Msaada: Mke wangu ana tatizo la uzazi

Msaada: Mke wangu ana tatizo la uzazi

Nampenda sanaa na tunaendelea kupambana kutafuta mtoto ata tuzeeke.

Nimejaribu kwenda hospital mbili za rufaa zenye hao maspecialist wanampima kisha wanasema hana tatizo.
Ndoa siku zote mtoto wa kwanza unaona kama unachelewa. Bado kabisa wala usipaniki. Usichoke kuona dr na kuelezea tatizo lako. Wakati mwingine unawezakupita hata hospital 5 kbla hujapata suluhisho.
 
Nimeishi na mke wangu kwa mwaka mmoja na nusu.

Alipata ujauzito mara ya kwanza katika maisha yake, ule ujauzito ulidumu kwa miezi 3 kisha ukatoka.

Akapata ujauzito kwa mara ya pili huu ulikaa kwa muda wa miezi 2 ukatoka.

Akapata ujauzito kwa mara ya tatu huu ulikaa kwa muda mwezi mmoja tu ukatoka yani tulivyopima ujauzito haikupita siku 3 ukatoka.

Tukienda hospitali zenye specialist wa masuala ya uzazi wanampima na wanasema hana tatizo lolote.

Sasa imekuwa ngumu kupata ujauzito na sijui tatizo ni nini? Yaani kila mwezi anaonesha dalili za ujauzito ila ukipima hamna kisha anaingia kwenye siku zake.
Jaribu pia maombi kwa imani yako (kama unaamini majibu mazuri mtayaona)
 
Kama kasoma chuo kikuu, chunguza pia mienendo yake kipindi kile. Wengine waliyoyafanya,yamekuwa chanzo cha tatizo hilo
 
Ndoa siku zote mtoto wa kwanza unaona kama unachelewa. Bado kabisa wala usipaniki. Usichoke kuona dr na kuelezea tatizo lako. Wakati mwingine unawezakupita hata hospital 5 kbla hujapata suluhisho.
Sawa Mkuu
 
Umeenda hospital za maana ama kwa wanesi?

Nenda hospital za kubwa ukapimwe uterus itakuwa Iko week inahitaji kufungwa/kukazwa ama apate full bed rest.
Pole sana ila mpende mkeo ndio huyo Mungu kakupa.

Kweli itakuwa kizazi kimelegea na pia asifanye kazi kabisa kipindi cha ujauzito iwe kula kulala tu ,aende kwa maspesholist watampa vidonge vya kukaza kizazi.
 
Au hormonal imbalance
Walimpima akaonekana yuko sawa, wakasema lamda kuta za uterus zake haziruhusu kuchimba ili kukaa mimba (implantation) so ikitokea akapata ujauzito niwahi akapewe dawa za kulainisha kuta ili mimba iweze kuchimba na kujishikiza vizuri kwenye uterus sasa shida tangu waseme hvyo ata mimba yenyewe haitokei yan anaweza akawa na dalili zote za mimba na hata kupitiliza siku zake kwa siku 2 ila ukipima hana mimba.
 
Wakati utafika tu atazaa...mwambie arelax
 
Kama kasoma chuo kikuu, chunguza pia mienendo yake kipindi kile. Wengine waliyoyafanya,yamekuwa chanzo cha tatizo hilo
Kamasoma chuo ana shahada ,Ana miaka 27,na aliniambia hakuwahi kutumi njia zozote za uzazi ili isiwe ngumu kutafuta mtoto atakapolewa na tulipooana tulikaa mwezi mmoja tu akapata ujauzito ingawa ulitoka baada ya miezi 3.
 
Nawashauri muende Kwa mwamposa mkaombewe ,Kwa Imani mtapata watoto
 
Nampenda sanaa na tunaendelea kupambana kutafuta mtoto ata tuzeeke.

Nimejaribu kwenda hospital mbili za rufaa zenye hao maspecialist wanampima kisha wanasema hana tatizo.
Hospitali za rufaa zina speshelist ,uko mkoa gani tukulengeshe

Nakuomba umuwaishe Kwa dokta kapona ,anapatikana chanika ,shuka kituo kinaitwa ccm ,uliza bodaboda Kwa dokta kapona , mkeo anenda kupona ,labda awe kalogwa na x wake

Na
Kama niwakulogwa tafadhari wasiliana na mshana JR ,unaweza pewa chakufanya

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Je ana tabia ya kula kula madawa kila atakaposikia tumbo linamuuma ama shida nyingine bila kuenda hospital? Kuna wanawake akiumwa kidogo tu bila kwenda hospital anakimbilia kwenye ma fragil na Cipro apo mimba lazima itoke
 
Back
Top Bottom