

Haya, next time atazingatia!
 
Mwaka 2018 niliwahi kudate mtoto mmoja wa kishua alikua anasoma Cyprus. Aliniomba nibook online ticket Turkish Airlines na akanitumia details za VISA card yake nikalipia kabisa. Safari ilikua saa 9 usiku. Akachanganya tarehe siku ya kuondoka no show. Alilipa fine ya $150 akaondoka siku nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…