MSAADA: Michakato na hatua za ndoa mpaka kukamilika

Hongera na kila la kheri.
 
Mahali tayri ila tu wazazi hawako tayari binti yao atoke pasi harsi
Hao wakwe zako basi hawajitambui. Jambo la muhimu ni kuposa tu kwao. Hayo mengine ni hiyari yako ufanye au kutofanya.

Kuposa ni mila ya kiafrika, na ndio halfa muhimu ya kuomba ruhusa ya wazazi kumchukua binti yao na kuanza nae maisha.

Hizo nyingine ndoa ya kanisani au msikiti ni halfa za kiimani na ndio maana hazihusishi watu wengine isipokuwa bibi na bwana yaani wanandoa mbele ya padre au sheikh.

Harusi kwa maana ya sherehe hiyo haina uzito sana maana ni shughuli ya kusheherekea tukio la ndoa na ndio maana huwa ndani ya masaa machache sana ingawa maandalizi yake huchukua miezi.

So kalipe posa kwanza na unaweza kuarrage ndoa ya gharama nafuu yaani ila ya kuwa na padre au mchungaji au sheikh na watu wachache watakaohudhuria then shughuli ifanyike then baada ya hapo mambo ya sherehe ya harusi unaweza ya ditch tu. Kwasasa hali ya uchumi si nzuri sana.

Wanajamii hawana pesa hali zao ni tete na wanapambana na gharama za maisha. Sasa wewe unaweza pelekea mtu kadi ya mchango na yeye anazo kama 10. Kadi 10 mara 50,000 au 100,000 huo ni mziki mnene. Nadhani kama utataka hili jambo liende vema itabidi at least uwe na 70% au 80% ya budget ili uweze kumudu gharama.
 
Kama sio bikira usimpe hadhi ya ndoa yenye sherehe, vuta maisha yaendelee. Sherehe za ndoa sio kwa wazinzi na makahaba.
 
Mada nzuri sana,,

Mimi ni Roman Catholic,na Mungu akisaidia alhamis ya tarehe 12 january ntafunga ndoa na mchumba wangu,na leo hii ni send-off ya mchumba wangu..

Hapa naongelea rc lkn najua rc na Lutheran tunaingiliana kwenye mambo mengi,kwanza nliwataarifu wazazi wangu kwamba nmepata bint hvyo nahtaji kwenda kujitambulisha hvyo nliwaeleza wazee nyumbani kwa bint na process za posa zikaanza na baadae mahari na kuvalisha pete ya uchumba,kwa wachaga mahari huwa yanalipwa na mzazi ila unaweza kuangalia status ya mzee ukampiga tafu ili jambo liende.

*ukimaliza hapo utaita watu wako wa karibu ili uweze kujiandaa na hatua inayofuata(ndoa),hapo mtakaa kikamati na utakaa na wazoefu wa ndoa na kusimamia ndoa thn mtapanga mtafunga lini ndoa,kuandaa budget na kila mtu kutoa pledge zake,(hyo ni siku ya kwanza) baada ya hapo kila mtu ataondoka akiwa amepewa majukumu yako,mf-wewe utapewa task ya kwenda kanisan kuomba ndoa kutokana na tarehe mliyokubaliana na wengine wataenda kutafuta ukumbi na bei na wengine watafatilia maswala ya vinywaji mc n.k.

*kikao cha pili mtakutana lbd baada ya week ambapo kila mtu ataleta majibu ya alichotumwa mfano wewe utaleta majibu ya kanisani,wengine mc,wengine ukumbi n.k(naimani kama ukipata kamati nzuri kuanzia hapo mambo yataenda smoothly)

*kama wewe n roman inatakiwa uwe unaenda jumuia maana jumuia ndio itatoa barua kukuthibitishia wewe n mwenzao,na wife pia thn kama hajapata kipaimara or komunio atapangiwa siku ya kupata kipaimara.

MUHIMU-kumvalisha mchumba ako kuanzia,juu mpaka chini na pamoja na wewe na saloon siku ya ndoa pamoja na Pete
Ni jukumu lako,kumvalisha mchumba wako siku ya mahari yaani ni jukumu lako,kugharimikia shughuli yote siku ya kutoa mahari ni jukumu lako,,hii kitu nmeiandika kwa mkazo maana n gharama kubwa usije ukalia ukahisi umesusiwa kumbe ni jukumu lako.

Mwisho,,,karibu nafunga ndoa January 12,,karibu upate mc na dj na mwangaza.
 
Shirikisha ndugu zako waliokwisha oa...
 
Usitegemee sana hela za watu siyo zote zinatolewa kwa moyo mkunjufu....wengi hutoa kwa kinyongo na maneno juu.....kandoa katabutuliwa keshokutwa tu
Kama anajiweza afanye sherehe ndgo ndgo isiyohusisha watu wengi..

Ila mkewe sidhani kama atakubali hilo
 
Safi,umeeleza vizuri sana mkuu
 
Inategemea na wewe umeamua nini. Kama unataka mkeo apate furaha na wazazi wake waridhike fanya matakwa yao..lakin kama unaweza kusimama kiume na kufanya maamuzi ili baada ya ndoa muweze kuishi fresh kwa muda ni wewe tu.
 
Ubarikiwe sana mtu wa Mungu
 
Umesema vizuri sana mkuu
 
HAPA SASA UMEJIBU MASWALI YANGU YOTE. UBARIKIWE SANA MKUU, NIMEFAHAMU SASA WAPI KWA KUANZIA NA WAPI KWA KUISHIA
 
KATAA NDOA JALI AFYA YAKO YA AKILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…