Msaada: Dojo kwa hapa Dar es Salaam

Msaada: Dojo kwa hapa Dar es Salaam

Donlucchese

Sijui una umri gani. Ila naona kwa sasa maisha yamebadilika sana. Miaka ya nyuma nikiwa kijana kijana nilianza kujifunza AEKIDO. Alikuwa anafundisha mke wake mcheza sinema maarufu marekani Steven Seagal. Steven Seagal mwenyewe kabla ya kuachana na mke wake hilo ndo lilikuwa chimbo lake.

Baada ya kuanza mafunzo nilipata shida sana. Japo kijana lakini umri ulikuwa sio flexible kuendana na vijana wengine. Nilipata shida sana. Wakati mi ndo najifunza madogo wengine walikuwa kwenye mazoezi ya majambia yaani swords. Wenzetu mazoezi wanaanza tangu miaka mitatu.

Nataka kusema nini.

Kama wewe bado umri haujaenda ni vizuri ukaanza. Ila kama umri umeenda kama Mimi kikubwa ni kujiweka fit na hasa kuwa na pumzi. Hata kama unakimbizwa unawanyanyasa tu.

Lakini pia kama unataka kujifunza karate basi jifunze weak points kwenye mwili. Kuna maeneno matano au sita kwenye mwili ambayo kama huna jinsi unaweza kupiga na ukamwondoa mtu. Lakini hii ni kama huna jinsi nyingine. Kwa sababu unaweza ukapiga mtu akadondoka kesi ikarudi kwako.

Kingine siku hizi watu wengi wanataka kuwa fit kimazoezi na kuzuia magonjwa. Bastola zimefanya watu wawe wazembe sana. Na mwenzio akiwa nayo hata kama hajawahi kwenda gym akikuwahi tu dojo yako inaishia hapo.

Sikukatishi tamaa ila wewe ndo mwamuzi.
Umefanya nicheke eti "dojo yako inaishia hapo"....
 
sio jazba wala usielewe vibaya, nenda jeshini kaangalie utanipa jibu sio makomando wala wanajeshi wa kawaida "karate" haifundishwi jeshini, jeshini wanafundishwa kupigana kuvunja vitu kuwa sugu na kadhalika sio karate/karatedo yeye ni mwalimu ambae ameshawahi na bado anafundisha wanajeshi. kwa hiyo ninachokuambia sio mbwembwe. kujua kupiga na kujua ufanyaji wa karate ni vitu viwili tofauti na havina uhusiano
hao wanajeshi anawafundisha nini? au anawafundisha privately?
 
mkuu ww unapatikana wapi?
kama huta jali umbali kuna chikoko huyu ndiye nazani anayeongoza hapa tanzania ana dani 1 ya SHOTOKAN ila sasa yy anapatikana KAWE na ndipo dojo lake lilipo anapatikana TANGANYIKA PEKERS kama vipi wapo wengine kama steve bella mshindi wa kata za shotokan tanzania mara 3 mfululizo yy ana black belt wapo wa kina dulla n.k kama utahitaji unaweza nicheki hapa 0717 228064

Lege mkuu vipi upo dunia hii hii.
 
Habari wana JF
Nakaa Ubungo golani...kwa anayejua naomba anipe location ya dojo la karate mitaa ya uku nimpeleke mtoto wangu,seven Yrs Old.
 
Habari wana JF
Nakaa Ubungo golani...kwa anayejua naomba anipe location ya dojo la karate mitaa ya uku nimpeleke mtoto wangu,seven Yrs Old.
Shule ya ubungo islamic kuna mwalimu wa karate tena qualified na ni mjumbe wa TASHOKA =Tanzania shotokan association

Huyu amewatoa sana vijana ktk mashindano ya kimataifa ,huwa ana dojo lake kiwalani na hapo shuleni kila siku na outsiders anafundisha hapohapo
 
Ubungo sehemu gani? Nisaidie
 
Mkuu karate haifundishwi Jeshini ??
Anyway ngoja tu nikubaliane kutokukubaliana ,sawa uwe na jioni njema
Wala sijasema kujua kupiga na ufanyaji wa karate ni kitu kimoja ,ndio maana tuna Kung fu ,Karate,Kick box,gujuru nk ,zote ni mapigo ila kila moja ina sanaa zake
uncle ben, uko sahihi kuwa jeshini kareti inafundishwa tena na masensei walioiva vizuri kabisa, huyo mnaebishana nae anataka kuiweka kareti anayoifundisha huyo Chikoko as if ni kitu special mno ambacho wengi hawawezi, kwa taarifa tu ni kwamba jeshini kuna wataalam wa martial arts waliobobea sana, baadhi tu ya martial arts zinazofundishwa jeshini ni kama Kareti ( kwa mifumo yote) Tae kwon Do, Judo ( kombati), Krav maga, n.k, kwa hiyo asikudanganye eti huyo Chikoko anawafundisha wanajeshi as if jeshini hatuna masensei, pia aelewe kareti ya jeshini sio ya kupoteza miaka unahangaika na kata za kijinga zisizo na faida, jeshini unasukwa na kuiva tayari kwa lolote kwa mwaka mmoja tu.

