Msaada: Kuondoa utelezi maji ya mvua

Msaada: Kuondoa utelezi maji ya mvua

Anga halipo clossed if that is the case. Nadhani Uneona povu lililoenda kuangukia Useriver Arusha wakati sabuni ilimwagikia morogoro.
Mkuu kwa mujibu wa wanamazingira wanasema anga likishajaa mahewa ya sumu ni rahisi mvua yenye kemikali hatari ikanyesha.

Kikubwa tutunze mazingira
 
kwangu nahifadhi lita 47,000 elfu za maji ya mvua na hayana utelezi na hakuna dawa imewekwa mwaka pili

ishu kubwa zuia mwanga wa jua usipenye

hata kama ni jaba hakikisha unafunika vizur kuzuia hewa na mwanga kuingia

asante
 
Kule vijijini au maeneo yenye kuzingirwa na miti mingi hatari hupungua kwa sababu miti husaidia kusafisha hewa.... lakini kwa mfano mtu anaishi jirani na kiwanda cha wazo cement, halafu kuna wakati kiwanda kinawasha mtambo wa zamani kukamua saruji kisha mvua inanyesha na jamaa wanakinga maji ya mvua..... kuna hatari hapo
 
kwangu nahifadhi lita 47,000 elfu za maji ya mvua na hayana utelezi na hakuna dawa imewekwa mwaka pili

ishu kubwa zuia mwanga wa jua usipenye

hata kama ni jaba hakikisha unafunika vizur kuzuia hewa na mwanga kuingia

asante
Habari mkuu.
Unaposema mwanga na hewa isiingie huoni si sahii? Je tank linapumulia wapi? Maana linapojaa bila kuruhusu yamwagike lazima utasababisha tank kupasuka.
Tundu kidogo kwa ajili ya overflow ni muhimu. Muhimu ni kutoacha sehemu kubwa kwa ajili ya mwanga na hewa.
Ila usiseme mwanga na hewa visiingie.

Asante.
 
Nyie ndo wabishi msiokuwa na facts
Soma hapo
Screenshot_20240123-081157_Chrome.jpg
 
Utelezi hautoki! Mimi nimetia chumvi kuzuia yasioze kuweka wadudu

Asubuhi nimefungua bomba bado limenuna....
Mnaishi maeneo Gani nyie mbona mnateseka sana? Huku maji tunayaacha tu yanamwagika tu
 
Wakuu, kutokana na maji ya bomba ya dawasa kutoka kwa muda wa lisaa limoja tu kwa kila miezi 3, nimeona nihifadhi maji ya mvua

Tatizo yana utelezi fulani mwilini mimi napooga, je njia rahisi ya kuondoa huo utelezi ni ipi? Msaada tafadhali.
Mambo Agano,
Njia rahisi ya kuzuia wadudu na kuoza kwa maji ni kutumia chumvi au water guard.

Pia kuna njia mbili ambazo huwa natumia.
1. Shabu - hii ni kama chumvi ya mawe inasaidia kufanya maji yadumu muda mrefu sana na pia kuyasafisha. Uwekapo hii hata ule uchafu wote ushuka chini kabsa ya tank na maji kubaki meupe pee. Hii hupatikana misikitini au kariakoo wanaouza dawa za asili.
2. Chukua waya/kipande cha aluminium pure/asili kiweke kwenye tank kitazama chini. Kiache humo miaka na miaka hakuna maji kuoza. Kinafanyaje kazi sijui ila ndio njia nitumiazo kwa miaka kadhaa sasa. Uzuri upate ule waya wa aluminium mgumu ukunje kipande hata cha cm 30 dumbukiza.

Karibu.
 
Kwann uweke chumvi. Yalivyo hivyo laini ni bora zaidi
Mkuu hayo maji anayosema jamaa ni kwamba yameharibika , yana wadudu. Mwambie ukweli usijikite tu kwenye maji kuwa sijui kuwa magumu au laini. Maji ya mvua bila kuwa treated yanaharibika haraka sana mkuu.
 
Mkuu hayo maji anayosema jamaa ni kwamba yameharibika , yana wadudu. Mwambie ukweli usijikite tu kwenye maji kuwa sijui kuwa magumu au laini. Maji ya mvua bila kuwa treated yanaharibika haraka sana mkuu.
Hapana, amesema maji ya mvua, it means fresh hajasema maji ya mvua aliyohifadhi kwa muda mrefu
 
Maji laini na maji magumu huwa yana sabuni tofauti kidogo zilizo wekewa kemikali zinazofaa kwa hali ya maji katika jimbo. Nadhani hapa kwetu hii haipo
 
Back
Top Bottom