Msaada: Baba yangu mzazi ameuza nyumba yake na hataki kunipatia pesa japo kidogo

Hiyo nyumba ni yake na mkewe period. Wewe kajenge yako uuze. Wewe hukusiki wala hukuchangia chochote alaa.
 
Mleta mada hupaswi kulalamika hata chembe.
Ninachoweza kukushauri kukupa connection uende Mombasa utapewa pesa unayotaka zaidi ya hiyo baba yako aliyopata baada ya kuuza nyumba yake.
 
pole sana mkuu nakushauri kubaliana na mawazo yake mzee cha msingi upambane ujitafutie cha kwako.

Hapo huenda hakuwa na maelewano mazuri na Mama yako na huenda na wewe unamsikiliza Mama kuliko yeye... lakini huu ni mtazamo wangu tuu.
IMG_20220104_153911.jpg
 
Hiyo laki 2 uliyotumia ingetosha hata kukurudisha kijijini, fikiria miaka 20 mbeleni mwanao naye atataka umgawie mali je utampa nini? Stuka usingizini
 
Dah! Ukachoma zaidi ya 200k kufurahia pesa ambayo hauna uhakika nayo?

Sasa umpelekeka mzee mahakamani kwani unamdai kitu gani? Ingekua amefariki ungestahili mirathi.

Mie nilivyomaliza kidato cha sita nikaanza maisha sikuwahi kuomba hata kijiko kutoka kwa Mzee.

Usipobadili mtizamo kuhusu maisha, utalaumu watu sana mkuu
 
Habari zenu ndugu zangu, naombeni ushauri wenu kwenye ili naamini uku jukwaani kuna wenye ushauri bora zaidi na wenye experince na mambo mbalimbali, mimi ni kijana wa umri wa miaka 41, kwetu tumezaliwa 4 ila kwa sasa tumebaki 3 baada ya mmoja bahati mbaya kufariki miaka 6 iliyo pita, mimi ni mtoto wa tatu kwenye familia.

Baba yangu alijenga DAR ES SALAAM miaka mingi iliyo pita, sasa mwezi uliopita 12/2021 alikuja na mtazamo wake na kutueleza sisi watoto wake kuwa anataka kuuza nyumba yake hii na aende akaamie kijijini na kuchagua maisha yake yote ataishi uko.

Upande wangu nilipokea ombi lake ilo kwa furaha sana maana niliona kabisa kuwa baba akiuza ntapata pesa na mimi ya kuanzia maisha, baada ya kusema ivyo nikaingia kwenye miangaiko ya kutafuta mteja na dalali ambaye atasaidia iyo nyumba iuzwe haraka, mungu si Athumani ndani ya week mbili tu akatokea mteja akiwa anaitaka iyo nyumba kwa sh milion 245 (maana nyumba ipo eneo zuri sana).

Dalali alimleta yule mteja na kuikagua nyumba nzima na eneo na uyo mteja aliahidi kuja kufanya malipo baada ya siku 3, uwezi amini nilifurahi sana sana nilikuwa na bajeti yangu ya laki 2 na elfu 70 kwa furaha nzima iyo ela niliitumia kwa kufurahia maana nilijua kabisa nimesha kula maisha. Baada ya siku 3 kweli yule mnunuzi alikuja na kufanya malipo na kukamilisha kila kitu,

Ndugu zangu nashindwa ata kuandika vizuri, baba baada ya kupokea pesa ataki ata kunishirikisha kwa chochote, hajanipa ata sent kumi yake kwenye iyo ela, baada ya siku mbili kupita mzee akiwa kimya ikabidi nimuambie baba vipi kuhusu ela ya mauzo ya nyumba unioni mwanao na mimi nikaangalie maisha yangu mbele ya safari, baba amenijibu tu kwa wepesi kabisa eti "SAWA NENDA KAANGALIE MAISHA TU, NAKUTAKIA KILA LENYE HERI" nikamuambia baba naendaje kuangalia maisha wakati ujanipa chochote, akaniambia kwani nadai nini kwake, kwa kweli ni kauli zilizo nivunja sana moyo na kunikatisha kabisa tamaa ya kuishi.

Noambeni ushauri wenu ili fate atua za kisheria mzee aweze kunipa na mimi upande wa maali kama mtoto wake wa kumzaa, maana nina week sasaivi sina furaha kabisa na aya maisha, naombeni sana ushauri wa haraka, maana baba siwezi kumtazama ata usoni ananipa sana hasira.