Pia ajue tu kwamba tuna vikosi vilivyobobea kwa martial arts vikiongozwa na Sangasanga( 92kj) Ngerengere- Moro, kwa hiyo kama huyo chikoko anawafundisha wanajeshi labda ni kwenye dojo lake na sio kuletwa kikosini eti atoe martial art training kwa wanajeshi, hiyo haipo.
 
Kuna sensei mmoja alikua anafundisha maeneo ya mbagala kma unaenda kongowe karibu na shule ya st.mary opposite na sheli sijui kama mpka sasiv bado yupo maana nilipiga mazoez pale kitambo sana miaka ya 2007
 
Salaam wakuu,
mimi ni mpenzi sana wa sanaa za mapigano na nilijiunga na Sensei Ringo pale TASHOKA (Tanzania Shotokan Karate) Russian culture centre ila nilijikuta na drop kutokana na gharama na pia kuona mikanda inatolewa kimaghumashi, kwa kifupi unaweza kukuta mtoto mhindi mdogo tu ana mkanda wa maana wakati hata mkijaribu kufanya sparring unampa mawashi moja mtoto anaanza kutapika visheti (no joke). kwa wakuu wale wataalam wa martial arts naomba mnirecommend dojo ambalo wanatoa mafunzo vizuri ya maana na kwa gharama nafuu niweze kujiunga mapema mwenzi december. Natanguliza shukrani za dhati!
Scorpion ni mwalim mzuri yuko segerea, nadhani atakufundisha bure maana hana garama, anakula bure na kulala bure
 
uncle ben, uko sahihi kuwa jeshini kareti inafundishwa tena na masensei walioiva vizuri kabisa, huyo mnaebishana nae anataka kuiweka kareti anayoifundisha huyo Chikoko as if ni kitu special mno ambacho wengi hawawezi, kwa taarifa tu ni kwamba jeshini kuna wataalam wa martial arts waliobobea sana, baadhi tu ya martial arts zinazofundishwa jeshini ni kama Kareti ( kwa mifumo yote) Tae kwon Do, Judo ( kombati), Krav maga, n.k, kwa hiyo asikudanganye eti huyo Chikoko anawafundisha wanajeshi as if jeshini hatuna masensei, pia aelewe kareti ya jeshini sio ya kupoteza miaka unahangaika na kata za kijinga zisizo na faida, jeshini unasukwa na kuiva tayari kwa lolote kwa mwaka mmoja tu.

Pia ajue tu kwamba tuna vikosi vilivyobobea kwa martial arts vikiongozwa na Sangasanga( 92kj) Ngerengere- Moro, kwa hiyo kama huyo chikoko anawafundisha wanajeshi labda ni kwenye dojo lake na sio kuletwa kikosini eti atoe martial art training kwa wanajeshi, hiyo haipo.

Mimi napata tatizo sana hapo mtu anapodai sensei Chikoko ndio best kuliko wote. Labda aseme best kwenye Shotokan
ambayo ni competitive karate kama ambavyo Tae kwon do ilivyo competitive martial arts. kuna mifumo mingine
ya karate ambayo ni kwa ajili ya mapambano tu (combative) ambayo huikuti Olympics wala sehemu nyingine
ambazo ni za mashindano. Ukiikuta huko basi waashiriki wanashindana performance ya "kata" na wala si
mapambano. Mifumo hii inajumuisha Goju ryu na Kyokushin. Sasa Sensei Chikoko alipambanishwa na washiriki/wakufunzi wa hiyo mifumo ya aina hiyoTanzania? Maana wapo ila wamebana kimya tu.
 
yaani tatizo jamaa amegeneralize sana, haiwezekani Tanzania nzima yeye ndo awe best tena kwa maoni ( opinions)ya mtu mmoja tu, labda kungelikuwa na shindano la nchi nzima aliloshiriki na kuibuka mshindi.
 
Back
Top Bottom