MSAADA - ambaye ameshadeal na kuachwa na ndege / “no show” na Turkish airlines anisaidie

MSAADA - ambaye ameshadeal na kuachwa na ndege / “no show” na Turkish airlines anisaidie

Mimi nilipata tatizo na ndege nikajifunza kitu, ukiwa na shida ongea moja kwa moja na shirika la ndege na sio agents. Huko watamzungusha tu bila kumpa muafaka.
Kweli kabisa, tumeongea nao directly wamekua na msaada wa moja kwa moja.
 
Aisee
Waingereza poa sana
Wakati ule British Airways inatua bongo, nilichanganya madesa, kumbe ndege inaondoka saa moja asubuhi nikadhani ni saa7 mchana, mwenyewe natinga na mabegi yangu kwa madaha, kufika security wananiuliza unaondoka na ndege gani, mwenyewe kwa mikogo nikasema BA, wakanichekaaa...😀
Ila nilienda ofisi yao wakati huo Movenpick, wakaniambia next flight wewe nenda airport halafu subiri abiria wote wakipanda ndio unaiingia wa mwisho.
Nikajikuta na wazungu wengine wawili na wao wanasubiri hivyohivyo, bahati wote tulipata siti na nilipata ile legroom kabisa sikuamini na sikutoa hata senti ya kuongeza kwa kukosa ndege awali......
Daah hii ya kuchanganya ndege kumbe inawakumba wengi, ila naona ulipata bahati sana, pole na hongera!
 
Bora aende ofisini kwao, customer care yao wabovu sana, na kiingereza kibovu hata hamuelewani.
Mimi kuna wakati nilikosea jina la waifu kwenye kukata ticket, si wakamtoa kwenye booking yangu na kumtengenezea yake tofauti ikawa mawenge kweli siku tunatoa boarding pass....maswali mengi
Mimi nimeongea na mmoja, anaongea kingereza safi na ametusaidia sana!
 
Nashangaa kwa swali lake hapa wakati he could gat all info's from the call centre. Haya wewe mjuaji wacha mimi niendelee kushangaa kwa kadri uwazavyo.
Sasa hujaona nimejibu kwamba tulikua tunajaribu kote kote. unajua muda wa kusubiri kwenye hizo call center lakini?

Tupunguze ujuaji kwenye kila kitu jamani, humu kuna watu ambao nao wameshakua kwenye same situations safarini na wametoa experience zao na ushauri ambao umetusaidia.
 
Inategemea aina ya tiketi. Kama tiketi yake inaonyesha gharama za no show au kubadilisha tarehe awasiliane na alikokata tiketi ( kwa kurahisisha) watampa tiketi mpya akilipa hiyo gharama. Tiketi nyingine za bei ya chini haziruhusu mabadiliko yeyote. Ukiwa na hizo inakula kwako. Na kuna zile za gharama ya juu ambazo zinakuruhusu kubadilisha bila gharama yeyote. Ndugu yako aandae 200 dola ajiondokee. Ila wanaweza kumwambia bei ya tiketi ya siku anayotaka kuondoka ni ya juu zaidi hivyo alipie ile tofauti na US 200. Inabidi awe makini anapoongea nao.

Amandla...
Asante Fundi 🙏
 
Asante, yes inaonyesha anaweza kuchange with a penalty ila tatizo hawezi kuaccess her ticket online anymore, I guess sababu wameshaicancel ticket, hapo ndiyo hajui afanyaje.

View attachment 3441556

Awapigie simu au kwenye website yao lazima utakuwa na into zaidi za kuwafikia hata labda wana chat ot. Sijawahi kusafiri nao ila kama ni no show basi atalipia kiasi alivhoambiwa kwa T&C za tiketi yake yeye(usifananishe na wengine labda kama yao yapo sawa)

Bora kuwahi maana bei ya ticket ikitofautiana mara nyingi mtu unaambiwa ulipie tofauti yake.

Kama alinunua tiketi kwa agent awasiliane nao, kama online awatafute.
 
Kama ndege bado iko hewani, information zako bado outbound airport wanazo, unaingia tu airport unapambana nao humo wanakuweka next flight😀
 
Ilishawahi kunitokea hii hukooo kwa wenyewe kwa kutokuwa makini katika kusoma masaa ya safari. Nilidhani kuwa safari ipo kesho yake kumbe ni saa 6 na dakika mbili za usiku wa siku ile ile (2 minutes after midnight). Kesho yake kweli nikatimba airport kumbe safari ilikuwa jana yake na watu wameshafika huko walikokuwa wanakwenda.

Niseme tu pengine Mungu Alikuwa upande wangu maana nilipelekwa kwa mkuu mmoja hivi akahangaika wee ili niweze kuondoka usiku huo huo. Tatizo ikawa economy zote zimejaa ila huko business class kulikuwa na siti mbili ziko empty. Akaniangalia weee akaniambia niongezee dola 250 tu. Kweli nikaongeza huyoo nikapelekwa business classs. Na hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kusafiri business class aisee. Bahati nzuri nikiwa nasafiri haya masafari marefu huwa naweka pamba za kueleweka na sikuwa out of place. Pengine walidhani ni bonge la businessman kumbe mlima nyanya na dengu tu kutoka Misungwi....

Huyo kuna hela watamwambia aongezee na akifanya hivyo watambump kama kuna ndege ina nafasi. Ila ni vizuri kusoma terms and conditions maana kila shirika la ndege lina sheria zake. Na pia kuna tiketi kama zile za discount kubwa huwa hazina mwanya wo wote. Ukikosea tu ndiyo imekula kwako mazima. Na awe makini zaidi siku zingine. Afike airport masaa angalau matatu kabla ya safari na kama kuna dharula ahangaike kubadilisha safari mapema!
Bhagosha mashikolo mageni, naseka sana nene
 
Msiwe mnaagaaga vijana mnaposafiri safari ambazo huku Africa tunaamini tayari umetoboa.

Unaweza ukajikuta hufiki airport, wewe kila ukifika Tazara unarudi kuelekea buguruni.

ndani ya mitaa ya Afghanistan.
Ume nikumbusha uki taka kuondoka, una sema naenda mtoni kufua.

wakija kushituka uko location nyingine, lose lips sink ships ali sema Kiranga
 
Refund hawezi kupata, just achange travel plan aombe ticket mpya in 24hrs wataona wampe.ipi, kama kina cost kodogo itazidi alipie tu no way out
 
Back
Top Bottom