Msaada: Mbinu Kufukuza Nyoka mashambani

Msaada: Mbinu Kufukuza Nyoka mashambani

Asante sana kwa michango yenu kuna mtu ametaja Rosemary nimeutafuta huu mmea kumbe ni so common na inaota vizuri tu karibia kila mkoa nitaujaribu. Nadhani kikubwa ni usafi pia maana ukipunguza vichaka basi na nyoka watakimbia.
 
Choma matairi au bidhaa za mpira shambani
 
Asante sana kwa michango yenu kuna mtu ametaja Rosemary nimeutafuta huu mmea kumbe ni so common na inaota vizuri tu karibia kila mkoa nitaujaribu. Nadhani kikubwa ni usafi pia maana ukipunguza vichaka basi na nyoka watakimbia.

Unafukuza nyoka huo mti?
 
Mutensa na Mama Joe pia unaweza kutafuta waya wa shaba (Cooper) ukazungushia shamba lako au banda lako katika level ya chini hakuna nyoka atakayethubutu kuvuka waya huo.
 
Last edited by a moderator:
Unafukuza nyoka huo mti?
kuna mtu kataja mimea inayosaidia kufukuza ukiwemo huo sasa sijui unatumiwaje au kuupanda tu ni dawa sijajua. Hizi ni aina Fulani za maua zinanukia mfano wengine wanatumia kama fencing kama umeishapita jengo next to Merrywater pale makumbusho. Wametaja zina maua ya pink, white na puple ingawa common ni pink na ina harufu nzuri sana tofauti na Roses zenyewe hazina miba na zina majani marefu. Ninaweka picha yake amesema unaupanda kama wigo
 

Attachments

  • 550px-Identify-Rosemary-Step-9.jpg
    550px-Identify-Rosemary-Step-9.jpg
    30.4 KB · Views: 238
Hatua ya muda mfupi ni kunyunyizia diesel (au mafuta ya taa) kuzunguka eneo lako. Unaweza kutumia sprayer kama hii hapa chini kwenye picha kunyunyizia diesel hiyo kuzunguka eneo lako. Harufu ya diesel inawakera sana nyoka na wataenda mbali. Ila itabidi urudie ku-spray kama mvua itanyesha, maana maji ya mvua yakapunguza harufu ya diesel.

Tumia Oil chafu unaweza kuipata bure au kwa bei ndogo sana, nyunyiza kuzunguka shamba lako ila kikubwa usafi wa shamba ni muhimu sana, shamba likiwa safi nyoka wote watahama na pia fuga kuku wa kienyeji na uwaache wajitafutie chakula nje.

Mwaga mafuta ya taa, dizel au oil chafu kuzunguka shamba. Aidha, choma matairi au mipira katika vichaka husika.

solution ni ...mwaga oil tena chafu kuzunguka shamba lote alieko ndani hatoki na alieko nje haiingii tena.. hakika utanikubali mkuu sikuamini lakini mi nimemaliza tatizo nineuwa mmoja mmoja waliokuwa ndani na sasa hali ni safi...

Huu ushauri siyo mzuri kabisa kwa sababu unaharibu mazingira.
 
Mkuu name nilikuwa na nyoka sana shambani maana majirani wananunua ardhi for over ten years hawafanyi chochote wala kusafisha. Kulikuwa na kila aina ya nyoka isipokuwa black mamba ila kuna mmoja kulingana na wataalam wa nyoka alikuwa ni hatari sana na alikuwa mkubwa mno. Nilikusanya matairi na kuachoma kwa wingi sana na ninaamini alihama (alikuwa na shimo lake mpakani na jirani yangu). Hatujaona tena fujo zake maana alikuwa anafika hadi nyumbani vijana wanasikia akipita usiku na ukiamka unakutana na michirizi yake. Ilikuwa inanifadhaisha sana hasa pale mtaalam toka tabora alipotuhakishia kuwa ni nyoka wa sumu sana wanaita koboko/ngoboko (sijui ndilo jina lake vizuri, siwapendi nyoka na sitaki kuwajua hasa, japo black na green mamba nililazimika kuwafahamu maana ni hatari sana). Hivyo jaribu oil chafu kidogo tu pembeni mwa shamba, choma matairi, na panda mchaichai kama walivyokushauri. Ila kuna member amesema fuga kuku wa kienyeji sasa sijajua wanafukuzaje nyoka hasa wale wanaopambana kama black mamba.
 
