Habari ya Uzima wanajamvi. Natumai wengi wetu, Mungu wetu wa Rehema ametuvusha Salama kufika mwaka 2023. Jambo la Kumshukuru sana Mungu.
Nijikite sasa kwenye Mada yetu husika wanajamvi. Kama ilivyoada kila mwanadamu huwa ana malengo yake husika ndani ya Mwaka mzima ili kujiweka juu zaidi katika maendeleo yake.
Mwaka 2023 ni mwaka ambao nimejishuhudia kabsa kwamba, miongo 3 kamili inatosha sasa kwa Kijana Mimi kuishi maisha ya Mume na Mke na kupunguza au kuacha kabisa tabia za uzinzi.
Ninamshukuru Mungu mchumba amenipatia na Hatua zote za awali zilikamilika mwishoni mwa mwaka 2022 (posa na Mahali) na Sasa kilichosalia ni Ndoa ili kusudi familia ya mke wangu mtarajiwa wanikabidhi Mke rasmi.
Ombi langu sasa, Ninaomba Ushauri wenu wa mawazo kwa wale ambao wamefanikiwa kufunga ndoa: Ni hatua gani napaswa kuzifuata sasa ili michakato yote iweze kwenda sawa? Mpaka sasa sijajua wapi naanzia na wapi namalizia!
List ya wanakamati watakaonisaidia hili swala ninayo kichwani na bila shaka hakuna atakayenigomea kwa hao wote.
Swala la kadi za harusi sijajua naliandaaje, je ni kwamba nikaripoti kanisani kwanza ili nijue muda wa harusi ndipo niandae kadi za harusi au niandae kwanza kwa utashi wangu na kuzigawa kwa watu watakaonishika mkono kwa hilo?
Najikuta nachanganyikiwa sana Tafadhali kwa mliofunga ndoa hivi karibuni na mnafahamu hatua zote mlizopitia naomba tusaidieni kimawazo ili kusudi sisi wageni tupate kunufaika katk Hili na tuje kuwasaidia wengine.
Tusaidiane ili kasherehe kawe kazuri nisije nikamuaibisha Muhaya wangu na familia yake.
NB: Ndoa kwa mipango yangu ni mwezi wa sita (6).
Mada nzuri sana,,
Mimi ni Roman Catholic,na Mungu akisaidia alhamis ya tarehe 12 january ntafunga ndoa na mchumba wangu,na leo hii ni send-off ya mchumba wangu..
Hapa naongelea rc lkn najua rc na Lutheran tunaingiliana kwenye mambo mengi,kwanza nliwataarifu wazazi wangu kwamba nmepata bint hvyo nahtaji kwenda kujitambulisha hvyo nliwaeleza wazee nyumbani kwa bint na process za posa zikaanza na baadae mahari na kuvalisha pete ya uchumba,kwa wachaga mahari huwa yanalipwa na mzazi ila unaweza kuangalia status ya mzee ukampiga tafu ili jambo liende.
*ukimaliza hapo utaita watu wako wa karibu ili uweze kujiandaa na hatua inayofuata(ndoa),hapo mtakaa kikamati na utakaa na wazoefu wa ndoa na kusimamia ndoa thn mtapanga mtafunga lini ndoa,kuandaa budget na kila mtu kutoa pledge zake,(hyo ni siku ya kwanza) baada ya hapo kila mtu ataondoka akiwa amepewa majukumu yako,mf-wewe utapewa task ya kwenda kanisan kuomba ndoa kutokana na tarehe mliyokubaliana na wengine wataenda kutafuta ukumbi na bei na wengine watafatilia maswala ya vinywaji mc n.k.
*kikao cha pili mtakutana lbd baada ya week ambapo kila mtu ataleta majibu ya alichotumwa mfano wewe utaleta majibu ya kanisani,wengine mc,wengine ukumbi n.k(naimani kama ukipata kamati nzuri kuanzia hapo mambo yataenda smoothly)
*kama wewe n roman inatakiwa uwe unaenda jumuia maana jumuia ndio itatoa barua kukuthibitishia wewe n mwenzao,na wife pia thn kama hajapata kipaimara or komunio atapangiwa siku ya kupata kipaimara.
MUHIMU-kumvalisha mchumba ako kuanzia,juu mpaka chini na pamoja na wewe na saloon siku ya ndoa pamoja na Pete
Ni jukumu lako,kumvalisha mchumba wako siku ya mahari yaani ni jukumu lako,kugharimikia shughuli yote siku ya kutoa mahari ni jukumu lako,,hii kitu nmeiandika kwa mkazo maana n gharama kubwa usije ukalia ukahisi umesusiwa kumbe ni jukumu lako.
Mwisho,,,karibu nafunga ndoa January 12,,karibu upate mc na dj na mwangaza.