Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana kwa michango yenu kuna mtu ametaja Rosemary nimeutafuta huu mmea kumbe ni so common na inaota vizuri tu karibia kila mkoa nitaujaribu. Nadhani kikubwa ni usafi pia maana ukipunguza vichaka basi na nyoka watakimbia.
kuna mtu kataja mimea inayosaidia kufukuza ukiwemo huo sasa sijui unatumiwaje au kuupanda tu ni dawa sijajua. Hizi ni aina Fulani za maua zinanukia mfano wengine wanatumia kama fencing kama umeishapita jengo next to Merrywater pale makumbusho. Wametaja zina maua ya pink, white na puple ingawa common ni pink na ina harufu nzuri sana tofauti na Roses zenyewe hazina miba na zina majani marefu. Ninaweka picha yake amesema unaupanda kama wigoUnafukuza nyoka huo mti?
Hatua ya muda mfupi ni kunyunyizia diesel (au mafuta ya taa) kuzunguka eneo lako. Unaweza kutumia sprayer kama hii hapa chini kwenye picha kunyunyizia diesel hiyo kuzunguka eneo lako. Harufu ya diesel inawakera sana nyoka na wataenda mbali. Ila itabidi urudie ku-spray kama mvua itanyesha, maana maji ya mvua yakapunguza harufu ya diesel.
Tumia Oil chafu unaweza kuipata bure au kwa bei ndogo sana, nyunyiza kuzunguka shamba lako ila kikubwa usafi wa shamba ni muhimu sana, shamba likiwa safi nyoka wote watahama na pia fuga kuku wa kienyeji na uwaache wajitafutie chakula nje.
Mwaga mafuta ya taa, dizel au oil chafu kuzunguka shamba. Aidha, choma matairi au mipira katika vichaka husika.
solution ni ...mwaga oil tena chafu kuzunguka shamba lote alieko ndani hatoki na alieko nje haiingii tena.. hakika utanikubali mkuu sikuamini lakini mi nimemaliza tatizo nineuwa mmoja mmoja waliokuwa ndani na sasa hali ni safi...
Huu ushauri siyo mzuri kabisa kwa sababu unaharibu mazingira.
Kusema tu ushauri kuwa ushauri huu unaharibu mazingira bila kutoa option ilihali mwenzio ana shida haina maana ni sawa na kusoma na kuacha.
Unataka nitoe opinion kuhusu oil chafu?
Hujui maana ya oil chafu mpaka kutaka opinion?
Sidhani kama Watanzania tumekuwa vilaza hivyo mpaka kata opinion kama oil chafu inafaa kwa matumizi.
Usimshauri tu kuwa hii ni sumu usile, mwambie hii ni sumu kwa hiyo kula maandazi...tehe tehe tehe!
Unataka nitoe opinion kuhusu oil chafu?
Hujui maana ya oil chafu mpaka kutaka opinion?
Sidhani kama Watanzania tumekuwa vilaza hivyo mpaka kata opinion kama oil chafu inafaa kwa matumizi.
Usimshauri tu kuwa hii ni sumu usile, mwambie hii ni sumu kwa hiyo kula maandazi...tehe tehe tehe!
![]()
Mamba wapo wa rangi nyingi kutofautiana kadiri ya mazingira wanayoishi. Huyu ni deadly, na ndio nyoka anauma kwa kukusudia na kupanga kabisa kufanya ubaya.
![]()
Huyu Green Mamba ni hatari zaidi ya Black Mamba, uzuri ni kwamba huishi kwenye misitu mikubwa na amwe hakai karibu na mazingira yenye binadamu. Huyu ni tofauti na hawa nyoka wa kijani wanaokaa kwenye miti hata majumbani, huyu ni mkubwa na anaruka mti mmoja hadi mwingine kwa namna ya ajabu. Black Mamba haishi kwenye miti, yeye hupendelea vichuguu kama Cobra