Msaada kuhusu mbegu za nyanya

Kwahiyo mkuu hizi nyanya fupi hutushauri kuto kuzipunguza matawi
 
Asante vip kwa uzoefu wako mwezi gani nioteshe kitalu ambacho ntakuja kuvuna mwezi gani ambao nyanya huwa dili
Kilimo sio rahisi hivyo ndugu ,kila mtu kwa kufuata tu tarehe apate hela ,kikubwa tafuta soko kwanza kisha utazalisha kulingana na huko utakako uza wewe ,hapo kujipa utofauti na wengine ,soko ndilo la kumaanisha faida au hasara
 
Naomba usaidie hivi kwenye udongo wa kichanga kabisa...kama ule wa baharini...nikijitahidi nikapata samadi nyingi naweza kupata mazao mazuri...maji yapo 24/7
 
Naomba usaidie hivi kwenye udongo wa kichanga kabisa...kama ule wa baharini...nikijitahidi nikapata samadi nyingi naweza kupata mazao mazuri...maji yapo 24/7
Kama unaweza pata samadi kiasi cha ndoo moja kwa sqm 1 yaani unapana mita 1 na urefu mita 1 inatosha kabisa kukupa mazao bora pia kuupa udongo wako uwezo wa kutunza maji ,kama huwezi pata samadi kiasi hiko basi weka kiasi ulichonacho na utumie na mbolea za kiwandani
 
Asante...ila kaka kwenye hii bustani yangu baadhi ya vitumba vinavyoleta maua kimoja kina kauka...siju tatizo ninini hapo
 
Asante...ila kaka kwenye hii bustani yangu baadhi ya vitumba vinavyoleta maua kimoja kina kauka...siju tatizo ninini hapo
Unaweza tuma picha inaweza kua ukosefu wa madini hususani ya calcium ,maji machache ,wadudu (thrips) au ukungu picha kidogo itanipa mwanga ila je umeweka can? Unanyesha vyema? Umepiga dawa gani ya wadudu !? Umepiga dawa za ukungu zenye kiuatilifu cha azoxystrobin/difenoconazole/propamocarb etc yaani tofauti na mancozeb na metalaxyl ?
 
Hizo ndio dawa pekee nilizo piga

Maji huwa namwagia mara mbili kwa siku...ila nilisimama kwa siku kadhaa kutona na mvua zinazonyesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…