Hizi estimates kwa kweli huwa zinatuchanganya wengi wetu nadhani. Maana nimeshauliza swali kama hili la kujenga nyumba ya vyumba vitatu kwa baadhi ya jamaa na marafiki, ila quotations nazopata zina range kwenye million 50 mpaka million 100, kutokana na finishing. Hii ni mpaka kuhamia - na ni kwa ujenzi wa mpakani mwa Dar na Bagamoyo. Sasa naona huku majibu mengi wanasema unaweza jenga kwa millioni 26 nyumba ya 2 bedrooms kwa Dar au Pwani na hukamia kabisa. Very confusing. Inakuwa ngumu mtu kujipanga. Maana unaweza kujipanga kwa Million 30 ukajua itatosha, kumbe bado kabisa, au ikatosha na chenji kubaki. Waliojenga for real, nyumba zenu zimewagharimu kiasi gani mpaka kuhamia? 3-bedroms, at least one master suite, spacious living and dining rooms. Jikoni na stoo ya jikoni. Na baraza nje mlando wa mbele. Nitawashakuru kwa ushauri wa uhakika. Maana wengine ndiyo tunajipanga. Nina 38 million tayari