MSAADA: Michakato na hatua za ndoa mpaka kukamilika

MSAADA: Michakato na hatua za ndoa mpaka kukamilika

Kama unajiweza kiuchumi tafuta event planner. If not, huna rafiki yoyote alieoa? Mchumba ako hana marafiki walioolewa? Mnaweza mkashirikiana wenyewe then kwenye kamati kila mtu anakaa na kamati yake
 
Njo nikutengenezee hizo kadi za harusi na kukushutia sherehe yako kwa bei nzuri zaid...
 
Hapa n wewe na mwenzako. Unataka li kitu kuubwa au unataka small n sweet?
Kwa uchumi ulivo, wachana na masinemarie.
Tafuta hela kias hapo, then ttafta hata bustani hapo kwenu, watu wale mchele hata kilo 50 na kilo chache za ng'ombe yaishe.
Tofaut na hapo subiri waanze kukupelekesha. Ukikubali ukweni wakupeleke hatua za mwanzo hata ndoani watakupelekesha pia.
Yoyote atakaekupa stress mwambie aje umuoe yeye maana ana kiherehere
 
Sisi tulioingia na tukatoka tunajua chungu nantamu .Andaa 6m (3m iwe bajeti yako 3m michanngo au ahadi ) inatosha kukamilisha mchakato wako watu watakaula na kushiba .
 
Kama unajiweza kiuchumi tafuta event planner. If not, huna rafiki yoyote alieoa? Mchumba ako hana marafiki walioolewa? Mnaweza mkashirikiana wenyewe then kwenye kamati kila mtu anakaa na kamati yake
Wapo wengi japo sikuona vbaya kuanzia humu nione namudu kiasi gani bila kusumbua sana watu. Japo majibu ya wengi niliyokutana nayo yamenikata maini hahah
 
Hapa n wewe na mwenzako. Unataka li kitu kuubwa au unataka small n sweet?
Kwa uchumi ulivo, wachana na masinemarie.
Tafuta hela kias hapo, then ttafta hata bustani hapo kwenu, watu wale mchele hata kilo 50 na kilo chache za ng'ombe yaishe.
Tofaut na hapo subiri waanze kukupelekesha. Ukikubali ukweni wakupeleke hatua za mwanzo hata ndoani watakupelekesha pia.
Yoyote atakaekupa stress mwambie aje umuoe yeye maana ana kiherehere
Nakuelewa vizuri Boss
 
Wapo wengi japo sikuona vbaya kuanzia humu nione namudu kiasi gani bila kusumbua sana watu. Japo majibu ya wengi niliyokutana nayo yamenikata maini hahah
Watu wa humu hujawajua? Kwanza watakwambia usioe ndoa ni mzigo ila ye yumo anakomaa mwaka wa 20 kwenye ndoa yake. Sa skia, inategemea we unataka sherehe ya aina gani.

At least uwe na idea ya ukumbi unaoutaka, kaulize bei, mpambaji ukitafuta instagram utalia, nenda kwenye kumbi husika lazima wanawajua wapambaji. Ukimpata mpambaji atakwambia wa keki na wa chakula huwa wanajuana. Ila ukiingia kuwasaka insta jua harusi yako itadai milioni za kutosha.

Yani inshort hawa vendors wanajuana. Watu wa kadi ukiingia kariakoo huwakosi. Kikubwa uwe na rafiki wa kukusaidia lasivyo utablow. Hekaheka za harusi usiombe.
 
Ushauri wangu ni kwamba nenda kanisani kajue taratibu za mafundisho ya ndoa kawaida ni mwezi mmoja, wajue wadhamini wako wa ndoa, alafu panga siku ya ndoa yako. Kingine hebu jipange sikuhizi ukitaka sherehe nzuri isio na lawama achana na mambo ya kamati watakuyeyusha hela nyingi inaishia kwenye kamati vikao visivyo na mipango ww kichwani kwako jua kwamba sherehe ni kula na kunywa. Mambo ya mziki na burudani zingine mc anaweza simamia vizuri tu wapo ma mc wana kujana camera man dj sasa inakua nafuu.

Epuka sana kuchangisha watu kwanza inakera na pili sherehe inakua ya kufakamia nimetoa 100k yangu nataka ninywe beer mpka nitosheke ila ukiamua kubajet watu wanywe beer 4 kila mmoja unaweza vizur tu na sherehe fanya ya watu 100 mpka 120 ndugu jamaa na rafiki kadhaa hao ndugu pia sio lazima waje wote wawepo wale wa muhimu kuwakilisha familia upande wako na wa mkeo.

Ni ushauri wangu usiige kila kitu kisa umekikuta unafanya kulingana na uwezo wako na nafsi yako inapenda nini.

Usije ukawa wale wenye 3m alafu anataka sherehe ya 30m utachekesha umati
 
Nimesoma vizuri uzi wako. Kumbe unauliza pia na process za kanisani? We ni dhehebu gani? Kama ni kkkt unaenda kanisani kwako unakosali unawaambia. Watakuuliza maswali. Utaandikisha ndoa hapo kanisani kwenu au usharikani kwenu then kunakuwa na seminar ya wanandoa ambapo utaenda na barua ya utambulisho kutoka usharikani kwenu.

