Msaada kuhusu kusafirisha parcel kutoka Marekani

Naomba kusaidiwa na yeyote humu ambaye ni mzoefu wa kusafirisha percel kutoka Marekani kuja Tanzania ,KWA kutumia makampuni kama DHL na mengineyo hasa napenda kufahamu gharama za kusafirisha simu, ziko mbili kutoka Ohio Cleaveland kuja Tanzania

Upo bongo au upo Cavs?

Kama upo Cavs nenda ofisi ya karibu ya Fedex utapewa utaratibu...
 
Mbona kuna WaTz wengi tu kila siku wanasafiri kati ya nchi hizi. Huyo mtu wako hajuani na WaTz huko wakakubebea?
 
Tumia EMS service ya USPS.
Huwa natuma simu 10 kwenye box dogo, nazungusha tape box zima.
Kwenye customs declaration form naandika solar calculators au solar chargers.
Pia naandika USB type C wire chargers (kwa sababu zitascan wataona wires).
Utajaza mji na Telephone #. Zikifika baada ya 3-5 days watampigia simu.
Simu 10 average natumia 100$.
Zikifika Dar watachaji customs. but basically EMS ya USPS is the best option.
Kutuma simu 2 ni hasara inaweza ikawa hiyohiyo 100$.
 
Waone Silent ocean
 
Ok.
Waone Silent ocean
Wanasafirisha kutoka US to Bongo?
Shukrani mkuu.
Usitumie Fedex, Tz hakuna Fedex Agent, kuna makanjanja
ok.
 
Mbona kuna WaTz wengi tu kila siku wanasafiri kati ya nchi hizi. Huyo mtu wako hajuani na WaTz huko wakakubebea?
WaTz Hakuna wa kuwaagiza.
 
Mzigo hutumwa kwa uzito. Ukipokea jua kabisa watakutoza kodi. Tumia EMS na uandae hela ya kutosha ya kodi. Siku hizi kodi ni kubwa zimeongezeka. .

DHL wasumbufu achana nao kabisa hawachelewi kukuimba document za ofisi mara invoice. Tumia EMS wewe utalipia na kubeba mzigo wako. .
 
Usitumie Fedex, Tz hakuna Fedex Agent, kuna makanjanja
Hehehe natumia FedEx mara nyingi sana na mostly mzigo wangu napata ndani ya siku 8, na delay inakuwa dar otherwise ingekuwa mapema zaidi. Anyway, labda ni upande wangu ila sijawahi kupata shida na FedEx neither DHL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…