Msaada: Gari hii ya milioni 9 inafaa? Nipeni uzoefu nisije nikapigwa

Msaada: Gari hii ya milioni 9 inafaa? Nipeni uzoefu nisije nikapigwa

Kwa muonekano wa hiyo gari, bei halali inatakiwa icheze kati ya milioni 5-6. Ni gari nzuri inayoweza kuhimili barabara zote (lami na vumbi).

Ila mmiliki pia kajitahidi sana kuitunza. Ni aghalabu kukutana na Toyota Corona zenye usajili wa C na D. Nyingi zilizobakia ni za usajili wa A na B.
 
 
Nataka kununua hii gari jamaa kaniambia milioni 9. Alianza na 11 tukashuka hadi 9, je, hiyo bei ni sawa kulingana na hali ya gari ilivyo?

Naomba saada wakuu.

View attachment 2719570
Mpe Mil 7 Mkuu. Kwa sasa Dolla imepanda hadi 2600 kutoka 2300 hivyo magari yamepanda bei sana. Usisikilize maneno ya wasio na uzoefu kwenye hiyo field
 
Back
Top Bottom