Kamata kula, ni kitoweo kuzuri sana hicho
 
Kuna aina mimie ambayo ni jamii ya mkonge ila ina vi miiba vidogo vidogo sana na inastahimili sana ukame, ukiitoshe kama fance kuzunguka shamba lako au hata nyumba yako ina provide ulinzi wa kufa mtu kwa sababu hakuna aina ya kiumbe anaye weza kupenya au kuishi kwenye huo mmea, labda apae juu, Iko Karatu kwa wingi ingawa watu huwa wanaingamiza sana, ina miiba ya kipekee na yenye sumu, nitawawekea picha zake siku si nyingi
 
Waweza tumia mkaa mdogo wa moto kwenye chetezo au kifaa chochote na kuweka samli na mchanganyiko wa pilipili.

Ila hakikisha uelekeo wa upepo unaenda kwenye vichaka husika.Wingi wa mkaa wa moto,samli na pilipili utategemea ukubwa wa kichaka.

Tahadhali; Weza jiko /kifaa cha moto mbali kidogo kama 1.0-1.3m kutoka kichaka kilipo.
 
Kusema tu ushauri kuwa ushauri huu unaharibu mazingira bila kutoa option ilihali mwenzio ana shida haina maana ni sawa na kusoma na kuacha.

Unataka nitoe opinion kuhusu oil chafu?

Hujui maana ya oil chafu mpaka kutaka opinion?

Sidhani kama Watanzania tumekuwa vilaza hivyo mpaka kata opinion kama oil chafu inafaa kwa matumizi.
 
Unataka nitoe opinion kuhusu oil chafu?

Hujui maana ya oil chafu mpaka kutaka opinion?

Sidhani kama Watanzania tumekuwa vilaza hivyo mpaka kata opinion kama oil chafu inafaa kwa matumizi.

Usimshauri tu kuwa hii ni sumu usile, mwambie hii ni sumu kwa hiyo kula maandazi...tehe tehe tehe!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Usimshauri tu kuwa hii ni sumu usile, mwambie hii ni sumu kwa hiyo kula maandazi...tehe tehe tehe!

Only kama nitakuwa nimejihakikishia mwenyewe kuwa hayo maandazi nayo hayana sumu. Sitaki kuwadhuru my neighbours.

" The rule that you are to love your neighbour becomes in law, you must not injure your neighbour; and the lawyer's question, Who is my neighbour? receives a restricted reply. You must take reasonable care to avoid acts or omissions which you can reasonably foresee would be likely to injure your neighbour. Who, then, in law, is my neighbour? The answer seems to be – persons who are so closely and directly affected by my act that I ought reasonably to have them in contemplation as being so affected when I am directing my mind to the acts or omissions which are called in question" - per Lord Atkin in Donoghue v Stevenson [1932] UKHL 100
 
Unataka nitoe opinion kuhusu oil chafu?

Hujui maana ya oil chafu mpaka kutaka opinion?

Sidhani kama Watanzania tumekuwa vilaza hivyo mpaka kata opinion kama oil chafu inafaa kwa matumizi.

Mkuu EMT, mbona unakuwa mkali ilhali hukuelewa ulichoulizwa !!! maneno "Opinion" na "option" sio sawa. Katika ushauri wangu nilikuelekeza utoa "option" yaani plan B (Mbadala wa oli chafu)itakayotumika kufukuza nyoka badala ya oil chafu kwa kuwa umesema inachafua mazingira na kila mtu anafahamu hilo. Sasa wewe bila kutafakari kilichoandkwa ukarukia na neno opinion. Na unaposema Watanzania, kumbuka kwamba wewe sio kiwakilishi cha Watanzania na wala sio Msemaji wao. Watu wengine sijui bila kutumia maneno makali na ya kuudhi hawawezi kuishi !!!
 
Usimshauri tu kuwa hii ni sumu usile, mwambie hii ni sumu kwa hiyo kula maandazi...tehe tehe tehe!

Mbona unarukia yasiyokuhusu ? Kwani neno opinion ni sawa na option ? Chukua muda, tafakari kabla ya kuingia kwenye mjadala.
 
photo-31838.jpg

Mamba wapo wa rangi nyingi kutofautiana kadiri ya mazingira wanayoishi. Huyu ni deadly, na ndio nyoka anauma kwa kukusudia na kupanga kabisa kufanya ubaya.

Green%20Mamba%202.JPG


Huyu Green Mamba ni hatari zaidi ya Black Mamba, uzuri ni kwamba huishi kwenye misitu mikubwa na amwe hakai karibu na mazingira yenye binadamu. Huyu ni tofauti na hawa nyoka wa kijani wanaokaa kwenye miti hata majumbani, huyu ni mkubwa na anaruka mti mmoja hadi mwingine kwa namna ya ajabu. Black Mamba haishi kwenye miti, yeye hupendelea vichuguu kama Cobra


Huyu mbona anafanana saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana na EGYPTIAN COBRA???????????????????????
 
Naombeni nami pia ,mniambie dawa ya kufukuza fuko shambani
 
Back
Top Bottom