uncle ben, uko sahihi kuwa jeshini kareti inafundishwa tena na masensei walioiva vizuri kabisa, huyo mnaebishana nae anataka kuiweka kareti anayoifundisha huyo Chikoko as if ni kitu special mno ambacho wengi hawawezi, kwa taarifa tu ni kwamba jeshini kuna wataalam wa martial arts waliobobea sana, baadhi tu ya martial arts zinazofundishwa jeshini ni kama Kareti ( kwa mifumo yote) Tae kwon Do, Judo ( kombati), Krav maga, n.k, kwa hiyo asikudanganye eti huyo Chikoko anawafundisha wanajeshi as if jeshini hatuna masensei, pia aelewe kareti ya jeshini sio ya kupoteza miaka unahangaika na kata za kijinga zisizo na faida, jeshini unasukwa na kuiva tayari kwa lolote kwa mwaka mmoja tu.
Pia ajue tu kwamba tuna vikosi vilivyobobea kwa martial arts vikiongozwa na Sangasanga( 92kj) Ngerengere- Moro, kwa hiyo kama huyo chikoko anawafundisha wanajeshi labda ni kwenye dojo lake na sio kuletwa kikosini eti atoe martial art training kwa wanajeshi, hiyo haipo.