Leseni ya kununua na kuuza inaitwa Broker licence unaanzia halmashauri unachukua fomu ya leseni unajaza unaenda nayo TRA wanakukadiria kodi unalipia robo wanakupa tin na tax clearance certificate unatoa copy na kitambulisho na passort picha 3 unaenda madini unaomba form ya kuomba broker licence unapewa akaunti ukalipie 250,000/= naada ya kupeleka deposit slip unawapa siku moja unapewa fasta. auina ya madini unaandika yoyote usiandike dini maalumu mfano unataka tanzanite andika all gemstones ,unataka dhahabu weka all precious metals ,the wellcome to the business
Fomu ya halmashauri hii hapa
http://barakaconsult.com/uploads/LESENI_YA_BIASHARA_en.pdf
NB: Kama unataka ya kuchimba kwa sasa zimesitishwa hadi itapoundwa tume ,usiskize maneno ya watu serikali iko so sapportive kwenye hii biashara ilimradi ufuate sheria tu na uwe na maarifa ya kutosha juu ya madini uliyoamua kufanyia kazi ,kama unaswali lolote usinifate inbox ulizia hapa hapa wafaidike vijana wengi.