Msaada: Baba yangu mzazi ameuza nyumba yake na hataki kunipatia pesa japo kidogo

HApo Mzeya chakufanya ni moja tuu...wee mpeleke mbele za haki kwa muumba maana ana roho mbaya sana huo baba yako. Alafu fanya aliyofanya yule kijana arusha....waambie kabisa polisi hamna shida ya upelelezi mie ndio nimemtoa roho sababu ikiwa ni roho mbaya ya baba
 
Ni mali ya baba yangu ila mimi ni mtoto wa wake kabisa kabisa wa kumzaa
Unajuaje kama ni baba yako, inawezekana Mama yako alikwishamuumiza hapo nyuma kwa kumwambia hao siyo watoto wake. Ndo maana mzee kauza nyumba asije acha urithi kwa watu baki, hayo yapo sana kwenye jamiii zetu. Akina Mama wengi wanaharibu familia zao kwa maneno yasiyofaa kwa waume zao, hivyo kuharibu familia nzima. Kwa hali ya kawaida baba mwenye upendo kwa watoto wake usingekosa hata 10million, . Pia inawezekana wewe ni mfuja Mali, upo upo tu. Huna mbele wala nyuma na miaka yote hiyo 41. Kwa hali ya kawaida miaka hiyo ulitakiwa uwe na mji wako na nyumba yako au apartment yako na Maisha yako.
 
Kuua mtu ni kiwango cha chini sana cha kufikiri, kwann asitafute vyake
 
Ushauri wako ni kama nguvu za giza.
 
Kuua mtu ni kiwango cha chini sana cha kufikiri, kwann asitafute vyake

Wazazi wengine wanakera bwana....sasa wee umenizaa kwa kutaka raha yako ya maisha leo hutaki na mie nifurahie maisha basi bora nikudedishe tuu.
 
Yaani miaka 41 bado unamtegemea Mzee wako ndo akupe maisha hata ukipewa zote hizo ndani ya miezi 3 zimekwisha.Kama uliweza tafuna 270000 kwa siku tatu wakati huo ni mtaji tosha
 
KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI.

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.


2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.


3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?


4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani?


6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.


12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli...


" Kama mnataka Mali mtaipata Shambani".
Kila la Heri Mkuu.

La Aquila non capit muscas!
 
Una akili nzur kweli wewe lakini ?
 
Hahaha naomlna aibu Bro.

Ilitakiwa hela yako utafute mwenyewe kwenye kuuza nyumba ungechukua dau la baab iyo milioni 200+ alafu ungeongeza yako sasa ifike milioni 320 ungekamata kibunda chako kizuri tu ukaangalie maisha mengine mbele.

Huwezi mlazimisha akupatie fedha hata kisheria haiwezekani labda tu kama mliingia makubaliano yakukulipa fedha kwa kazi ya kuuza nyumba, ila kama mtoto wake tena 40+ hauwezi mlazimisha popote Bro. Pole pia maana hii pengine sio habari njema kwako.
 
Mkuu,

Bado kidogo utaufikiria ujambazi wa kumuua baba yako kwa mali yake. Hayo tumeyaona.

Hiyo mali haikuhusu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…