Msaada daktari bingwa wa mishipa ya fahamu na ubongo MOI

Msaada daktari bingwa wa mishipa ya fahamu na ubongo MOI

Hahaha!

Sababu za vifo nasikia hazikutokana na uzembe wa huduma. Inasemekana wagonjwa waliokuwa wanapelekwa kule walikuwa hoi bin taaban hivyo madaktari walikuwa wanajitahidi kwa upande wao kuokoa maisha ya wagonjwa lakini inakuwa tofauti.

Na sababu ya kuwapeleka kule wanadai Muhimbili~Upanga kulikuwa hakuna nafasi kwasababu ya wagonjwa kuwa wengi.
 
Habar wakuu,nimefika dar kwa tatizo la mtoto wangu miaka9 anashida ya mgongo kunyooka,nilileta kwenu mpaka vipimo vya x-ray mkashairi Nifike moi hasa hasa nionane na daktar bingwa wa mishipa ya fahamu kwa uchunguzi
Sasa nimefika hapa naomba kuonana nahao nimekuwa directed kwa datar yoyote tu ,wameniandikia x ray Tena
Sasa wakuu naomba kwa anaefahamu daktar bingwa wa mishipa ya fahamu moi anitajie
Ulipofika hapo MOI ulijaribu kuonana na Mganga mkuu? Sikia, ni hivi......omba kuonana na huyo mganga mkuu haraka sana kwani hawa wengine watakuangusha tu makusudi ili tu uwape hongo.
 
PCMC Upanga, Kigamboni na Kimara. Tulipata huduma Kigamboni, maana tulikuwa tunaishi huko.
MRI ilifanyika BESTA Diagnostic Centre, Kinondoni na Nerve Conduction Studies (NCS) ilifanyika hapo hapo Kigamboni.
Tulitumia bima ya NHIF.
Mkapiga MRI kwa kutumia bima ya NHIF? Ni kifurushi gani cha hiyo bima yenu?Naomba kujua pia bima ya NHIF inatoaga huduma ya kumuona daktari bingwa na bingwa bobezi?
 
Comment nyingi zinaonesha namna gani sisi wa TZ ambavyo hatupendi kufuatilia mifumo ya sekta mbalimbali inavyofanya kazi.

Mkuu mwenye mtoto, MOI ndiyo wako vizuri zaidi kwenye mambo ya mifupa na mifumo ya fahamu, endapo tu shida ya mwanao itahitaji OPERATION.

Kama shida ni pingili za mgongo, basi nakushauri baki hapohapo MOI hakuna haja ya kwenda kwingine.

Kama shida ni mishipa ya fahamu ya ubongo, na ikawa haihitaji operation basi kuna uwezekano mkubwa wakakupa transfer ya Mloganzila.

Kikubwa ninachokishauri, achana na habari za kudankidanki kuulizia daktari huyu mara yule, utaamza kufanya wahudumu waanze kuwa na trust issue na ww na kukuona mwenye poor perception juu yao.

Wewe be calm, sikiliza wataalamu wote waliokupokea, kwa sababu kwenye matibabu lazima upite kwenye mikono ya kuanzia wa chini mpaka juu.

BE HUMBLE.
 
Mkapiga MRI kwa kutumia bima ya NHIF? Ni kifurushi gani cha hiyo bima yenu?Naomba kujua pia bima ya NHIF inatoaga huduma ya kumuona daktari bingwa na bingwa bobezi?
Mkuu, inaonekana hujasoma kwa utulivu post #59, nimeelezea kwa upana.

Ndiyo, tulipiga MRI kwa kutumia bima ya NHIF 2019, si kwa vifurushi vya NHIF 2024.

Huyo daktari bingwa sikumuona kupitia MOI, bali moja ya hospitali zake binafsi.
 
Ooh, SAWa SAWa,

Umemjibu vyema sana sana.Umekua na mawazo kama niliyokua nayo.Hiyo shida ya mtoto wake inahitaji Dr wa mifupa tu.Inaonekana yupo busy kutafuta uhakika jamii forum kuliko kuamini wanaomuona mgonjwa.Atulie hapo hapo wataalam wanajua aache mambo ya kuuliza uliza huku haitamsaidia
 
Back
Top Bottom