Msaada: Dojo kwa hapa Dar es Salaam

Umefanya nicheke eti "dojo yako inaishia hapo"....
 
hao wanajeshi anawafundisha nini? au anawafundisha privately?
 
Mtafute sensei Taifa liwewa au Ngonyani.
 

Lege mkuu vipi upo dunia hii hii.
 
Habari wana JF
Nakaa Ubungo golani...kwa anayejua naomba anipe location ya dojo la karate mitaa ya uku nimpeleke mtoto wangu,seven Yrs Old.
 
Habari wana JF
Nakaa Ubungo golani...kwa anayejua naomba anipe location ya dojo la karate mitaa ya uku nimpeleke mtoto wangu,seven Yrs Old.
Shule ya ubungo islamic kuna mwalimu wa karate tena qualified na ni mjumbe wa TASHOKA =Tanzania shotokan association

Huyu amewatoa sana vijana ktk mashindano ya kimataifa ,huwa ana dojo lake kiwalani na hapo shuleni kila siku na outsiders anafundisha hapohapo
 
Ubungo sehemu gani? Nisaidie
 
uncle ben, uko sahihi kuwa jeshini kareti inafundishwa tena na masensei walioiva vizuri kabisa, huyo mnaebishana nae anataka kuiweka kareti anayoifundisha huyo Chikoko as if ni kitu special mno ambacho wengi hawawezi, kwa taarifa tu ni kwamba jeshini kuna wataalam wa martial arts waliobobea sana, baadhi tu ya martial arts zinazofundishwa jeshini ni kama Kareti ( kwa mifumo yote) Tae kwon Do, Judo ( kombati), Krav maga, n.k, kwa hiyo asikudanganye eti huyo Chikoko anawafundisha wanajeshi as if jeshini hatuna masensei, pia aelewe kareti ya jeshini sio ya kupoteza miaka unahangaika na kata za kijinga zisizo na faida, jeshini unasukwa na kuiva tayari kwa lolote kwa mwaka mmoja tu.

Pia ajue tu kwamba tuna vikosi vilivyobobea kwa martial arts vikiongozwa na Sangasanga( 92kj) Ngerengere- Moro, kwa hiyo kama huyo chikoko anawafundisha wanajeshi labda ni kwenye dojo lake na sio kuletwa kikosini eti atoe martial art training kwa wanajeshi, hiyo haipo.
 
Achana na Karate... Cheza wing chun au drunken gods.
 
Kuna sensei mmoja alikua anafundisha maeneo ya mbagala kma unaenda kongowe karibu na shule ya st.mary opposite na sheli sijui kama mpka sasiv bado yupo maana nilipiga mazoez pale kitambo sana miaka ya 2007
 
Scorpion ni mwalim mzuri yuko segerea, nadhani atakufundisha bure maana hana garama, anakula bure na kulala bure
 
Mungu wangu watu wa dar mnataka mzidi kuzalisha mascopion sio?
 

Mimi napata tatizo sana hapo mtu anapodai sensei Chikoko ndio best kuliko wote. Labda aseme best kwenye Shotokan
ambayo ni competitive karate kama ambavyo Tae kwon do ilivyo competitive martial arts. kuna mifumo mingine
ya karate ambayo ni kwa ajili ya mapambano tu (combative) ambayo huikuti Olympics wala sehemu nyingine
ambazo ni za mashindano. Ukiikuta huko basi waashiriki wanashindana performance ya "kata" na wala si
mapambano. Mifumo hii inajumuisha Goju ryu na Kyokushin. Sasa Sensei Chikoko alipambanishwa na washiriki/wakufunzi wa hiyo mifumo ya aina hiyoTanzania? Maana wapo ila wamebana kimya tu.
 
yaani tatizo jamaa amegeneralize sana, haiwezekani Tanzania nzima yeye ndo awe best tena kwa maoni ( opinions)ya mtu mmoja tu, labda kungelikuwa na shindano la nchi nzima aliloshiriki na kuibuka mshindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…