MSAADA - ambaye ameshadeal na kuachwa na ndege / “no show” na Turkish airlines anisaidie

Awapigie simu au kwenye website yao lazima utakuwa na into zaidi za kuwafikia hata labda wana chat ot. Sijawahi kusafiri nao ila kama ni no show basi atalipia kiasi alivhoambiwa kwa T&C za tiketi yake yeye(usifananishe na wengine labda kama yao yapo sawa)

Bora kuwahi maana bei ya ticket ikitofautiana mara nyingi mtu unaambiwa ulipie tofauti yake.

Kama alinunua tiketi kwa agent awasiliane nao, kama online awatafute.
Asante dada, tumefanya hivi na tumefanikisha.

Turkish huwa hawana chat kwenye website ila through help desk yao ya Twitter wametupatia namba ya simu ya watu wa call center wakatusaidia.
 
Kama ndege bado iko hewani, information zako bado outbound airport wanazo, unaingia tu airport unapambana nao humo wanakuweka next flight😀
Bado ipo hewani ila watu wa airline walimgomea kabisa 😅.
 
Mdogo wangu amechanganya tarehe na muda akamiss flight yake.
Tiketi yake inaonyesha kwamba kuna penalty ya $200 ya no show. 

MASWALI:
  1. Je anaweza kuchange flight na kulipia hiyo $200 au how does it work?

  2. Au inabidi akate tiketi nyingine halafu aclaim refund?
Kwa sasa akiingiza taarifa za reservation yake anapata hili jibu, mwenye uzoefu na hii ishu anisaidie.

View attachment 3441541
Analipa hiyo fine kisha anapangiwa route nyingine
 
min -me (pia naomba niitie wazoefu wengine)

Cc: Mshana Jr , Grahams , Ushimen
Uzoefu wangu wa karibuni kabisa
Nilikuwa narudi bongo. Nikapata booking Air Tanzania nikalipia online.. Ndege ilikuwa inaondoka siku inayofuata saa moja kamili asubuhi lakini reporting time saa 11 alfajiri
Jioni ile nikawa na kazi ya kumalizia ambayo kuna mtu alinichelewesha kwahiyo ilibidi tuifanye mpaka saa nane na nusu usiku
Mpaka napanda kitandani ilikuwa saa tisa! Nikaamini nitalala kidogo niamke niwahi airport mwendo wa nususaa hivi kwa alfajiri
Nikapiliza nikaamka 12:25 hivi.. Nikaitisha bolt iniwahishe airport., ambako nilifika 12: 35 na kuambiwa ndege imeshaondoka! Nikaelekezwa niende office a za Air Tanzania pale airport nikalalamike
Kufika pale naambiwa nilichelewa mwenyewe kwakuwa reporting time ni saa 11 na ndege imeondoka 12:30 hivyo nilipie faini ya usd 236.. Sikuwa na jinsi nikalipa na kupangiwa ndege ya usiku
 
Asante, yes inaonyesha anaweza kuchange with a penalty ila tatizo hawezi kuaccess her ticket online anymore, I guess sababu wameshaicancel ticket, hapo ndiyo hajui afanyaje.

View attachment 3441556
Sasa si inatakiwa aende pale Airport kwenye ofisi yao hao turkish Airlines kwenye table yao(customer service representatives) awaulize kisha atalipia hiyo fine kisha watambadilishia ticket.
Mbona huyo ndugu yako ni mzito sana sasa akifika huko nje atasurvive vipi?
Kumbuka nchi za watu huko hakuna utamaduni wa kusimamisha watu hovyo kuulizauliza kila kitu kipo kwenye sign boards na system.
Siku nyingine akikosa ndege kwa kuchelewa mwambie asirudi nyumbani hadi awaone wahusika pale pale ili apate muafaka wa safari yake.
Kama hela ya fine iko sio ishu kubwa sana ilishawahi kunitokea mara nyingi sana hiyo inshu
 
Kwa nini unauliza maswali nani kujijibu mwenyewe? Hawezi kwenda kuulizia kwenye ofisi zao akapata msaada zaidi? Eti I guess! Come on!
 
Uzoefu wangu wa karibuni kabisa
Nilikuwa narudi bongo. Nikapata booking Air Tanzania nikalipia online.. Ndege ilikuwa inaondoka siku inayofuata saa moja kamili asubuhi lakini reporting time saa 11 alfajiri
Jioni ile nikawa na kazi ya kumalizia ambayo kuna mtu alinichelewesha kwahiyo ilibidi tuifanye mpaka saa nane na nusu usiku
Mpaka napanda kitandani ilikuwa saa tisa! Nikaamini nitalala kidogo niamke niwahi airport mwendo wa nususaa hivi kwa alfajiri
Nikapiliza nikaamka 12:25 hivi.. Nikaitisha bolt iniwahishe airport., ambako nilifika 12: 35 na kuambiwa ndege imeshaondoka! Nikaelekezwa niende office a za Air Tanzania pale airport nikalalamike
Kufika pale naambiwa nilichelewa mwenyewe kwakuwa reporting time ni saa 11 na ndege imeondoka 12:30 hivyo nilipie faini ya usd 236.. Sikuwa na jinsi nikalipa na kupangiwa ndege ya usiku
kwa experience yako watu huwa tunaamua kwenda kuzuga airport kusogeza muda. nilwahi kwenda India ndege ya saa 9 usiku jamaa host wetu wakatupeleka airport saa 3 wakijua mbalanga za foleni mjin, kama utalala tu mbele ya safari. Ikibidi kwa hiyo fine unaweza kukuta ni bora kukata ticket nyingine kwa gharama nafuu zaidi. ilishanitokea natoka Arusha ATC ya alfajiri kufika katikati hapo mvua imenyesha imesomba daraja na nishacheck online, mpaka nachomoka kufika airport ndege imeondoka, kuangalia gharama ya kufidia nikacheck na Precision iko chini ya hiyo na nafasi ipo inaanza kutua, ikabidi nikate hiyo badala ya kurud mjini kusubiri ya jioni
 
