Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Mabro ni kusapotiana kwa kila hali kama hivi
Mi kupika ni hadi niwe na mood, nikiwa na mood kwakweli napika vitu vya kueleweka hata chapati inakua mashaalah ila nikiwa sijisikii chapati huwa natoa mkate wa yesu inavunjika kama kuni bro.
 
Wakuu,

Nilishawahi kuleta uzi wa kutojua kupika way back Mwanamke kutojua kupika inaweza kuwa sababu ya kupewa talaka?
Jioni hii nimepika wali...nauangalia hapa naona aibu mimi...wali una mafuta huoo

Nilianza kujua kupika lakini sjui nimesahau ama ni vipi lakini kila nikipika naharibu 🙌

Nisaidieni tips za kujua kupika vizuri...

Aaliyyah
Mwachiluwi
Sis Carleen

Bro Evelyn Salt nisaidie braza

Find a budget kidogo ya vitu, nunua, watch you tube and practice, kutokujua kupika sio shida, shida ni kufanya Kama ni tatizo sana la kuogopa; ila mwanamke lazima ajue kupika aisee!
 
Mkuu chakula sio wali Pelee


Kuna


Maboga
Viazi
Mihogo ya kuchemsha
Mayai

N.k

Bila kusahau kukata kata matunda..mume hawez kukuachia kisa wali
 
mwaya mdogo wangu mzuri Joanah,
Cooking is an art, ndiyo maana chakula hicho hicho kimoja watu wana mapishi mengi na tofauti balaa, hivyo lolote lile lisiku disappoint, hata kwa wanaojua kuna siku vyakula vinagoma kabisa..!!

Imagine, Jana kuna group moja wadada walikuwa wanasema huwa wanaanza kupika wali na maji baridi, yaani wanatia maji na mchele kwa pamoja na vinaiva vyema na kwa pamoja, tukabaki tunashangaa..!!

kupika ni baby steps, unajaribu -unakosea, kesho unatazama ni wapi ulikosea unarekebisha tena, ili usipate tabu, pika chakula kidogo ili pia isiwe hasara incase ukatoa muujiza..!!

Leo umekosea sababu umezidisha mafuta, jaribu kesho, punguza mafuta, punguza chumvi, na siku zote jitahidi pale mchele unapoishia kwenye sufuria maji yasipite sana, na wali wako ukichemka tu vizuri, punguza moto mpaka mwisho kabisa, yaani mpaka natamani nikupigie simu nikuelezee kwa sauti..!!

you're such a smart lady, kitu kama kupika hakiwezi kukushinda akili mdogo wangu, cha kuzingatia ni usichoke kujaribu wala usikate tamaa hata ukiharibu mara kadhaa..!!
 
Back
Top Bottom