Msaada: Mke wangu ana tatizo la uzazi

Msaada: Mke wangu ana tatizo la uzazi

Whk

Member
Joined
Oct 1, 2020
Posts
77
Reaction score
76
Nimeishi na mke wangu kwa mwaka mmoja na nusu.

Alipata ujauzito mara ya kwanza katika maisha yake, ule ujauzito ulidumu kwa miezi 3 kisha ukatoka.

Akapata ujauzito kwa mara ya pili huu ulikaa kwa muda wa miezi 2 ukatoka.

Akapata ujauzito kwa mara ya tatu huu ulikaa kwa muda mwezi mmoja tu ukatoka yani tulivyopima ujauzito haikupita siku 3 ukatoka.

Tukienda hospitali zenye specialist wa masuala ya uzazi wanampima na wanasema hana tatizo lolote.

Sasa imekuwa ngumu kupata ujauzito na sijui tatizo ni nini? Yaani kila mwezi anaonesha dalili za ujauzito ila ukipima hamna kisha anaingia kwenye siku zake.
 
Umeenda hospital za maana ama kwa wanesi?

Nenda hospital za kubwa ukapimwe uterus itakuwa Iko week inahitaji kufungwa/kukazwa ama apate full bed rest.
Pole sana ila mpende mkeo ndio huyo Mungu kakupa.
Nampenda sanaa na tunaendelea kupambana kutafuta mtoto ata tuzeeke.

Nimejaribu kwenda hospital mbili za rufaa zenye hao maspecialist wanampima kisha wanasema hana tatizo.
 
Nimeishi na mke wangu kwa mwaka mmoja na nusu.

Alipata ujauzito mara ya kwanza katika maisha yake ule ujauzito ulidumu kwa miezi 3 kisha ukatoka.

Akapata ujauzito kwa mara ya pili huu ulikaa kwa muda wa miezi 2 ukatoka.

Akapata ujauzito kwa mara ya tatu huu ulikaa kwa muda mwezi mmoja tu ukatoka yani tulivyopima ujauzito haikupita siku 3 ukatoka.

Tukienda hospitali zenye specialist wa maswala uzazi wanampima na wanasema hana tatizo lolote.

Sasa imekuwa ngumu kupata ujauzito na sijui tatizo ni nini?
Yani kila mwezi anaonesha dalili za ujauzito ila ukipima hamna.
Mnahitaji msaada wa kiroho hpo mkuu, hakuna njia nyingne
 
Nisikilize....
Wewe kunywa vidonge vya Vitamin C, kama 100gm kila siku, kwa muda mwezi mmoja, unaweza kuendelea. Mkeo akishika mimba aanze progestrone tablets sio chini ya miezi mitatu ya kwanza.
Mungu sio mwanadamu, mtapata watoto. Kila la heri
 
Back
Top Bottom