Matumaini yangu nitapata ushauri mzuri na wakufanya nipate aki yangu.
Nimecheka kinoma yani huyo mshua mimi kabisa miaka kadhaa mbele
 
nyumba ni yetu, maana nimezaliwa hapo hapo
Una share ngapi kwenye hiyo nyumba? Kuzaliwa humo hai-justify your ownership. Ninyi ndio hamkawii kuwauwa wazazi wenu kwa sababu ya mali zao; ref. lile jinga la Arusha lililomuua mama yake mzazi.
 
Habari zenu ndugu zangu, naombeni ushauri wenu kwenye ili naamini uku jukwaani kuna wenye ushauri bora zaidi na wenye experince na mambo mbalimbali, mimi ni kijana wa umri wa miaka 41, kwetu tumezaliwa 4 ila kwa sasa tumebaki 3 baada ya mmoja bahati mbaya kufariki miaka 6 iliyo pita, mimi ni mtoto wa tatu kwenye familia.

Baba yangu alijenga DAR ES SALAAM miaka mingi iliyo pita, sasa mwezi uliopita 12/2021 alikuja na mtazamo wake na kutueleza sisi watoto wake kuwa anataka kuuza nyumba yake hii na aende akaamie kijijini na kuchagua maisha yake yote ataishi uko.

Upande wangu nilipokea ombi lake ilo kwa furaha sana maana niliona kabisa kuwa baba akiuza ntapata pesa na mimi ya kuanzia maisha, baada ya kusema ivyo nikaingia kwenye miangaiko ya kutafuta mteja na dalali ambaye atasaidia iyo nyumba iuzwe haraka, mungu si Athumani ndani ya week mbili tu akatokea mteja akiwa anaitaka iyo nyumba kwa sh milion 245 (maana nyumba ipo eneo zuri sana).

Dalali alimleta yule mteja na kuikagua nyumba nzima na eneo na uyo mteja aliahidi kuja kufanya malipo baada ya siku 3, uwezi amini nilifurahi sana sana nilikuwa na bajeti yangu ya laki 2 na elfu 70 kwa furaha nzima iyo ela niliitumia kwa kufurahia maana nilijua kabisa nimesha kula maisha. Baada ya siku 3 kweli yule mnunuzi alikuja na kufanya malipo na kukamilisha kila kitu,

Ndugu zangu nashindwa ata kuandika vizuri, baba baada ya kupokea pesa ataki ata kunishirikisha kwa chochote, hajanipa ata sent kumi yake kwenye iyo ela, baada ya siku mbili kupita mzee akiwa kimya ikabidi nimuambie baba vipi kuhusu ela ya mauzo ya nyumba unioni mwanao na mimi nikaangalie maisha yangu mbele ya safari, baba amenijibu tu kwa wepesi kabisa eti "SAWA NENDA KAANGALIE MAISHA TU, NAKUTAKIA KILA LENYE HERI" nikamuambia baba naendaje kuangalia maisha wakati ujanipa chochote, akaniambia kwani nadai nini kwake, kwa kweli ni kauli zilizo nivunja sana moyo na kunikatisha kabisa tamaa ya kuishi.

Noambeni ushauri wenu ili fate atua za kisheria mzee aweze kunipa na mimi upande wa maali kama mtoto wake wa kumzaa, maana nina week sasaivi sina furaha kabisa na aya maisha, naombeni sana ushauri wa haraka, maana baba siwezi kumtazama ata usoni ananipa sana hasira.

Matumaini yangu nitapata ushauri mzuri na wakufanya nipate aki yangu.
Kwani Sasa hivi mnaishi wapi na nyumba imeuzwa? Baba yako hajakupa hata cha udalali? Alikusomesha? Alisha Kupa mtaji? Kwenye urithi atakwambia subiri afe.Cha msingi ongea naye akikaza jaribu kuwashirikisha wazee wenzie.
 
unakaa hapo kwenu kama mfugo miaka 41 😀😀😀😀
 
nyumba ni yetu, maana nimezaliwa hapo hapo
Kwakuwa hukuchangia tofari wala bati hiyo nyumba ni ya baba yako.Una haki kupata share akikurithisha au kwa mujibu wa sheria Ila kwakuwa bado yuko hai,huwezi kumlazimisha.
 
Dah! Ukachoma zaidi ya 200k kufurahia pesa ambayo hauna uhakika nayo?

Sasa umpelekeka mzee mahakamani kwani unamdai kitu gani? Ingekua amefariki ungestahili mirathi.