Baada ya hapo unapeleka barua dayosisi kutoka huko utapewa mlolongo mzima. Kama wewe ni Roman catholic sijui ila anzia kanisani kwenu pia utapewa mlolongo. Na uwaambie mwenzako kama ni dhehebu moja na wewe ama vipi. Mmepokea kipaimara? Vyote hivyo vinatakiwa.

Na kingine wapange kabisa wadhamini wa ndoa, watatakiwa kuwa na barua kutoka kwenye usharika wao. Watakua wanahudhuria semina pia. Sijajua kwa madhehebu mengine utaratibu ukoje
 
Habari ya Uzima wanajamvi. Natumai wengi wetu, Mungu wetu wa Rehema ametuvusha Salama kufika mwaka 2023. Jambo la Kumshukuru sana Mungu.

Nijikite sasa kwenye Mada yetu husika wanajamvi. Kama ilivyoada kila mwanadamu huwa ana malengo yake husika ndani ya Mwaka mzima ili kujiweka juu zaidi katika maendeleo yake.

Mwaka 2023 ni mwaka ambao nimejishuhudia kabsa kwamba, miongo 3 kamili inatosha sasa kwa Kijana Mimi kuishi maisha ya Mume na Mke na kupunguza au kuacha kabisa tabia za uzinzi.

Ninamshukuru Mungu mchumba amenipatia na Hatua zote za awali zilikamilika mwishoni mwa mwaka 2022 (posa na Mahali) na Sasa kilichosalia ni Ndoa ili kusudi familia ya mke wangu mtarajiwa wanikabidhi Mke rasmi.

Ombi langu sasa, Ninaomba Ushauri wenu wa mawazo kwa wale ambao wamefanikiwa kufunga ndoa: Ni hatua gani napaswa kuzifuata sasa ili michakato yote iweze kwenda sawa? Mpaka sasa sijajua wapi naanzia na wapi namalizia!

List ya wanakamati watakaonisaidia hili swala ninayo kichwani na bila shaka hakuna atakayenigomea kwa hao wote.

Swala la kadi za harusi sijajua naliandaaje, je ni kwamba nikaripoti kanisani kwanza ili nijue muda wa harusi ndipo niandae kadi za harusi au niandae kwanza kwa utashi wangu na kuzigawa kwa watu watakaonishika mkono kwa hilo?

Najikuta nachanganyikiwa sana Tafadhali kwa mliofunga ndoa hivi karibuni na mnafahamu hatua zote mlizopitia naomba tusaidieni kimawazo ili kusudi sisi wageni tupate kunufaika katk Hili na tuje kuwasaidia wengine.

Tusaidiane ili kasherehe kawe kazuri nisije nikamuaibisha Muhaya wangu na familia yake.

NB: Ndoa kwa mipango yangu ni mwezi wa sita (6).
Hongera. Kwanza kwa mila na desturi nyingi za kiafrika, ukishaposa ukakubalika na kulipa mahari, tayari umeshaoa. Unachokitaka wewe ni uthibitisho wa kidini/serikali na sherehe.
 
Hongera. Kwanza kwa mila na desturi nyingi za kiafrika, ukishaposa ukakubalika na kulipa mahari, tayari umeshaoa. Unachokitaka wewe ni uthibitisho wa kidini/serikali na sherehe.
Sahihi kabisa mkuu ni hicho tu
 
Nimesoma vizuri uzi wako. Kumbe unauliza pia na process za kanisani? We ni dhehebu gani? Kama ni kkkt unaenda kanisani kwako unakosali unawaambia. Watakuuliza maswali. Utaandikisha ndoa hapo kanisani kwenu au usharikani kwenu then kunakuwa na seminar ya wanandoa ambapo utaenda na barua ya utambulisho kutoka usharikani kwenu.

Baada ya hapo unapeleka barua dayosisi kutoka huko utapewa mlolongo mzima. Kama wewe ni Roman catholic sijui ila anzia kanisani kwenu pia utapewa mlolongo. Na uwaambie mwenzako kama ni dhehebu moja na wewe ama vipi. Mmepokea kipaimara? Vyote hivyo vinatakiwa.

Na kingine wapange kabisa wadhamini wa ndoa, watatakiwa kuwa na barua kutoka kwenye usharika wao. Watakua wanahudhuria semina pia. Sijajua kwa madhehebu mengine utaratibu ukoje
Nadhani katika wote walionielewa wewe utakuwa umenielewa zaidi Boss wangu ndicho kikubwa haswaa nilikuwa nakihitaji. Ukiachilia mbali gharama nilihitaji hatua kama hizi ili nitathmini mm mwenyewe uzito wake kwa maana binafsi napenda sana Ndoa ya mchana kweupe kanisani kuliko kujinyakulia tu
 
Back
Top Bottom