Kalunya
JF-Expert Member
- Oct 5, 2021
- 13,322
- 18,609
True Elimu pekee haitoshi zama zimebadilika kama hali inaruhusu unamfunza kumiliki biashara kidogo kidogo so akiwa na vyeti pamoja na ujuzi hawezi kuwa tegemezi.Kuna kitu cha kujifunza kutoka kwa mtoa mada. Wazazi tunatakiwa kuwajengea watoto wetu uwezo wa kujitegemea siku za baadaye kupitia elimu bora na pia kuwaelimisha kuhusu umiliki wa mali. Kwenye hii mada, baba na mtoto wake wote kwa pamoja wanahusika kwa hii sintofahamu.
Binafsi najitahidi kuwaambia vijana wangu kusoma kwa bidii kupitia mamilioni ya shilingi kwa mwaka kama ada zao za shule, kwa sababu hiyo elimu ndiyo urithi wao wa baadaye! Na kamwe wasizifikirie mali zangu ambazo nazitafuta kwa shida.
Ukimjaza mtoto aina hii ya maneno, na ukiwekeza kwenye kumpatia elimu bora! Kamwe hawezi kubweteka kama mtoa mada! Unless awe na kichwa kibovu. Inasikitisha katikaa umri wake huo, mtoa mada bado anaota kupata mgao wa mali kutoka kwa baba yake, na ambaye bado yuko hai.
Wasomee kile watakachokuja kufanya ukubwani.Wakati wa likizo au weekend unakuwa nao field mfano garage,dukani, kwenye ujenzi,uvuvi, mifugo, shambani,mgodini,sokoni,nk.
So hata asipoajiriwa tayari anayo nguzo ya maisha.Na sio amalize masters kisha aanze kuendesha bodaboda.