Mdogo wangu amechanganya tarehe na muda akamiss flight yake.
Tiketi yake inaonyesha kwamba kuna penalty ya $200 ya no show. 

MASWALI:
  1. Je anaweza kuchange flight na kulipia hiyo $200 au how does it work?

  2. Au inabidi akate tiketi nyingine halafu aclaim refund?
Kwa sasa akiingiza taarifa za reservation yake anapata hili jibu, mwenye uzoefu na hii ishu anisaidie.

View attachment 3441541
Una uhakika Turkish Airlines wana account humu JF?
 
Aliweza kuingia ndani? Labda ni hao Turkish wachovu. Kuna jamaa yangu aliachwa hivyo hapo JKIA na KLM kaingia ndani walimweka next flight bure. Experience yangu pia ukipambana nao lazima wakupe flight cha muhimu uwe airport ndani
Hatokei bongo, aliingia airport ndani ila kwa sababu alichelewa masaa mengi, Turkish walikua wameshafunga check in counter na hawakua na ofisi kwenye hiyo airport.
 
Uzoefu wangu wa karibuni kabisa
Nilikuwa narudi bongo. Nikapata booking Air Tanzania nikalipia online.. Ndege ilikuwa inaondoka siku inayofuata saa moja kamili asubuhi lakini reporting time saa 11 alfajiri
Jioni ile nikawa na kazi ya kumalizia ambayo kuna mtu alinichelewesha kwahiyo ilibidi tuifanye mpaka saa nane na nusu usiku
Mpaka napanda kitandani ilikuwa saa tisa! Nikaamini nitalala kidogo niamke niwahi airport mwendo wa nususaa hivi kwa alfajiri
Nikapiliza nikaamka 12:25 hivi.. Nikaitisha bolt iniwahishe airport., ambako nilifika 12: 35 na kuambiwa ndege imeshaondoka! Nikaelekezwa niende office a za Air Tanzania pale airport nikalalamike
Kufika pale naambiwa nilichelewa mwenyewe kwakuwa reporting time ni saa 11 na ndege imeondoka 12:30 hivyo nilipie faini ya usd 236.. Sikuwa na jinsi nikalipa na kupangiwa ndege ya usiku
Asante kwa kushare kaka Mshana, mambo haya yanatokea, mara nyingi bila kutarajia.
Bora wewe ulipata replacement flight ya siku hiyo hiyo na faini haikua ya kutisha sana.
 
Sasa si inatakiwa aende pale Airport kwenye ofisi yao hao turkish Airlines kwenye table yao(customer service representatives) awaulize kisha atalipia hiyo fine kisha watambadilishia ticket.
Mbona huyo ndugu yako ni mzito sana sasa akifika huko nje atasurvive vipi?
Kumbuka nchi za watu huko hakuna utamaduni wa kusimamisha watu hovyo kuulizauliza kila kitu kipo kwenye sign boards na system.
Siku nyingine akikosa ndege kwa kuchelewa mwambie asirudi nyumbani hadi awaone wahusika pale pale ili apate muafaka wa safari yake.
Kama hela ya fine iko sio ishu kubwa sana ilishawahi kunitokea mara nyingi sana hiyo inshu
Hayuko Tz, anatokea Europe anarudi Bongo.
kama umesafiri mara nyingi, unajua si kila airport wana customer representative wa kila airline.

Dogo alifika check in counter zimeshafungwa na hakukua na customer desk ya Turkish airlines.
 
min -me (pia naomba niitie wazoefu wengine)

Cc: Mshana Jr , Grahams , Ushimen
Nimechelewa kufika Mjukuu pamoja na kuniita Kwa sauti.

Babu yenu nilikuwa shambani tangu juzi, ambapo network haikuwa active sana 🙌

Natumai utakuwa umepata mwongozo sahihi.

Ila unachotakiwa kufanya ni kwenda ukiwa na tiketi yako zilipo Ofisi za Turkish airlines ndani ya masaa 24 ukiwaeleza ulipata changamoto either za kiafya (You can cook and provide evidence) ili wakupatie nafasi ya kusafiri Kwa schedule ya next day.

Next time, mwambie ndugu wako aongeze umakini anapofanya booking ya safari hasa na mashirika makubwa ya Ndege

Hizi za kwetu za ndani wanaweza kuwa waelewa, ila hayo ya nje ni hadi kuwa na dharula inayoeleweka

Ndiyo maana nikashauri upike taarifa za kuugua kabla ya hiyo safari
 
Back
Top Bottom