Mie nilivyomaliza kidato cha sita nikaanza maisha sikuwahi kuomba hata kijiko kutoka kwa Mzee.

Usipobadili mtizamo kuhusu maisha, utalaumu watu sana mkuu
Yaani wewe mzee alikubeba sana mpaka unamaliza form 6.
Mie Mzee mpaka namaliza Form IV jukumu lake lilikuwa ni Ada tu...
Mavazi na vikorokoro vingine utajijua mweneywe...
Baada ya Form nilijua nitaaendelea na Elimu na nililima ekari 6 za mahindi nikavuna gunia 50. Hela ya kukodi shamba iliyotokana na kupiga picha maana nilifanyaga vibarua wakati wa likizo nikanunua camera YASHICA Gunia hizo ndio nikasoma Diploma ya Ufundi Umeme. Hapo ada plus pesa ya Field nikajisomesha mpaka namaliza. Tayari nimekuwa fundi unataka nini tena. Nimejiendeleza... yaani haya maisha sometimes ukiona Mzee anakukataa ndio anakupa akili.
 
Habari zenu ndugu zangu, naombeni ushauri wenu kwenye ili naamini uku jukwaani kuna wenye ushauri bora zaidi na wenye experince na mambo mbalimbali, mimi ni kijana wa umri wa miaka 41, kwetu tumezaliwa 4 ila kwa sasa tumebaki 3 baada ya mmoja bahati mbaya kufariki miaka 6 iliyo pita, mimi ni mtoto wa tatu kwenye familia.

Baba yangu alijenga DAR ES SALAAM miaka mingi iliyo pita, sasa mwezi uliopita 12/2021 alikuja na mtazamo wake na kutueleza sisi watoto wake kuwa anataka kuuza nyumba yake hii na aende akaamie kijijini na kuchagua maisha yake yote ataishi uko.

Upande wangu nilipokea ombi lake ilo kwa furaha sana maana niliona kabisa kuwa baba akiuza ntapata pesa na mimi ya kuanzia maisha, baada ya kusema ivyo nikaingia kwenye miangaiko ya kutafuta mteja na dalali ambaye atasaidia iyo nyumba iuzwe haraka, mungu si Athumani ndani ya week mbili tu akatokea mteja akiwa anaitaka iyo nyumba kwa sh milion 245 (maana nyumba ipo eneo zuri sana).

Dalali alimleta yule mteja na kuikagua nyumba nzima na eneo na uyo mteja aliahidi kuja kufanya malipo baada ya siku 3, uwezi amini nilifurahi sana sana nilikuwa na bajeti yangu ya laki 2 na elfu 70 kwa furaha nzima iyo ela niliitumia kwa kufurahia maana nilijua kabisa nimesha kula maisha. Baada ya siku 3 kweli yule mnunuzi alikuja na kufanya malipo na kukamilisha kila kitu,

Ndugu zangu nashindwa ata kuandika vizuri, baba baada ya kupokea pesa ataki ata kunishirikisha kwa chochote, hajanipa ata sent kumi yake kwenye iyo ela, baada ya siku mbili kupita mzee akiwa kimya ikabidi nimuambie baba vipi kuhusu ela ya mauzo ya nyumba unioni mwanao na mimi nikaangalie maisha yangu mbele ya safari, baba amenijibu tu kwa wepesi kabisa eti "SAWA NENDA KAANGALIE MAISHA TU, NAKUTAKIA KILA LENYE HERI" nikamuambia baba naendaje kuangalia maisha wakati ujanipa chochote, akaniambia kwani nadai nini kwake, kwa kweli ni kauli zilizo nivunja sana moyo na kunikatisha kabisa tamaa ya kuishi.

Noambeni ushauri wenu ili fate atua za kisheria mzee aweze kunipa na mimi upande wa maali kama mtoto wake wa kumzaa, maana nina week sasaivi sina furaha kabisa na aya maisha, naombeni sana ushauri wa haraka, maana baba siwezi kumtazama ata usoni ananipa sana hasira.

Matumaini yangu nitapata ushauri mzuri na wakufanya nipate aki yangu.
Hiyo nyumba baba yako alipewa na babu yako? Tafuta vya kwako na yeye Kaiza mali yake
 
KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI.

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?

4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli...

" Kama mnataka Mali mtaipata Shambani".
Kila la Heri Mkuu.

La Aquila non capit muscas!
Kitambo sana darasa la nne au tano kama sikosei
 
Back
Top Bottom